Serikali inafanya nini kuhusu wizi katika posta nchini Tanzania? Hata barua za kawaida zinaibiwa na kufunguliwa na wafanyakazi wa posta.
Nimewaandikia ndugu zangu mara nyingi na, kila mmoja wao, wamesema barua pamoja na picha nilizowatumia hazikuwafikia. Na wote wameniambia nisithubutu kuwatumia kitu chochote kupitia posta nchini Tanzania. Na mmoja wao amesema wananchi wengi wanasema itakuwa ni vizuri posta zikifungwa kwa sababu ya wizi huo ambao unaendelea kwa kasi.
Malalamiko hayo yanatoka sehemu zote za Tanzania. Ndugu zangu niliowaandikia wanaishi sehemu mbali mbali - Dar es Salaam, Mtwara, Iringa, Mbozi, Mwanza, Bukoba, Tabora, na Arusha.
Hakuna posta nchini ambayo haina wafanyakazi wanaoiba vitu mbali mbali - barua, vifurushi - vinavyotumwa kutoka n'gambo. Pia wana akili pungufu wanapofikiri kwamba kuna fedha katika barua hizo wanazozifungua.
Labda wananchi wakigoma kutumia posta, hatua zitachukuliwa kupambana na wizi huo.
Nimeishi n'gambo miaka michache (au mingi?) - zaidi ya kumi - na ni jambo la kukatisha tamaa kwa watu kama mimi tunaotaka kurudi nyumbani tunapoona serikali haifanyi chochote kurekebisha mambo - wizi, rushwa, mahongo, ufisadi na kadhalika.
Tutajengaje taifa letu? Kama Mwalimu alivyosema, "Tanzania itajengwa na wenye moyo."
Haitajengwa na wezi. Haitajengwa na wala rushwa au mahongo, na haitajengwa na mafisadi. Wamejaa serikalini na katika kila wizara na idara na sehemu mbali mbali kazini.
Halafu kuna viongozi wanashangaa kwa nini wananchi wengi hawataki kurudi nyumbani? Si Tanzania tu bali nchi zote katika bara letu.
Haisaidii sana! kuna aliyetuma simu na charger Tanzania(registered), baada ya muda alipata ujumbe kuwa mzigo wake umerudishwa kwa vile jina la aliyetumia halifanani na mmiliki wa adress.Ukituma mzigo au ukitumiwa mwambie anaekutumia atume as Registered(small parcels) atalipia a little bit extra lakini huo mzigo hautapotea coz kila anaeupokea atasign hadi ufike mkononi mwako.huwa natumia njia hii siku moja tu nilisahau nikatuma kawaida mzigo haukufika,inaelekea hata wafanyakazi wa posta wanaiba once wakijua mzigo sio registered.
kila kitengo kuna wezi duuh hii Tanzania imelaaniwaSerikali inafanya nini kuhusu wizi katika posta nchini Tanzania? Hata barua za kawaida zinaibiwa na kufunguliwa na wafanyakazi wa posta.
Nimewaandikia ndugu zangu mara nyingi na, kila mmoja wao, wamesema barua pamoja na picha nilizowatumia hazikuwafikia. Na wote wameniambia nisithubutu kuwatumia kitu chochote kupitia posta nchini Tanzania. Na mmoja wao amesema wananchi wengi wanasema itakuwa ni vizuri posta zikifungwa kwa sababu ya wizi huo ambao unaendelea kwa kasi.
Malalamiko hayo yanatoka sehemu zote za Tanzania. Ndugu zangu niliowaandikia wanaishi sehemu mbali mbali - Dar es Salaam, Mtwara, Iringa, Mbozi, Mwanza, Bukoba, Tabora, na Arusha.
Hakuna posta nchini ambayo haina wafanyakazi wanaoiba vitu mbali mbali - barua, vifurushi - vinavyotumwa kutoka n'gambo. Pia wana akili pungufu wanapofikiri kwamba kuna fedha katika barua hizo wanazozifungua.
Labda wananchi wakigoma kutumia posta, hatua zitachukuliwa kupambana na wizi huo.
Nimeishi n'gambo miaka michache (au mingi?) - zaidi ya kumi - na ni jambo la kukatisha tamaa kwa watu kama mimi tunaotaka kurudi nyumbani tunapoona serikali haifanyi chochote kurekebisha mambo - wizi, rushwa, mahongo, ufisadi na kadhalika.
Tutajengaje taifa letu? Kama Mwalimu alivyosema, "Tanzania itajengwa na wenye moyo."
Haitajengwa na wezi. Haitajengwa na wala rushwa au mahongo, na haitajengwa na mafisadi. Wamejaa serikalini na katika kila wizara na idara na sehemu mbali mbali kazini.
Halafu kuna viongozi wanashangaa kwa nini wananchi wengi hawataki kurudi nyumbani? Si Tanzania tu bali nchi zote katika bara letu.
Nimetumiwa parcel kwa EMS tangu trh 24 sept, mpaka sasa sijaipata. Naambiwa bado haijafika. Ngoja mie nivute subira kidogo.
3days, maximum 7days. Bt mm leo ni siku ya 9.