Wadhifa mpya wa mheshimiwa Edward N. Lowassa

Wadhifa mpya wa mheshimiwa Edward N. Lowassa

Unaweza kuwa chunga ng'ombe na wakati mwingine msuluhishi, mshauri nk. Japo naino kauli yako imekaa kikejeli zaidi
 
mkuu usiwe mnafiki alipokuwa ccm kipaji hiki hamkukiona na kwanini uje kujadili sifa hizi kipindi hiki

Mwaka 1995 Nyerere alimkata, mwaka 2015 Kikwete akamkata tena na Oktoba 25 mwaka 2015 Watanzania walio wengi wamkata pia.

Kwa kuwa amekatwa kwenda Ikulu, sasa ni muda muafaka afanye kazi za upatanishi kwa mujibu wa karama zake.
 
Alinyamaza Raira Odinga itakuwa Lowassa Ben akatulie aache nchi itafute maendelea, mzee was msoga katuacha hoi
 
Bado tunakumbuka wamchague yeye kua raisi lakini wabunge na madiwani wachague ccm
 
Ni mtazamo wako ndugu. Kila mtu kajaliwa ubongo wake. Kuna wanao ona mambo kwa upeo mpana hawa wanaitwa Great Thinkers na pia kuna Myopic minds ambazo wao hufikiri juu juu tu. Sikuchagulii kundi ila tafakari.

Nimefungua uzi huu nikidhani kuna kuna taarifa kumbe ni upuuzi mtu. EL anachokiweza ni kupiga dili na ufisadi tu. Hafai hata kushauri wanandoa.
 
Kimsingi Lowassa ni Mwizi namba moja asiye na mfano hapa TZ ,na anastahiri kuwa jela na naishangaa serikali ni kwann huyu jamaa bado anadunda mtaani.....inasikitisha sana
 
Sina lengo la kutafuta umaarufu kwa kumzungumzia mtu ambaye kwa sasa anaonekana kuwa maarufu zaidi nchini Tanzania. Ana mvuto wa pekee na kajijengea heshima kubwa katika jamii. Anakubalika kila eneo. Bara na Visiwani; Wakristo na Waislamu, Wenye kumcha Mungu na Wapagani; Wazee na Vijana; Wanaume na Wanawake wote wanamkubali.

Hauhitaji kuwa msomi sana, wala tajiri sana ili kupata umaarufu kama alionao Ndg. Edward Nyoyai Lowassa. Naweza kusema bila ya wivu wala donge kuwa Mungu mwenyewe ndiye alimjalia Ndg Lowassa karama hii. Amefanya siasa kwa miaka mingi na tumeona mazuri na mapungufu yake na hivi karibuni alijikita katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais lakini yaliyotokea sina haja wala sababu ya kuyajadili hapa lakini JIBU kila mmoja wetu analo kwa namna tulivyopokea matokeo.

Kinachonisukuma kuandika waraka huu; ni kuikumbusha jamii na Ndg. Lowassa kuwa Mungu ametujalia kumpata mtu ambaye anaweza kutumika vizuri katika kuleta mtangamano wa Kitaifa. Kwa karama yake ya kukubalika, binafsi, naona ni mtu sahihi wa kufanya usuluhishi yaani MEDIATION. Mwl. J.K. Nyerere alijaliwa kipawa hiki na alitumika kufanya usuluhishi wa ndani na nje ya nchi. Amefariki akiwa ni mpatanishi wa mgogoro wa Burundi. Ninaiona karama hiyo kwa Lowassa. Kwangu mimi hii ni hazina kubwa ambayo hatuna budi kuitumia kwa manufaa ya taifa letu.

Ninatambua wale ambao wanawaza siasa katika kila jambo wanaweza kuja na kejeli nyingi juu ya hiki, lakini ningependa mnipe mbadala wa Lowassa katika kukubalika katika jamii. Je, ni Pinda, Ben, Mzee Ruksa, JK, Salim, Mzee Wassira, au Warioba??? Kwangu mimi, Lowassa ndiye mtu pekee kwa sasa ambaye anaweza kuwaambia watu wenye jazba, tulieni na wakatulia, wenye silaha mikononi kuwa wekeni chini na watu wakaheshimu; anaweza kuwaambia wanaopigana tulieni na watu wakatii.

Baada ya maisha ya siasa, sasa ni wakati muafaka sana kwa Mzee Lowassa ukawatumikia Watanzania kwa njia hii ambayo kwangu mimi naona ina thawabu kubwa sana mbele za Mungu. Tuna migogoro ya muda mrefu hapa nchini mf. Wakulima na Wafugaji, Wachimbaji wa madini na Wawekezaji, misuguano ya kidini ya chini kwa chini nk. Migogoro hii kwa upande mwingine haihitaji mabavu au mkono wa Serikali bali watu wenye busara zao kama Ndg. Lowassa. Kama hili halitoshi, familia ya Lowassa imebahatika kuwa na Mama mwenye mvuto na ushawishi kuliko wanawake pengine wote kwa sasa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anajiheshimu, ana busara na anakubalika mno mno. Hii ni nyongeza kwa Mzee Lowassa katika kukamilisha kazi ambayo naiona imebaki katika kipindi cha maisha yake. Neno la Mungu linasema Heri Wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu!!

Mwenyezi Mungu akupe jicho la pekee Mzee Lowassa ili uweze kutumika kwa namna mpya na yenye manufaa makubwa kwa Taifa, Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla. Mungu akuzidishie maisha marefu na wote wenye kuwaza na kupanga mabaya dhidi yako washindwe.
MAISHA MAPYA NDIYO HAYA MZEE LOWASSA, TUTUMIKIE KWA NAMNA HII.

Bora hata ungeandika chenga kuliko hizj pumba hata kuzipepeta haiwezekan ni kutupa jalalani
 
Unatafuta pesa ya kumpeleka mwanao shule za hela ndefu. Kuanzia mwakani elimu bure,kuanzia kindergarten to form IV. Hapa kazi Tu
 
Lowassa ahataa kujitumikia mwenyewe hawezi.

Angekuwa na umaarufu huo unaosema saa hizi tungemuona Ikulu.

Kashindwa kujitumikia mwenyewe hata ya kutumia fedha nyingi sana, ataweza kutumikia watu?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Jamaa hadhi yake imepanda sna ila mbowe aache kuchakachua luwasa
 
Wewe ndio unamkubali na kuona hizo sifa ulizomwagia. Mimi binafsi simkubali lowassa hata kidogo. Ndio maana tulio wengi tulimkata kwenye sanduku la kura. Pole mkuu.
 
Kwa lipi? Unamjua lowasa au umekutana nae kwenye mitandao? Hana sifa yoyote zaidi ya umafya na ujizi tu, tunaomjua ndo tunakwambia,
 
Mungu ameliepusha taifa letu na dhahama ya lowasa ,kwa macho ya kibinadamu hauwezi kuelewa lakini huyu jamaa hafai hata kidogo,
 
Sasa kama Lowassa ni mchunga ng'ombe wewe si utakuwa houseboy wa hawara yake na Mwigulu Nchemba!

Alisema mwenyewe wewe unaejipendekeza ni muongo,kafanye yako na upunguze kupiga mizinga kwa kutegemea unafiki
 
Back
Top Bottom