Heshima mbele kwa wakuu wote, naomba kuligusa hili kidogo:-
1. Ni kwamba wafanyabiashara wetu ndio wakulamiwa kwa kutokuwa uptodate na information concerning shughuli zao, maana kama wangekuwa basi wasingekubali kujiingiza na huyo mwanadada, ambaye naye ni mfanyabiashara kama wao anayetafuta profit by anymeans necessary,
2. According to my .....dataz...., hawa wakuu wamemlipa dola 1,200 kila mmoja, na wao walikuwa kama 60 hivi, kwa hiyo piga hesabu ya 1,200 x 60, nafikiri kama sikosei jumla ya dola kama 70,000 that is a hell of money, ambazo wangeweza kuwasiliana na wabongo walioko kwenye makampuni makubwa huko USA yanayohusika na investment, ninawajua wabongo kibao ambao wangeweza kuwasaidia, tena for less money, kwa sababu hata ukitoa nusu tu ya hizo hela, unaweza kuwalipa an investment firm yoyote kule NY, na wakakufranyia more than what they got kutoka kwa huyu mwanadada, mkorofi na mwenye dharau sana,
3. Halafu pia nimepata habari kuwa kuna some of hawa wafanyabiashara ambao wanajaribu kuitumia hiyo nafasi kumfuata rais ili waongee naye maana huwa ni impossible kwao kuonana naye bongo, my point ni kwamba ukweli ni kwamba kati ya hawa 60, the real businessman kwa standards za US, I am sorry kusema kwamba hawazidi wawili tu! wengi wao ni wababaishaji tu ambao walitaka kulepeleka ubabaishaji mpaka majuu, just to meet another one of their own huyu mwanadada Mona, poleni sana wakuu!
4. Heshima kwa Mzee wa Mererani, mmoja kati ya hawa wafanyabiashara waliofuatna na rais, yeye ndiye mfano wa kuigwa, maana kwanza alikuwa akikaaa Sheraton Hotel, yaani mahali pa uhakika kuweza kupata wawekezaji wa USA, muwekezaji anayekukuta Sheraton, atakupa deal tu hata iwe vipi, lakini huwezi kujibanza sebuleni kwa jamaa huko majuu, halafu ukategemea deal, come on wakuu tuache huu ubongo mpaka majuu, yes maana rais anaweza kukutana na muwekezaji mkali wa kitengo chako cha biashara, basi anamuuliza waziri aliyefuatana naye kuwa huyu muwekezaji vipi, basi waziri anajibu kuwa kuna kijana yuko Hilton au Sheraton, nafikiri atweza kuongea naye, basi huyu muwekezaji anapewa jina na hotel yako mnakutana, deal safi!
Ndio maana ninampa heshima huyu mkuu wa Mererani, maana kwanza alikuwa proper on every area, anakaa kwenye the right address, Sheraton Hotel, pale West Manhattan, ndani ya NYC, halafu on the weekend akaangusha bonge la party, lililohudhuriwa na mawaziri na karibu viongozi wote wa serikali waliokuwepo, watu walikuwa served na wazungu eeenh! Yaani wewe ni kukaa tu na kuletewa mapocho pocho na wazungu, I mean vijana tuwe wakweli, huyu atakosa deal huyu? Huyu anamuhitaji huyo dada Mona? Plae kwenye party pia aliwaalika wawekezaji sasa unafikiri huyu Mzee Wa Mererani atalala na njaaa?
Wakuu yaani wafanyabiashara wabongo wenzangu tubadilike kidogo, kama mambi ni maji ya shingo tusiyarukie tu, huko majuu hakuna uchache kwenye biashara eithr unazo au huna, lakini msiende huko kuanza kuwalaumu watu bure na viongozi wetu wakati mambo hamuyawezi, waacheni kina Mzee wa Mererani, jipangeni sawa kwanza ndio muingizane huk maju kutafuta biashara za kweli, mkae hteli zinazoeleweka, hivi mliwahi kuona muwekezaji toka nje ankuja bongo na kulala sebuleni kwa mtu akitegemea deal na viongozi wa bongo?
Wewe mbongo, mtu mzima na akili zako timamu unamuamini, mama Mshona, tena kwa ma-deal ya majuu? OOh my God!