Wadhifa mpya wa mheshimiwa Edward N. Lowassa

Wadhifa mpya wa mheshimiwa Edward N. Lowassa

Mawaziri wakuu wawili tu waliotokea Tanzania na kuwa na mvuto pia wachapa kazi ni Lowassa na Sokoine tu lakini serikali ya ccm huwashughulikia mara moja wakiona kiongozi mwenye kupenda watu.
 
Acheni kejeli za viroba. Jamaa yuko sahihi, hadi sasa baada ya uchaguzi amani imetawala tofauti na enzi za kina muhogo mchungu. Lowassa anastahili heshima, na ukweli ni kuwa hapana wa kulingana naye.

Sasa angefanya mini nyoo angeona moto ameshindwa amaekubali kiutu uzima chapwa
 
Kama huna cha kuandika si ulale tu, lowassa lowassa mwiz mkubwa
 
What a pathetic thread, then they call themselves great tinkers! This shows how low JF has become.
 
Kumfananisha Nyerere,Mwinyi au Dr Salim na Lowasa ( ambaye maadili yake yana shaka kiutumishi) ni dhihaka ya hali ya juu sana.
Tetetetete CCM bana kwa nini msiudhihirishe ulimwengu kuwa ni fisadi kwa kumpeleka mahakamani na kutolewa hukumu?Mambo ya tetesi kila mtu anayo sifa hizo,mfano wanasema nyerere aliua watu wengi hasa ukisikika unavuma mfano Sokoine ila haya hayana msaada kwa sasa maana huwezi kuthibitisha na wenye uwezo huo wamekaa kimya.
 
Lowassa mpaka anakwenda mbele ya haki atabakia kuwa Kigogo wa ufisadi hapa Tanzania (cf. List of shame na matamko mbalimbali ya viongozi wa CHADEMA + Kubenea na Mwanahalisi). Mmejaribu sana kumsafisha lakini imeshashindikana and you can stop now. Tuiachie historia sasa lakini naamini nayo itatenda haki kwa kumhukumu kwa kuwa Kigogo wa ufisadi mwenye uchu wa madaraka aliyejaribu kununua ikulu. Mengine haya mnadanganyana tu!
 
Mmh Nyamgessi umenichekesha sana usiku huu kwa comment yako,tunaisubiri hiyo mahakama ya mafisadi itakapozinduliwa,ingawa baadhi ya viongozi wa Chadema zaidi ya miaka minane walituambia hayo,wengine wamiliki wa magazeti ya Kiuchunguzi,ambao leo hii wako ktk CDM kwa nafasi ya ubunge akina Kubenea,chama kikabadilisha gea angani na kuufuta ule usemi wa ufisadi,ni kazi kubwa mno kumsafisha mtu aliyechafuliwa kwavmiaka kumi uje kumuosha kwa siku sitini na awe kiongozi mkuu wa nchi.Nimekuelewa Nyamgessi.
 
teh teh eti JIPE MOYO ni kwer mkuu mpeni sifa zoooote lakin ikulu imepata mpangaji iko fulu nakuusu umaarufu aliupata tangu kitambo tu usimshushe mzee wa watu ila kwasasa KAZI TUU
 
Anaemdharau LOWASSA ni yule asiyeweza kuwa na fikra pevu na hata kama ana elimu chunguzeni vyeti vyake yaani ni. IPP
 
Sina lengo la kutafuta umaarufu kwa kumzungumzia mtu ambaye kwa sasa anaonekana kuwa maarufu zaidi nchini Tanzania. Ana mvuto wa pekee na kajijengea heshima kubwa katika jamii. Anakubalika kila eneo. Bara na Visiwani; Wakristo na Waislamu, Wenye kumcha Mungu na Wapagani; Wazee na Vijana; Wanaume na Wanawake wote wanamkubali.
Hauhitaji kuwa msomi sana, wala tajiri sana ili kupata umaarufu kama alionao Ndg. Edward Nyoyai Lowassa. Naweza kusema bila ya wivu wala donge kuwa Mungu mwenyewe ndiye alimjalia Ndg Lowassa karama hii. Amefanya siasa kwa miaka mingi na tumeona mazuri na mapungufu yake na hivi karibuni alijikita katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais lakini yaliyotokea sina haja wala sababu ya kuyajadili hapa lakini JIBU kila mmoja wetu analo kwa namna tulivyopokea matokeo.

Kinachonisukuma kuandika waraka huu; ni kuikumbusha jamii na Ndg. Lowassa kuwa Mungu ametujalia kumpata mtu ambaye anaweza kutumika vizuri katika kuleta mtangamano wa Kitaifa. Kwa karama yake ya kukubalika, binafsi, naona ni mtu sahihi wa kufanya usuluhishi yaani MEDIATION. Mwl. J.K. Nyerere alijaliwa kipawa hiki na alitumika kufanya usuluhishi wa ndani na nje ya nchi. Amefariki akiwa ni mpatanishi wa mgogoro wa Burundi. Ninaiona karama hiyo kwa Lowassa. Kwangu mimi hii ni hazina kubwa ambayo hatuna budi kuitumia kwa manufaa ya taifa letu.

Ninatambua wale ambao wanawaza siasa katika kila jambo wanaweza kuja na kejeli nyingi juu ya hiki, lakini ningependa mnipe mbadala wa Lowassa katika kukubalika katika jamii. Je, ni Pinda, Ben, Mzee Ruksa, JK, Salim, Mzee Wassira, au Warioba??? Kwangu mimi, Lowassa ndiye mtu pekee kwa sasa ambaye anaweza kuwaambia watu wenye jazba, tulieni na wakatulia, wenye silaha mikononi kuwa wekeni chini na watu wakaheshimu; anaweza kuwaambia wanaopigana tulieni na watu wakatii.

Baada ya maisha ya siasa, sasa ni wakati muafaka sana kwa Mzee Lowassa ukawatumikia Watanzania kwa njia hii ambayo kwangu mimi naona ina thawabu kubwa sana mbele za Mungu. Tuna migogoro ya muda mrefu hapa nchini mf. Wakulima na Wafugaji, Wachimbaji wa madini na Wawekezaji, misuguano ya kidini ya chini kwa chini nk. Migogoro hii kwa upande mwingine haihitaji mabavu au mkono wa Serikali bali watu wenye busara zao kama Ndg. Lowassa. Kama hili halitoshi, familia ya Lowassa imebahatika kuwa na Mama mwenye mvuto na ushawishi kuliko wanawake pengine wote kwa sasa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anajiheshimu, ana busara na anakubalika mno mno. Hii ni nyongeza kwa Mzee Lowassa katika kukamilisha kazi ambayo naiona imebaki katika kipindi cha maisha yake. Neno la Mungu linasema Heri Wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu!!

Mwenyezi Mungu akupe jicho la pekee Mzee Lowassa ili uweze kutumika kwa namna mpya na yenye manufaa makubwa kwa Taifa, Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla. Mungu akuzidishie maisha marefu na wote wenye kuwaza na kupanga mabaya dhidi yako washindwe.
MAISHA MAPYA NDIYO HAYA MZEE LOWASSA, TUTUMIKIE KWA NAMNA HII.

a?
Unaandika upumbavu Lowassa katoka nje ya nchi na kama hajatoka nje ya nchi migogoro ya wakulima na wafugaji alishindwa nini kuitatua mpaka leo hii unapoandika ujinga wako hapa? Matatizo ya ardhi alikuwa waziri wa ardhi alifanya nini kuondoa matatizo ya ardhi naona umeandika upumbavu wako hapa kwakuwa humjui Lowasa alipotokea na kama ungelijua usingeandika pumba zako hapa kanda ya kaskazini ina migogoro mikubwa ya ardhi na wawekezaji mpaka wananchi wanavamia mashamba ya wawekezaji na kuchoma moto mitambo yao ya kilimo huyo Lowassa wako alikuwa chooni au uvunguni mwa kitanda hakuyaona hayo? Tuliwaambia na upumbavu wenu acheni kumshabikia mtu msiyejua background zake, mnakurupuka kumbe hamjui lolote wajinga nyie kwa taarifa yako Lowasa hawezi lolote zaid ya kulalamika kaibiwa au kaonewa basi kama humjui tulize sisi tunaomfahamu.
 
Kama Lowassa ana karama na ni kiongozi bora arudi kijijini kwake awe m/kiti wa kitongoji tuonee mfano wa mafanikio kwenye kitongoji chake. Huyo hatakiwi kuonekana kuanzia ofisi za kata kwenda juu labda ofisi za Ukawa tu.
 
usipojipa muda wa kuisoma, kutafakari na kuijibu hoja kwa kuichambua hakika unaweza ukajikuta unasema lolote ili mradi tu akili imetangulia kuwaza na mdomo kutamani kuropoka. Jamii Forum - Home of great thinkers

Mimi kwangu habari yeyote inayotaka kumsafisha huyu bwana nikishasoma heading tu basi simalizii utumbo uliyobaki. Yani hii post hata sijapoteza muda kuisoma.lowassa kitu gani bwana nyie wenyewe mumuite mwizi leo hii mtuambia siyo mwizi.haingii akilini.nadhani wewe ndio unapaswa kujifikiria mara mbili kuitwa great thinker. Mpaka kesho kwa mungu lowassa kwangu atabaki mwizi na fisadi wa Mali ya umma.
 
Back
Top Bottom