Wafanyabiashara wa Tanzania hawataki kabisa kulipa kodi, wana tatizo gani vichwani? Too much kulia lia

Nimeona clip ya Naibu waziri wa Kilimo, Bashe na baadhi ya wakulima wa bustani pale Arusha, wakijieleza kwa kudeka sana, na kueleza eti kodi ni kubwa. Kodi yenyewe ni 18%. Huu ni uzembe ktk biashara na ni tatizo la mazoea.
Hawakuzoea kulipa,walizoea kuona barabara na miundombinu nyingine inafanyika bila kujua kwamba kuna wanaoumia.
Mimi naona dawa ni serikali kukaa kimya hadi hapo watakapozoea wakakaa kimya kama wafanyakazi na wasafirishaji.
Nashauri kama wakulima wadogo(small scales) waangaliwe wasilipe kodi kama ilivyo kwa wafanyakazi wa kima cha chini
na hii ifanyike baada ya kujiridhisha kwamba kweli ni wadogo na kuwekwe vigezo. Waliobaki walipe kodi kwa maendeleo ya taifa.
 
Elimu ya kodi kwa wananchi bado haijawafikia,serikali ianzishe kabisa somo maalumu kuanzia O'level (kidato cha kwanza kuendelea), taifa haliwezi kusonga mbele kwa kujitegemea bila wananchi wake/wafanyabiashara kulipa Kodi inayotakiwa

Kodi hatujakataa kulipa, kodi ndio uhai wa taifa lolote na tunafahamu hata misaada tunauopokea kutoka nje ni kodi ya wanannchi wao hili la kulipa kodi halina Ubishi
 
Alipe kodi vipi
1wakati hawatengenezi faida
2.Hakuna mazingira ya uwezeshaji
3.Serikali hamna wanachowafanyia mbali na kuonekana siku za kudai kodi
4.kodi ina viwango vikubwa inakaribiana kabisa na turnovers zao it's just like ukianzisha biashara serikali ndo inapata kula na kupunguza mtaji wako
5.Kuhusianisha biashara na mlengo wa kisiasa
6.Political insecurity(risks) ,yaani usipopendwa tu hata na diwani biashara yako inapigwa neno moja tu ,wanakuharibia reputation na kushuka mapato
7.utadai vipi kodi wakati mindset ya kiunyonge Tajiri yoyote ni mwizi ,mnyonyaji na mzurumaji wa taifa?(mhujumu uchimi)
8.Sheria nyingi za biashara zinaadhibu badala ya ku create room ya negotiation (resolution)
9.Mazingira ya ujasiamali mabovu
Ongezeeni wadau
Ndugu unapomiliki gari,tuongelee pick up,lori n.k
Latra wanapokutoza ushuru huwa wamekuwezesha kununua gari hilo?
Kumbuka kuna ushuru wa barabara unalipia,kwenye mafuta unayoweka kwenye gari kuna tozo kibao za serikali,bado kuna ushuru wa Latra
na usipolipa unatozwa faini,miaka yote tunalipa ili nchi ifanye maendeleo.Wakulima mlikuwa mmesahulika na sasa mmekumbukwa
tunaomba muwe watulivu tujenge nchi.
 
Nimeona clip ya Naibu waziri wa Kilimo, Bashe na baadhi ya wakulima wa bustani pale Arusha, wakijieleza kwa kudeka sana, na kueleza eti kodi ni kubwa. Kodi yenyewe ni 18%. Huu ni uzembe ktk biashara na ni tatizo la mazoea.

Wakati mukilenga kumtisha rais, kumbukeni pia kuna maelezo ya kupanua wigo wa kodi, hivyo kama hamkuwa mukilipa kodi, lipeni. Anayekwenda Kenya wasikolipa kodi, aende! Mbona Kenya wanalipa kodi ya ardhi kubwaaa lakini wako kimya!

Mara ajira, mara hasara, visingizio viiingi! Wafugaji wanalipa, wasafirishaji wanalipa, waajiliwa wanalipa. Ninyi wakulima ndani ya viyoyozi hamtaki kwa tishio la kuhama, hameni Mbona wezi wanahamia wanakoruhusiwa kuiba! Too much demands!

It's useless to play lullabies for those who cannot sleep
Kabla sijachangia naomba utujuze unafanya biashara gani na unalipa kodi ya wastani kiasi gani
Tusije kuwa tunaongelea mambo ya biashara na mtu ambaye hajawahi hata kuuza Vocher ya simu au pengine niseme machungwa
Na kama humiliki biashara inayolipa VAT nakushauri ufute hii post kwani unaongelea kitu usichokuwa na uelewa nacho kwani unalinganisha VAT na zile hesabu za form one; kuwa 18% ya shs 1000 ni shs180.
 
Kodi inalipwa mtu anaenda kununua ndege kwa trillion 2 ili zije ziingize hasara nyingine kwa walipa kodi ya bilioni 60, tumia akili acha uzwazwa....
 
VAT ni asilimia 18 ya mauzo yote sasa jiulize kwa nini iwe asilimia 18 ya mauzo kwa ujumla? Kwa nini isitafutwe njia ya kuchukua hiyo 18 kwenye faida ya biashara ili kulinda mtaji, sasa hapo kwenye mauzo ya jumla bado mtu anadaiwa marejesho kwa sababu ule mtaji pia kakopa hasa ukija kuweka 18%. Ndio hapo hesabu hua zinaanza kukataa kwa hiyo hapo mnakaribisha mazungumzo na wajamaa wa mapato ili mzigo uishe huo
 
Niko sokoni nina meza yangu tangu nimalize chuo kikuu. Hapa nalipa kodi ya maana kabisa! Bila hata kuzunguka kila kona nikilia lia bila sababu. Lipa kodi. Ukishindwa tafuta unakoona kodi haitakiwi.
Wewe kodi ya nini ulipe wakati kitambulisho cha wamachinga cha elfu 20 tu kinakutosha?
 
Wewe kodi ya nini ulipe wakati kitambulisho cha wamachinga cha elfu 20 tu kinakutosha?
Huenda hata hicho Kitambulisho hana, hapo analipa ushuru wa Meza anadai ni Kodi
sasa Kina Manji, Habinder Singh, Rugemalila, Bakharesa, Mengi wanaolipa Kodi na wana TIN sijui atajipanga nao vipi
Ushuru wake wa kuchinja mbuzi au kuuza utaishia kwa mchinjaji pale Manispaa
 
Niko sokoni nina meza yangu tangu nimalize chuo kikuu. Hapa nalipa kodi ya maana kabisa! Bila hata kuzunguka kila kona nikilia lia bila sababu. Lipa kodi. Ukishindwa tafuta unakoona kodi haitakiwi.
meza gani unayolipa VAT?
 
meza gani unayolipa VAT?
Nilisema nalipa kodi, wewe unaniuliza VAT nikupe jibu gani sasa! Kila biashara ina kodi zake. Anayelima maua aelewe ana kodi zake kabla hata ya kuanza kilimo.
 
Nilisema nalipa kodi, wewe unaniuliza VAT nikupe jibu gani sasa! Kila biashara ina kodi zake. Anayelima maua aelewe ana kodi zake kabla hata ya kuanza kilimo.
sasa unawezaje kuwasemea watu mnaolipa kodi tofauti?
 
Tatizo makadirio hayafanyiki kiusahihi,na vilevile wengi wanafanya biashara kwakuchukua mikopo yenye riba kubwa kubwa ambayo ni matokeo ya usimamizi mbaya toka serikalini.Kingine ni serikali kua na irrational decisions nyingi,kwa mfano wamezuia malipo huko TARURA toka tarehe 20march,bila sababu za msingi,ni kama hawajui inawaadhiri vipi wafanyabiashara..wengine walitakiwa kurejesha mikopo,wengine wameshindwa kulipa mishahara wafanyakazi..nachomaanisha complex problems should be tackled by system approach techniques,sio kisiasa siasa!
Ndiyo maana ya kuwa na tax consultants; TRA wanakuja na mahesabu yao, wewe unapa mahesabu yako, mkishindana namba basi mnapelekana mahakamani bila kutumia rushwa!!
 
Back
Top Bottom