MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 295
- 679
Wafanyabiashara ndogondogo, wachonga Vinyago na Wachoraji wa picha mbalimbali wanaouza bidhaa zao kwa wajumbe wa mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),katika barabara ya chuo cha IFM, wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, wakiwahudumia watu mbalimbali waliofika katika eneo hilo kwa ajili ya kununua mahitaji yao .Aidha wafanyabiashara hao wameishukuru Serikali kwa kuwapa fursa hiyo ya kuonesha na kuuzaa bidhaa zao huku wakizidi kujitangaza na kutanua wigo wa biashara zao.