Wadau wa demokrasia mnauonaje huu ujumbe?

Zeni2017

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
1,247
Reaction score
534
9621b8ab5cb92e69f8f90dbcd24d683b.jpg

Kwa kifupi Franklin Roosevelt rais 32 wa Marekani alisema ili demokrasia ifanikiwe wanaofanya maamuzi ya kidemokrasia ni lazima watumie busara. Hivyo basi kitu pekee kinachoilinda demokrasia ni ELIMU.
 
CCM fed up with democracy things, we are at war

Hakuna kulala Mullah
 
Kwa hiyo tungemchagua Fisadi siyo?vipi ile inayosema ni heshima kumzomea fisadi?
 
9621b8ab5cb92e69f8f90dbcd24d683b.jpg

Kwa kifupi Franklin Roosevelt rais 32 wa Marekani alisema ili demokrasia ifanikiwe wanaofanya maamuzi ya kidemokrasia ni lazima watumie busara. Hivyo basi kitu pekee kinachoilinda demokrasia ni ELIMU.
Huko kwa Roosevelt kwenyewe kwa sasa demokrasia ina hali gani?
 
Busara inatumika mkuu. Pamoja na kuwa kuna rais nusu kichaa hakuna kiongozi anaewaambia wananchi wote wenye akili timamu wampinge rais. Wananchi wenye akili timamu ni pamoja na jeshi.
 
Mtaji mkubwa wa wahuni na mafisadi wa MACCM ni MAZWAZWA wa nchi hii.
Kiongozi, sidhani kama unafahamu kuwa mtaji mkubwa wa wanasiasa ni hao wanaojiita WASOMI?

Kama unaongelea wapiga kura wao, jua pengine si wote walipita kwa karatasi. Mathalani, inasemekana mbunge mmoja kutoka kusini alipitishwa na mtu mmoja tu.

Ila kama nchi kufika hapa, ni matokeo ya WANASIASA, WASOMI na WABINAFSI. Mtu mmoja anaweza kuwa na sifa zote hizo tatu.

Wanaosaini mikataba mibovu, wanaoidhinisha EPA, wanaotunga sera, wanaosimamia, wanaohusika na masuala ya fedha, na woooooote wafananao ndio wametutumbukiza huku tuliko.

Pengine LEO utuambie, WASOMI wengi wa nchi hii ni MAZWAZWA.
 
Katika population zaidi ya Watanzania milioni 50 wasomi ni percentage ndogo sana ya wapiga kura wote nchini.

Back
Top Bottom