Wafanyakazi jijini Dar, leo wameandamana kumpongeza Rais Magufuli kuhusu kikokotoo

Wafanyakazi jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Januari 03,2019 wameandamana kwa lengo la kumpongeza Rais John Magufuli kwa uamuzi wake wa kufuta kikokotoo kipya cha mifuko ya hifadhi za jamii na kurejesha cha zamani.
View attachment 984778
Maandamano hayo ambayo yameanzia ofisi za Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), Mnazi Mmoja jijini humo hadi viwanja vya Mnazi Mmoja wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kumpongeza Rais Magufuli, yamepokewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva.

Akizungumza na waandamanaji hao, Lyaviva ametoa rai kwa wafanyakazi wa umma nchini kufanya kazi kwa uadilifu na kuwahudumia wananchi bila upendeleo.

Aidha amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo.

Amesema wapo baadhi ya watumishi wa Serikali wanaochelewesha huduma kwa wananchi kwa makusudi hali inayosababisha malalamiko.

“Zingatieni nidhamu ya utumishi na utendaji, bahati nzuri kila taasisi ina mfumo wake wa utendaji kazi zingatieni hiyo mifumo, furaha hii ya kikokotoo haimanishi mjisahau katika kuwahudumia wananchi,” amesema.

Akizungumzia kuhusu tamko la Rais Magufuli la kusitisha kikokotoo walichokiita kandamizi amesema uamuzi huo uwe chachu ndani ya mioyo ya wafanyakazi hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma zaidi.

Akisoma risala iliyoandaliwa na wafanyakazi hao, Katibu wa kamati za wanawake wa Tucta, Jenijely James amesema kikokotoo hicho kilichorejeshwa kina mafao bora katika sekta ya umma.

“Ni wazi kutokana na malipo duni ya mishahara kwa watumishi wa umma, wengi wao hawakuweza kujenga makazi bora wakati wa utumishi wao hivyo matarajio yao yote yalikuwa kwenye malipo ya mkupuo kwa kanuni bora za waliyojiunga na hatukujiandaa kisaikolojia kuhusu kikokotoo kipya,” ameongeza.

Desema 28, 2018, Rais Magufuli alikutana na Tucta, viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na wadau wengine Ikulu jijini Dar es Salaam na kusitisha kikokotoo kipya na kurudisha cha zamani ambacho kitatumika hadi 2023.

Wafanyakazi Dar waandamana kumpongeza Rais Magufuli

MAONI BINAFSI.
—Hao kweli ni wafanyakazi ambao tangu July, 2016 hawajapata increment wala kupandishwa mshahara?

—Hao kweli ni wafanyakazi ajira mpya 2012, 2013, 2014 ambao hawajapanda daraja?

—Hao kweli ni wafanyakazi waliotakiwa kupanda kwa mara nyingine 2016, 2017 na 2018?

Sitaki kuamini kama wameandamana kwa ridhaa yao. Je, siku hayo hapo juu yakitekelezwa, tutarajie maandamano nchi nzima?
View attachment 984783
View attachment 984784
Nakuhakikishia Hakuna aliyemtumishi wa Umma yupo miongoni mwa hao! Hao ni Lumumba Buku 7. I swear, hayupo Mtumishi wa Umma hapo!
 
Bado kuna wajinga sana Nchi hii, haijarishi wana nyadhifa zipi Serikalini lkn mambo wanayoyafanya hudhihirisha ujinga mkubwa walionao! Hata kama umelazimishwa, Mtu Mzima mwenye weledi na Fikra Pevu, hauwezi kukubali kutenda mambo yakujidhalilisha kama haya ya kuandamana kumpongeza Mtu/watu wale wale waliotunga kanuni za kinyonyaji za kuwanyonya Wafanyakazi na Familia zao halafu, Watu makini wamewasaidia kuipigia kelele Serikali ile ile iliyokusudia kufanya unyonyaji kisha ikabadili msimamo, kwa mshangao mkubwa eti hao Mbululaz wanaandamana kumpongeza Mkuu wa Watu wasiyojulikana!!

Haijalishi, Mfanyakazi una mahaba ya kiasi gani na CCM, inapokuja swala la maslahi na haki yako kupokonywa, ni lzma weledi utumike lkn kwa kufanya maigizo haya, nikuonesha udhaifu mkubwa wa kutojua kutafakari mambo muhimu kwa upana wake!
Viongozi wa TUCTA nao ni sehemu kubwa ya wasariti wa Watanzania, hususani wafanyakazi. Sikuona mantiki ya wao kujihusisha na Maigizo haya ya maandamano yenye sura mbili:

1. Yakuwaangamiza zaidi wafanyakazi kifikra na kiuchumi.
2. Yakujihusisha na Propaganda za siasa zenye lengo lile lile la kuwahadaa Wafanyakazi.
Maoni yangu juu yaTUCTA, hivi vyama vya Wafanyakazi chini ya utawala wa CCM, havina tija hata kidogo,vifutwe tu
 
Wafanyakazi jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Januari 03,2019 wameandamana kwa lengo la kumpongeza Rais John Magufuli kwa uamuzi wake wa kufuta kikokotoo kipya cha mifuko ya hifadhi za jamii na kurejesha cha zamani.
View attachment 984778
Maandamano hayo ambayo yameanzia ofisi za Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), Mnazi Mmoja jijini humo hadi viwanja vya Mnazi Mmoja wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kumpongeza Rais Magufuli, yamepokewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva.

Akizungumza na waandamanaji hao, Lyaviva ametoa rai kwa wafanyakazi wa umma nchini kufanya kazi kwa uadilifu na kuwahudumia wananchi bila upendeleo.

Aidha amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo.

Amesema wapo baadhi ya watumishi wa Serikali wanaochelewesha huduma kwa wananchi kwa makusudi hali inayosababisha malalamiko.

“Zingatieni nidhamu ya utumishi na utendaji, bahati nzuri kila taasisi ina mfumo wake wa utendaji kazi zingatieni hiyo mifumo, furaha hii ya kikokotoo haimanishi mjisahau katika kuwahudumia wananchi,” amesema.

Akizungumzia kuhusu tamko la Rais Magufuli la kusitisha kikokotoo walichokiita kandamizi amesema uamuzi huo uwe chachu ndani ya mioyo ya wafanyakazi hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma zaidi.

Akisoma risala iliyoandaliwa na wafanyakazi hao, Katibu wa kamati za wanawake wa Tucta, Jenijely James amesema kikokotoo hicho kilichorejeshwa kina mafao bora katika sekta ya umma.

“Ni wazi kutokana na malipo duni ya mishahara kwa watumishi wa umma, wengi wao hawakuweza kujenga makazi bora wakati wa utumishi wao hivyo matarajio yao yote yalikuwa kwenye malipo ya mkupuo kwa kanuni bora za waliyojiunga na hatukujiandaa kisaikolojia kuhusu kikokotoo kipya,” ameongeza.

Desema 28, 2018, Rais Magufuli alikutana na Tucta, viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na wadau wengine Ikulu jijini Dar es Salaam na kusitisha kikokotoo kipya na kurudisha cha zamani ambacho kitatumika hadi 2023.

Wafanyakazi Dar waandamana kumpongeza Rais Magufuli

MAONI BINAFSI.
—Hao kweli ni wafanyakazi ambao tangu July, 2016 hawajapata increment wala kupandishwa mshahara?

—Hao kweli ni wafanyakazi ajira mpya 2012, 2013, 2014 ambao hawajapanda daraja?

—Hao kweli ni wafanyakazi waliotakiwa kupanda kwa mara nyingine 2016, 2017 na 2018?

Sitaki kuamini kama wameandamana kwa ridhaa yao. Je, siku hayo hapo juu yakitekelezwa, tutarajie maandamano nchi nzima?
View attachment 984783
View attachment 984784

Ukiwaangalia sura zao wanaonekana kama wale ambao kijijini kwetu tunawaita "NDONDOCHA"!
 
Hivi DSM nzima wafanyakazi ni hao tu???? Au tutaambiwa wengi walishaamia Dodoma au hawajarejea kutoka kwenye kuhesabiwa makwao???

Ni Makada wa ccm wameletwa kuigiza ili kuhadaa umma. Nakumbuka maigizo ya wakulima wa korosho, leo hii wanalia hawaamini macho yao.
 
Heee!!! Mambosasa yuko wapi jamani? Mbona maandamano yamekatazwa nchi hii ili tufanye kazi? Hawa mbona wanataka kumzuia Rais wetu asitekeleze majukumu yake? Na pia kama walivyosema kwa hekima kabisa leo asubuhi, Hassan ngoma na mwenzake Sam Sasali wa Clouds 360, mtu anayedai haki ya kuandamana, akumbuke kwamba wengine wasiotaka kuandamana nao wana haki, asije akawaletea "fujo". Sasa hawa wanaachiwa tu wanaandamana? WANAANDAMANA NCHI YA MAGUFULI??? Mambosasa upo wapi? Likizo ya Mwaka mpya/
 
Hah hah! Wameandamana siku/saa ya kazi? Nani kawaruhusu? Wamepata mpaka mgeni rasmi? Sidhani kama hao wanawakilisha wafanyakazi wote. Hawajaandamana wakati sheria na kanuni zilipobadilishwa ili kuvipinga, ila wanaandamana kupongeza kwa kikokotozi kurudishwa kama kilivyokuwa awali. Hawataki kujua hali ya mifuko ya mafao yao, wanafurahia kikokotozi tu. Kutawala Afrika raha sana.
 
Haya Maandamaano yanngekuwa sawa ikiwa haohao wangekuwa wameandamana au hata kuonyesha nia ya kuandamana kupinga kikokotoo kilichoondolewa, Yaani unapigana na tatizo kiume ukishinda unashangilia.
 
Hii itakuwa kwa hisani ya bwana yule asie na uwezo wa kuona mbali na mwenye uwezo mdogo wa kufikiri.

Hata kwenye koroshow tulishuhudia maandamano ya kutengeneza kama haya!

Hapo wakija kuhojiwa utasikia tulilazimishwa/tulipewa maagizo.

Kweli tumekabidhi nchi kwa.............!

Only fools will be comfortable in this country and who will have something to celebrate and never smart people.
Halafu wote ninaowaona hapo kikokotoo cha zamani kitakachodumu hadi 2023 hakiwahusu!
 
Back
Top Bottom