Waepuke wanawake masikini

Sio vibaya mwanamke kuwa mama wa nyumbani, ingawa ni muhimu kuangalia kama kuna chain ya umasikini kwenye familia yake, otherwise utahudumia ukoo mzima. Mimi mke wangu ni mama wa nyumbani lakini anatokea kwenye familia inayojimudu, hata wakati tunakutana kwa mara ya kwanza alimua anafanya kazi. Tulikubaliana baadae aache kazi kwa sababu zetu za kifamilia.

Ulichoongea kwa kiasi kikubwa kilikua kinafanyika kwenye patriarchal society miaka ya zamani. Ukiangalia hata nature ina-flow kwenye pattern hiyo kwamba mwanaume ni mtafutaji, mwanamke ni household manager.

Lakini jamii ishaondoka uko kwenye patriarchy. Kutaka wanawake waendelee kuhudumiwa mahitaji yao na wanaume ni namna ya kupuuza uwezo wao pia. Maana indirectly tunawaambia they are weak so they need man's saving. Sikatai suala la mwanaume kuwa major provider, lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba mwanamke kutoka absolutely poverty background ni liability kwenye ulimwengu wa sasa
 
usichokijua ukiwa na mpenz anae kudai bill kila siku na ukawa unampenda mbinu za kutafta pesa huongezeka hivyo ata kusapot utoboe mapema zaid.

huwez kunielewa kama ww ni mdangaji ila kama unakuaga na mapenz ya kweli huyo mwanamke anae kuomba msaada daily na ukawa unajitafuta na uwe unampenda unatoboa fasta sana.

hii mbinu wajanja wanaijua nyinyi vilaza mwendelee kuwataka matajir tuone.
 
Hata huyo ambae unaona ana akiki na malengo ya mbali napo unafanya gamble tu. Hakuna assurance kama malengo yake yatatimia. Regardless of your effort, time and sacrifices hakuna guarantee kama ataendelea kuwa nawe baada ya malengo yake kutimia. So, it's better to prioritize rwsults, than potential.
 
Siku hizi maisha tunaviziana sana; wanaume wanataka wanawake wanaojiweza ili wawalee, wanawake wanataka wanaume matajiri ili watajirike. 😊

Wanawake wanatakiwa kupambana sana siku hizi; game imebadirika sana. Unaolewa sababu ya kitu flani. Hatari sana!
Ukiangalia siku hizi; mwanamke akipata kazi au akiwa anajiweza ndio anaolewa. Kazi ipo.
 
pisi zinatofautiana, kuna ambaye ni maskini hapendi kuwa tegemezi pia ana nidhamu ya pesa.
Kwa uelewa wangu pisi zinazotokea familia zenye uwezo kiuchumi ( wakishua ) wengi wao hawana nidhamu ya pesa !
Hapa niliowazungumzia ni wale pisi njaa kali na hawataki kujishughulisha kufanya kazi yeyote ya kuwaingizia kipato.

Zaidi hutumia mapenzi kama kitega uchumi na sehemu ya kupooza njaa zao, huwa hawanaga nidhamu ya pesa hawa wanaomba mnoo yani ni kero sana ukiwa karibu na pisi aina hii.

Na kazi hawataki kufanya, alafu ukiwanyima wanakuona mwanaume huna pesa. Wanasahu wamekuwa ombaomba mnoo!


#Hallelujah!!!
 
Wewe ungekua masikini halafu mwanamke yupo kwenye nafasi nzuri kiuchumi unafikiri angekubali kuwa na mahusiano na wewe?
Angekuwa na pesa basi angekuwa ni mtu tofauti kabisa. Hakuna mtu anazaliwa akiwa mtu tayari, mapito ya duniani ndio hutupa utu. Moja kati ya mapito ni pesa.

Kwahiyo hapa unamhukumu mtu mmoja kwa tabia za mtu mwingine tofauti(ambaye pia umekisia sana tabia zake kwasababu hayupo na humjui).

Licha ya hayo yote, mahusiano/ndoa ndio jambo lenye risk kubwa zaidi kwenye maisha na hiyo risk haikwepeki. Mada kama hii haiwezi kuwa na hitimisho kwasababu mahusiano ni fumbo. Hakuna jibu sahihi, kuna machaguo tu.
 
Mkuu smart ladies wako haijalishi wako kwenye hali gani. Na ukipata mmoja ume-win
 
Kama motivation yako ya kutafuta hela ni kutimiza mahitaji ya mwanamke uliyenae kwenye mahusiano basi uenda wewe ndie ukawa kilaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…