Wakati siku za kufanyika kwa Tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu 2025 zikikaribia, baadhi ya wadau wameshauri kuwa, tamasha hilo lihusishe waumini wa imani zote.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao wapenda amani walisema kuwa, endapo tamasha hilo litahudhuriwa na watu wa imani moja haitapendeza kwa sababu uchaguzi huo ni wa watu wa imani zote na suala la amani linamhusu kila Mtanzania.
"Kwanza kabisa wazo la kuandaa Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu (2025) ni zuri na sahihi kabisa.
"Kwa hiyo napendekeza washiriki wawe watu wa imani zote nchini. Wakristo kwa Waislamu kwa sababu amani inatuhusu sote...
"Uchaguzi ukiharibika maana yake Watanzania wote wataharibikiwa. Kwa hiyo hata sisi Waislamu tumuunge mkono Alex Msama na wazo lake sahihi kabisa," alisema Rashidi Ally wa Mtaa wa Miteja, Temeke Dar es Salaam.
Naye Onesmo Simon wa Kawe Beach, Kinondoni alisema yeye ni muumini wa kwa Mtume Mwamposa (Boniface) lakini anatamani wachungaji na mashehe wajumuike kwa pamoja kwenye tamasha hili kwa sababu madhumuni yake yanamlenga kila Mtanzania na hata asiye Mtanzania.
"Huu ni mwaka wa Uchaguzi. Kwa kweli kumwomba Mungu atupe amani tupite salama ni jambo la msingi kwa kila mwelewa nini maana ya amani.
"Huwa tunaona nchi za wenzetu inavyokuwa wakati wa Uchaguzi Mkuu. Vurugu, vituko, mauaji na kadhia mbalimbali hutokea. Ili sisi tusifike huko lazima tumwombe Mungu," alisema Onesmo.
Hata hivyo, muandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama alisema Tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu 2025 liko wazi kwa kila anayependa amani kushiriki bila kujali imani ya mtu.
"Hili tamasha ni kwa kila Mtanzania anayependa amani. Halina ubaguzi wala upendeleo wowote. Kila mtu anakaribishwa sana tena sana," alisema Msama.
Wakati huohuo, Msama alisema tamasha hilo litafanyika Mei, 2025 badala ya Aprili kama ilivyokuwa awali baada ya kiwanja alichotarajia kufanyika kwa tamasha hilo kutumika kwa matumizi mengine.