Wafanyabiashara wa JK ,New York watapeiliwa mamilion ya pesa.....

Hasara

Senior Member
Dec 29, 2006
138
9
Wafanyabiasha waliofuatana na Rais wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Jakaya Kikwete,
baada ya muandaaji wa safari na kuwakutanisha na wafanya biashara Tanzania na Wamarekani kutofanikiwa na pesa nyingi walizo lipa,

walikasirika na kutaka kumpiga muandaaji wa safari baada ya kuwajibu vibaya kuwa ''is not my business''
muandaaji wa safari ni binti wa afrika ya kusini aliye pewa hiyo dili.

mwaka jana safari ilikuwa nzuri kuliko hii, kampuni iliyo pewa tenda na serikali ya Tanzania kuanda ili sub contract kwa mtu mwingine ambaye ameboronga sana pamoja na kulipwa na wafanya biashara wakitanzania

na baadhi ya makampuni ya kimarekani yaliyokubali kuwafadhili wafanyabiashara hao, kama vile JPMOGACHASE, NA CHEMBER OF COMMERCE OF CAREBEAN mbalimbali na mengineyo.

wafanyabiasha hao wamekuwa wakilalamika kila siku hawajakutana na watu waliyo ambia watakutanana nao kujadiliana biashara na jinsi watakavyo weza kushirikiana kibiashara, wangi walikataa kwenda katika hiyo mikuta ambayo walingundua haiwasaidi wakafuta shughuli zao nyingine ambazo walizifuatilia,

wamesema malamiko yao wataya fikisha kwa Rais kueleza safari haikuwa na mafanikio kama walivyo kuwa wanatengemea, jamani watanzania kweli balozi na wsasomi tuliyo nao wote zimeshindwa kuandaa kitu kama hichi mpaka kulipa watu kutufanyia.

mimi nimechoka baada ya kusikia kutoka kwa wafanya biasha waliyo rudi hapa nyumbani na kulalamika wametapeiliwa kama safari nika hii watakwenda tenda na misafara ya rais

jingine wafanya biashara waliambia na huyo muandaaji kwajina MONA kwamba wafanyabiasha wanamfuata rais hapo nyuma tu yani viherehere ilizua fujo kubwa watu kudai wamekenda na pesa yao na siyo pesa ya serekali wawaache kabisa,

anaye jua mfanyabiashara yeyote aliye kuwa kwenye msafara wa rais awaulize kama haya maneno niya kweli
majina ya baadhi ya wafanyabiasha nitayaweka hapa baadaye...
asanteni
 
Hivi ndivyo vichekesho, marekani kuna watanzania kwa ma-elfu, kwa nini hawakuwasiliana na watu kama akina Mwanakijiji wawape direction? What is the use of having an Embassy or Tanzanians in that country? In what/which time age are we living?
 
Hivi ndivyo vichekesho, marekani kuna watanzania kwa ma-elfu, kwa nini hawakuwasiliana na watu kama akina Mwanakijiji wawape direction? What is the use of having an Embassy or Tanzanians in that country? In what/which time age are we living?

ni kweli ulichosema, kuhusu time age hilo usishangae, si ndio maana utakuta waziri fulani kasomea madawa lakini cha kushangaza anapewa uwaziri wa michezo ! kwa hilo usishangae !
 
Mwanakijiji, mjini shule, na kijijini je?.................

Kijijini dhikini (jocking).
Unajua Balozi zetu bado ziko kisiasa na sii kiuchumi (Economic Diplomacy). Mimi nadhani mambo kama haya yangeandaliwa na balozi zetu amabazo zinatumia mabilioni ya walipa kodi.

Kwanza sijui performance ya balozi zetu huwa inakuwa asesiwa vipi. Tukitaka kusema balozi fulani inaperform vizuri tunaangalia nini?
 
sasa wanalalamika kwa Rais ili iweje?

kwani TANZA TRADE hawana branch USA?

hawa wafanyabiashara wanajua fika mbaya wao ni Tanzania Investment Centre na Balozi yetu sasa hii JK haimhusu
 
sasa wanalalamika kwa Rais ili iweje?

kwani TANZA TRADE hawana branch USA?

hawa wafanyabiashara wanajua fika mbaya wao ni Tanzania Investment Centre na Balozi yetu sasa hii JK haimhusu

GT unajua kila kitu watu wanakimbilia kwa rais au waziri mkuu hatakama vymbo vyakushughulika hayo mambo kipo. Mtu akiiba atapelekwa kwa raisi badala ya mahakamani, mtu kala rushwa anashitakiwa kwa raisi badala ya TAKURU, watuhumiwa wa madawa ya kulevya wanapelekwa kwa rahisi na si kwa kitengo cha kuzuia madawa.

Hapa kunakasoro inawezekana rahisi kajilimbikizia majukumu au watu wamepoteza imani na vyombo husika. Pia hii inachangiwa na staili ya muungwana aliyoingia nayo madarakani yakutembelea wagonjwa, wafiwa na watu wote wenye michango ya harambee etc.
 
Raisi si ndo aliwaalika waende wote, wacha wamlalamikie. Nathani hata ndege walipanda moja(gulf stream si mkweche) sasa kwenye ndege unataka wakate isu gani Buzwagi? au mlokuwepo USA mtupe data za usafiri gani JK alitumia, maana siku hizi nasikia ni Emirates/Qatar Air tu.

Mimi mtizamo wangu ni kuwa siku hizi huitaji kwenda na raisi wala nini kokote duniani kutafuta business connections. Wanakijiji kibao wanaenda mpaka Mongolia,Vanuatu,Tazmania na wana close madeal itakuwa USA?
 
Waache wakione cha mtema kuni nani aliwaambia wafuatane na mafisadi?
 
kutokana na ile picha ya wafanyabiashara pale kwa michuzi sikuona hata mfanyabiasha mmoja zaidi ya matapeli wetu wa kila siku.na karibu wote pale ni watu wanaopata tenda za serikali tu.hakuna mwenye kujitegemea kibiashara
 
kutokana na ile picha ya wafanyabiashara pale kwa michuzi sikuona hata mfanyabiasha mmoja zaidi ya matapeli wetu wa kila siku.na karibu wote pale ni watu wanaopata tenda za serikali tu.hakuna mwenye kujitegemea kibiashara

Kumbe Tenda za Serikali sio biashara du!, by the way serikali inawajua ma-supplier wake zaidi kuliko wafanyabuiashara wengine... twendelee kujadili!
 
I can oly say this....If it's true that the TZ business persons were conned in the USA, then it serves them right!

My suggestion: In the future, they should try and locate a Tanzanian PR and/or Advertising company in the US (or anywhere else in the world), to make the arrangements. In this way there are numerous benefits both ways...
- The Tanzanian PR company will be doing business for TZ
- The company will never say "It's not my business", because it will be company's business to make everything a success....Tanzanians for Tanzania!
- Everyone will be happy ;-)!

Thank you.
 
Heshima mbele kwa wakuu wote, naomba kuligusa hili kidogo:-

1. Ni kwamba wafanyabiashara wetu ndio wakulamiwa kwa kutokuwa uptodate na information concerning shughuli zao, maana kama wangekuwa basi wasingekubali kujiingiza na huyo mwanadada, ambaye naye ni mfanyabiashara kama wao anayetafuta profit by anymeans necessary,

2. According to my .....dataz...., hawa wakuu wamemlipa dola 1,200 kila mmoja, na wao walikuwa kama 60 hivi, kwa hiyo piga hesabu ya 1,200 x 60, nafikiri kama sikosei jumla ya dola kama 70,000 that is a hell of money, ambazo wangeweza kuwasiliana na wabongo walioko kwenye makampuni makubwa huko USA yanayohusika na investment, ninawajua wabongo kibao ambao wangeweza kuwasaidia, tena for less money, kwa sababu hata ukitoa nusu tu ya hizo hela, unaweza kuwalipa an investment firm yoyote kule NY, na wakakufranyia more than what they got kutoka kwa huyu mwanadada, mkorofi na mwenye dharau sana,

3. Halafu pia nimepata habari kuwa kuna some of hawa wafanyabiashara ambao wanajaribu kuitumia hiyo nafasi kumfuata rais ili waongee naye maana huwa ni impossible kwao kuonana naye bongo, my point ni kwamba ukweli ni kwamba kati ya hawa 60, the real businessman kwa standards za US, I am sorry kusema kwamba hawazidi wawili tu! wengi wao ni wababaishaji tu ambao walitaka kulepeleka ubabaishaji mpaka majuu, just to meet another one of their own huyu mwanadada Mona, poleni sana wakuu!

4. Heshima kwa Mzee wa Mererani, mmoja kati ya hawa wafanyabiashara waliofuatna na rais, yeye ndiye mfano wa kuigwa, maana kwanza alikuwa akikaaa Sheraton Hotel, yaani mahali pa uhakika kuweza kupata wawekezaji wa USA, muwekezaji anayekukuta Sheraton, atakupa deal tu hata iwe vipi, lakini huwezi kujibanza sebuleni kwa jamaa huko majuu, halafu ukategemea deal, come on wakuu tuache huu ubongo mpaka majuu, yes maana rais anaweza kukutana na muwekezaji mkali wa kitengo chako cha biashara, basi anamuuliza waziri aliyefuatana naye kuwa huyu muwekezaji vipi, basi waziri anajibu kuwa kuna kijana yuko Hilton au Sheraton, nafikiri atweza kuongea naye, basi huyu muwekezaji anapewa jina na hotel yako mnakutana, deal safi!

Ndio maana ninampa heshima huyu mkuu wa Mererani, maana kwanza alikuwa proper on every area, anakaa kwenye the right address, Sheraton Hotel, pale West Manhattan, ndani ya NYC, halafu on the weekend akaangusha bonge la party, lililohudhuriwa na mawaziri na karibu viongozi wote wa serikali waliokuwepo, watu walikuwa served na wazungu eeenh! Yaani wewe ni kukaa tu na kuletewa mapocho pocho na wazungu, I mean vijana tuwe wakweli, huyu atakosa deal huyu? Huyu anamuhitaji huyo dada Mona? Plae kwenye party pia aliwaalika wawekezaji sasa unafikiri huyu Mzee Wa Mererani atalala na njaaa?

Wakuu yaani wafanyabiashara wabongo wenzangu tubadilike kidogo, kama mambi ni maji ya shingo tusiyarukie tu, huko majuu hakuna uchache kwenye biashara eithr unazo au huna, lakini msiende huko kuanza kuwalaumu watu bure na viongozi wetu wakati mambo hamuyawezi, waacheni kina Mzee wa Mererani, jipangeni sawa kwanza ndio muingizane huk maju kutafuta biashara za kweli, mkae hteli zinazoeleweka, hivi mliwahi kuona muwekezaji toka nje ankuja bongo na kulala sebuleni kwa mtu akitegemea deal na viongozi wa bongo?

Wewe mbongo, mtu mzima na akili zako timamu unamuamini, mama Mshona, tena kwa ma-deal ya majuu? OOh my God!
 
HAWA wafanyabiashara wameyataka ...kikwete ameshindwa nyumbani kusaidia wafanyabiashara ,ataweza ugenini?.....serikali imeshaingia hasara hapo..kupeleka watalii tu...mwaka jana kuna mmoja alipeleka viatu vya chatu..sasa sijui kama walmart wangempa oda ya pea laki moja angepata wapi chatu wa kutosha..watu hawatumii akili..mimi hapa tanzania wafanyabishara wa kuambatana na rais sioni zaidi ya 20[wazawa]..but utakuta ziara zinajaaa wasanii..na msanii...

kwanza wafanyabiashara wenyewe washamba ...walilipia dinner kwenye ile hafla ya sullivan huko ...@$750... wakawa wanasubiri nje wanangoja kadi hadi sherehe imeisha .. walifikiri kadi kama nyumbani,, kumbe walitakiwa tu ku confirm reception kama wamefika ili wapelekewe kwenye meza zenye majina yao....hasara!!
 
Kuna ule msemo "Experience is the best teacher"hivyo nadhani hawa wafanyabiashara watakuwa wamejifunza vyema, ila hiyo tuition fee yake si ya kitoto!
 
kwanza wafanyabiashara wenyewe washamba ...walilipia dinner kwenye ile hafla ya sullivan huko ...@$750...wakawa wanasubiri nje wanangoja kadi hadi sherehe imeisha ..walifikiri kadi kama nyumbani,,kumbe walitakiwa tu ku confirm reception kama wamefika ili wapeleke kwenye meza zenye majina yao....hasara!!

lah poor them. umenichekesha sana.
 
Tatizo la wafanyabishara wengi wa TZ hawana culture ya biashara bado wanataka kila kitu wafanyiwe, utashangaa wakiwa kwenye majadiliano ya biashara wanaingiza mambo ya kusaidiwa, grants etc
 
HAWA wafanyabiashara wameyataka ...kikwete ameshindwa nyumbani kusaidia wafanyabiashara ,ataweza ugenini?.....serikali imeshaingia hasara hapo..kupeleka watalii tu...mwaka jana kuna mmoja alipeleka viatu vya chatu..sasa sijui kama walmart wangempa oda ya pea laki moja angepata wapi chatu wa kutosha..watu hawatumii akili..mimi hapa tanzania wafanyabishara wa kuambatana na rais sioni zaidi ya 20[wazawa]..but utakuta ziara zinajaaa wasanii..na msanii...

kwanza wafanyabiashara wenyewe washamba ...walilipia dinner kwenye ile hafla ya sullivan huko ...@$750... wakawa wanasubiri nje wanangoja kadi hadi sherehe imeisha .. walifikiri kadi kama nyumbani,, kumbe walitakiwa tu ku confirm reception kama wamefika ili wapelekewe kwenye meza zenye majina yao....hasara!!

...hii ya viatu vya chatu kali mzee,jamaa ana kiwanda au ananunua tuu naye
 
Tatizo la wafanyabishara wengi wa TZ hawana culture ya biashara bado wanataka kila kitu wafanyiwe, utashangaa wakiwa kwenye majadiliano ya biashara wanaingiza mambo ya kusaidiwa, grants etc

Mkuu heshima mbele, wanachohitaji ni kuacha usanii, mambo ya Salamander huwezi kuyapeleka majuu, huko ma-US watu walishapita mambo ya usanii sasa huwa wanafanya kweli,

huwezi enda tafuta biashara wakati hata lugha haipandi, halafu umechoka, suti yako shati na suruali rangi tofauti maana ni mtumba, hukai hoteli inayoeleweka, huwezi kuchukua texi unataka kuleta mambo ya kupiga mateke huko majuu ukifika kwenye deal unanuka jasho, I mean we can go on and on, hao wakuu wanahitaji kuiga mfano wa Mzee Wa Mererani,

Next time huyu mzee awape darasa kabla kwenda huko majuu, but at the same token wajifunze matumizi mema ya internet, kwa sababu huyo mama mona hana ujanja wowote yeye huwa anaingia tu kwenye internt na kutafuta hizo biashara mbuzi anazowauzia!
 
Back
Top Bottom