Wafanyabiashara wa Tanzania hawataki kabisa kulipa kodi, wana tatizo gani vichwani? Too much kulia lia

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,238
2,866
Nimeona clip ya Naibu waziri wa Kilimo, Bashe na baadhi ya wakulima wa bustani pale Arusha, wakijieleza kwa kudeka sana, na kueleza eti kodi ni kubwa. Kodi yenyewe ni 18%. Huu ni uzembe ktk biashara na ni tatizo la mazoea.

Wakati mukilenga kumtisha rais, kumbukeni pia kuna maelezo ya kupanua wigo wa kodi, hivyo kama hamkuwa mukilipa kodi, lipeni. Anayekwenda Kenya wasikolipa kodi, aende! Mbona Kenya wanalipa kodi ya ardhi kubwaaa lakini wako kimya!

Mara ajira, mara hasara, visingizio viiingi! Wafugaji wanalipa, wasafirishaji wanalipa, waajiliwa wanalipa. Ninyi wakulima ndani ya viyoyozi hamtaki kwa tishio la kuhama, hameni Mbona wezi wanahamia wanakoruhusiwa kuiba! Too much demands!

It's useless to play lullabies for those who cannot sleep
 
Kiukweli nimejua kweli wafanyakazi tunalipa sana kodi kwa uaminifu

Ingawa hata marupurupu yetu tunayostaili tunapunjwa

Sasa hawa wafanyabiashara wanadeka sana aiseh
Acha kaz ukafanye biashara sasa
 
Ungekuwa unajua mfanyabiashara anavyoipata hela ya kulipa kodi usingeandika Post hii, ili mfanyabiashara apate hela ya kodi lazima awepo mnunuzi, huyu anayetegemewa kuwa mnunuzi leo hii hana hela kutokana na serikali kushindwa kuinua uchumi wa wananchi, sasa mfanyabiashara atapata wapi hela ya kulipa kodi?

Hatuna umeme kwa sababu Dawasa imeshindwa kusambaza maji, Tanesco hawatoi umeme kwa sababu hawana maji ya kupoza mitambo na Dawasa hawatoi maji kwa sababu hawana umeme!
 
Bashe ajihadhari kuanza kuwatishia mawaziri wenzake. Nimesikia eti akiahidi kwenda kwa Waziri > Waziri mkuu au ngazi za juu. Hii ina maana anamtishia waziri na Waziri Mkuu kwamba yuko tayari kwenda ngazi za juu. Yeye ni nani? Naibu waziri!

VIjana kwenye nafasi za juu ni tatizo. Thinking ni tatizo. Unawaahidi hivyo wakulima wasiotaka kulipa kodi kwa mkutano mmoja!

Kodi ilipwe! Sasa hivi hata baadhi ya miradi ya wafadhiri inalipa kodi. Hawa wanalima nini cha kutishia nyau?
 
Kila nikiaangalia makato ktk salary sleep yangu 30% ya kodi, 10% nssf, 15% bodi for a total of 45%, afu kuna mtu analia lia 18% nakua simuelewi kabisa. Naweza kukuzabua vibao viwili vya uso uone nyota nyota.
 
Lipa kodi, hata ukiuza karanga. Kodi ni kwa kila senti inayoingia kwako unatakiwa uilipie kodi.
Wafanyabiashara hawakatai kulipa kodi ila muda mwengine hubidi kupitia njia za pembeni kwasababu za baadhi ya watu wasiowaaminifu(wakusanya Kodi) unaweza tajiwa Kodi inayosonsomola hata mtaji wako wote! Halafu Kuna Kodi haziangalii umepata faida au hasara wao wanachota tu!. Nenda kafatilie magufuli alivyoita wafanyabiashara ikulu utaelewa changamoto zao.

Unatoa mzigo bandarini umelipa Kodi upo barabarani bado unakamatwa ulipo tozo sijui za mdudu gani! Ukifikisha mzigo bado Kuna Kodi za leseni huko. Halafu ukija kuuza bidhaa bado mteja analalamika apunguziwe! Sasa kwa haya yote kwanini mtu asipitishe mzigo wake bandari bubu!

Mambo ni mengi fatilia.
 
Elimu ya mlipa kodi bado sana kwa wafanyabiashara. TRA walijisahau sana wakawa wanakusanya pesa bila kutoa taarifa na elimu wa watoa pesa.

Wakielewa makundi ya walipa na vigezo vya kuwa kwenye kila kundi watalipa bila matatizo.

Watanzania sio wabishi kwa vitu wanavyoelewa.
 
Niko sokoni nina meza yangu tangu nimalize chuo kikuu. Hapa nalipa kodi ya maana kabisa! Bila hata kuzunguka kila kona nikilia lia bila sababu. Lipa kodi. Ukishindwa tafuta unakoona kodi haitakiwi.
Kwenye hiyo meza yako umechangia tsh ngapi ya kodi kwenye mwaka wa fedha wa 2020/21? Wateja wako unategemea waajiriwa wa hao unawaambia wahame au una soko lako la kipekee?
 
Ukisikiliza malalamiko ya kodi Tanzania kiini cha tatizo kipo sehemu mbili.

1 maafisa wa TRA wasio waadilifu wanatumia sheria na regulations ambazo zinatoa muongozo pale inapoainika mfanyabiara alikusudia kwa makusudi kukwepa kodi nini kifanyike kwenye auditing.

Wao unakuta mfanyabiashara kodi yake sahihi na wala aina tatizo ila kwa sababu wazijuazo wao wanatumia regulations za kuchunguza bila ya sababu maalum na kupelekea malalamiko.

2 uelewa wa kodi kwa walipaji na elimu duni ya kodi hasa kwenye VAT. Mfano malalamiko mengi ni ukadiriaji wa vat wakati biashara yenyewe ndio kwanza inaanza. Hilo ni jambo la kawaida ukikadiriwa vat kubwa baada ya trading period kama mauzo yako ayajafikia ulicholipa peleka ushahidi wakurudushie. Wengi awafanyi hivyo wanabaki wanalalamika tu mauzo kidogo makadirio makubwa, in short uelewa wa mambo ya kikodi kwa walipaji nalo ni tatizo.
 
Suala la kodi ni changamoto sana.

Kwa upande mmoja seriklali inawajibika kukusanya kodi. Kwa upande mwingine serikali inafanya unyonyaji katika kuwakamua raia wake kwa mwanvuli wa kodi.

Ili ukusanyaji kodi usitafsirike kama unyonyaji ni lazima kodi iwe realistic. Kuna upuuzi fulani unaendelea wa kukusanya mara kodi ya vat, hapo hapo kuna kodi za halmashauri, kodi ya jengo, ada ya TBS, huduma kwa wateja, huo ni unyonyaji wa kiserikali kama si ujambazi kabisa.

Kama serikali inadhani kufanya biashara ni dili kihivo hadi kodi hizo zote si ifanye yenyewe hizo biashara ione kama zinalipa? Yenyewe ikijiingiza kwenye ibiashara biashara zake zinakufa. Kwa nini idhani kufanya biashara ni rahisi ikifanywa na mtu binafsi.

Mantiki yangu ni kwamba kama serikali ikiwa realistic kwenye kodi watu watalipa kodi kwa moyo wa kupenda. Na inawezekana walipa kodi wakongezeka. Kimsingi watu watozwe kodi zilizo za msingi na pia matumizi ya hizo kodi yawe wazi na yanayoeleweka. Siyo tulipe kodi halafu tuone watu wa serikali wanazitumbua hela zetu kipuuzipuuzi.
 
Alipe kodi vipi
1wakati hawatengenezi faida
2.Hakuna mazingira ya uwezeshaji
3.Serikali hamna wanachowafanyia mbali na kuonekana siku za kudai kodi
4.kodi ina viwango vikubwa inakaribiana kabisa na turnovers zao it's just like ukianzisha biashara serikali ndo inapata kula na kupunguza mtaji wako
5.Kuhusianisha biashara na mlengo wa kisiasa
6.Political insecurity(risks) ,yaani usipopendwa tu hata na diwani biashara yako inapigwa neno moja tu ,wanakuharibia reputation na kushuka mapato
7.utadai vipi kodi wakati mindset ya kiunyonge Tajiri yoyote ni mwizi ,mnyonyaji na mzurumaji wa taifa?(mhujumu uchimi)
8.Sheria nyingi za biashara zinaadhibu badala ya ku create room ya negotiation (resolution)
9.Mazingira ya ujasiamali mabovu
Ongezeeni wadau
 
Back
Top Bottom