Wafanya usafi maofisini

Wafanya usafi maofisini

Hute

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,537
Reaction score
6,479
Ofisini kwa kawaida huwa nafika saa kumi na mbili kamili asubuhi, mida hiyo lile kampuni la kufanya usafi ofisini kwetu wafanyakazi wake wanafika hapa saa kumi au kumi na moja kasoro asubuhi, nawakuta wameshamaliza usafi sasa wanaelekea vyooni kusafisha.

Kuna msichana mmoja hapa amekuwa akinipiga mzinga wa nauli mara kwa mara anasema hana nauli, ni msichana mzuri sana hata huwezi amini kwanini anafanya kazi za usafi maofisini.

Siku moja al manusura shetani anishinde, lakini nilishinda nusu, nilimjaribisha kuomba mzigo, hakusita kukataa nikajuta kwanini nimemwomba halafu amekubali moja kwa moja ila hataki kufanyia ofisini anataka nje ya ofisi,

Nijajiuliza kwanini amekubali haraka hivi? halafu, kwanini nitembee na mfanya usafi ofisini anayeishi uswahilini huko? nikamwacha kama alivyo na nikaona huyu malaya tu kumbe na huo ulikuwa mtego wangu kwake kumfahamu ombaomba ya nauli yake.

Miezi mitano imeshapita sasa, anafanya usafi floor nzima wako na wanaume wawili vijana wenzie lakini yeye mcheshi kweli. Kuja kugundua, kumbe zile nauli alikuwa anatuomba wanaume wa vyumba vyote kwenye floor yetu kila mtu akimpiga kibuti cha nauli anakusanya kama konda wa daladala.

Kufanya utafiti, ametembea na wanaume wa floor nzima kasoro mimi, hapo ndipo nilichoka. Nikajiuliza kumbe hawa wasichana wa usafi ni wabaya hivi, si wanaweza kuambukiza UKIMWI ofisi au hata gorofa zima?

Hhalafu ni wazurii hadi unajiuliza inakuwaje msichana mzuri kama huyu anafanya kazi za usafi? kuweni makini wandugu.
 
Sasa mkuu kwani uzuri ni guarantee ya kuwa na kazi nzuri?

Anaweza kuwa mzuri lakini kisomo kikawa shida kwa hiyo huwezi shangaa. After all kufanya usafi ni kazi kama kazi nyingine tena siku hizi hadi kuna vyuo vinavyofundisha mambo hayo sema huwa hatuna utaratibu wa kuheshimu kazi na tuna dhana ya kuthamini baadhi ya kazi.
 
Kazi ni kazi acha atafute na kuongezea kipato, zaidi mshauri kwa anachofanya kuwa ni kujikusanyia magonjwa,! Bora hujapita hapo ila kama ulipendaga hako ka dada!!!!!! Joke
 
Hongera kwa kushinda hilo jaribu! Ndiyo tabia zao hizo! Tusipokuwa makini watatumaliza hao!
 
ebu wew j...... kuwa mkweli eti kasoro wew? mmmmm ebu nisiseme kitu hapa ahaaaa jock
 
Mkuu hata kama unakaa masaki usiwadharau wanaokaa Tandale kwa mfuga mbwa. Usafi ni kazi kama kazi nyingine. Hongera kwa kuyashinda majaribu ila si kwa sababu ni msafi, ila ulishinda kwa sababu ya 'DHARAU' zako.

Na kwa taarifa yako kuna wale si wafanya usafi na hawagawi koridoni za ofisini tu, bali kila sehemu, na ukimwi wa kwa anayefanya usafi hauna tofauti na wa kwa hr au accountant.
 
huyo dada hafai inawezekana hata elimu kuhusu ukimwi hana au ana maisha magumu sana yanayopelekea afanye hivyo ongea nae mwambie anajikaribishia kifo ajirekebishe
 
Kumbe ndio hivi ngoja nikae nao mbali kuna mmoja ameanza kunichekea chekea kumbe anataka kuniingiza mtegoni
 
huyo dada hafai inawezekana hata elimu kuhusu ukimwi hana au ana maisha magumu sana yanayopelekea afanye hivyo ongea nae mwambie anajikaribishia kifo ajirekebishe
Kila nikiufikria huo mtandao nachoka kabisa........maana hao wajamaa wana mademu zao na hao mademu zao wana michepuko yao na hio michepuko yao ina mabwana zao...................
 
huyo dada hafai inawezekana hata elimu kuhusu ukimwi hana au ana maisha magumu sana yanayopelekea afanye hivyo ongea nae mwambie anajikaribishia kifo ajirekebishe

miss neddy wapo wasomi na wenye pesa na wana taarifa kuhusu ukimwi ila ni malaya pia,,,watoto wa vyuo kwa umalaya motooo,na wengine maofisini wana status zao kubwa,
Umalaya Hulka
 
Last edited by a moderator:
Mtaendelea kuambukizwa na mimi nasema muambukizwe tu maana hatuna namna nyingine....kubaki njia kuu hamtaki,kutumia condom mnaona mzigo tuwasaidieje watu kama ninyi(nakuambia wewe kwa niaba ya hiyo floor nzima)
 
Aaa ndio maana wengine huwa hawahamishwiiiii.wengine wale wabaya wabaya ndio huhamishwa hamishwa .vizuri vizuri havihamishwiiiiii.uwiiiiii
 
Ukisema kua kwanini nitembee na mfanya usafi ofisini anayeishi uswahilini, inamana wewe ni mbora zaidi? mzuri sana msafi sana au hadhi yako ni ya watu gani? kazi ni kazi kama na nyote haiwezekani kufanya kazi kiwango cha juu lazima awepo wakusafisha,wakukata majani na wengineo dharau sio nzuri na ungekua CEO AU DG wewe watu wangetafuta pakupita...
 
Mkuu Hute Hao wadau ni sheedah kwani ukidonoa tu, yaani gusa unate.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom