wafanyabiashara ndogo ndogo wa ubungo waliondolewa leo wamevamia manispaa ya kinondoni, kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa eneo la mbadala. hiyo imetokea baada ya mbunge wa ubungo john mnyika kuwaarika kuja kwani kutakuwa na kikao fedha na uongozi cha manispaa ambacho mbunge ni mjumbe wa kamati hiyo. hatimaye mara baada ya kumaliza kikao mbunge alifanikiwa kuwatoa ofisini meya na timu yake kuja kuwasikiliza wafanyabiashara hao. na ndipo kamati iliundwa hapo na mwekiti wa kamati naibu meya, na zoezi hilo la kutafuta eneo ndani ya ubungo linaanza leo.