Wafanyabiashara washukuru fursa waliyoipata kupitia mkutano wa SADC

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
1566188703744.png


Wafanyabiashara ndogondogo, wachonga Vinyago na Wachoraji wa picha mbalimbali wanaouza bidhaa zao kwa wajumbe wa mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),katika barabara ya chuo cha IFM, wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, wakiwahudumia watu mbalimbali waliofika katika eneo hilo kwa ajili ya kununua mahitaji yao .Aidha wafanyabiashara hao wameishukuru Serikali kwa kuwapa fursa hiyo ya kuonesha na kuuzaa bidhaa zao huku wakizidi kujitangaza na kutanua wigo wa biashara zao.

1566188720774.png

1566188842317.png

1566188856887.png


1566188881368.png
 
Mimi nataka kujua in long run hawa wafanyabiashara wadogo wadogo watafaidika vipi na ujio/uwepo wa huu mkutano!
 
Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaelezwa kuleta neema nyingi kwa Watanzania hasa wafanyabiashara wakiwemo wauza vinyago.

Wafanyabiashara wengi wamedai kuwa mkutano huo umejenga sura mpya ya Tanzania kimataifa katika nyanja ya biashara, kwa sababu mazingira waliyojengewa yamefanikisha wao kupata connections nyingi kutoka nje ya nchi hali inayotoa mwelekeo na sura mpya kwa biashara zao.

Wafanyabiashara wa Vinyago katika soko la Mwenge wameishukuru serikali kwa kuthamini kazi zao za sanaa, na kwa kuweka mazingira mazuri ambayo yaliwawezesha wao kuonesha kazi zao kwa wageni, ambapo mbali na kuuza bidhaa zao kwa kiasi kikubwa lakini pia wamepata masoko ya nje hasa kwenye nchi wanachama na baadhi ya nchi kutoka nje ya jumuiya ya SADC. Wamesema kuwa wanamatumaini makubwa ya kufanikiwa katika biashara zao hasa katika kipindi hiki ambacho Rais Tanzania ndiye mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Wafanyabiashara wengine, akiwemo MO Dewji, wamesema, Agenda ya SADC ya kuwekeza katika Viwanda imeenda sambamba na dira ya nchi yetu ya kuwa Tanzania ya viwanda. Hivyo wana matumaini makubwa kuwa Tanzania itafanikiwa kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo. Wafanyabiasahara hao wakubwa wameweza kukutana na viongozi wa nchi wanachama na kujadiliana nao maeneo mbalimbali ya kiuwekezaji. SADC ilipitisha theme inayosema “A Conducive Environment of Inclusive and Sustainable Industrial Development, Increased Intra-Regional Trade and Job Creation” ambayo inabeba agenda ya viwanda.

Tuiombee nchi yetu chini ya Rais Magufuli, ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti wa SADC (2019/2020) ili tuweze kupata mafanikio yale ambayo tunayahitaji, na yeye kama kiongozi wetu amekuwa akituongoza huko. Together We Stand, Divided We Fall.
 
Back
Top Bottom