Wadau Nimeambiwa nitume Signed CV nifanyeje?

Wadau Nimeambiwa nitume Signed CV nifanyeje?

!
!
Elimu yako tafadhali ili nitoe ushauri stahiki. Vyeti saba? vya ubatizo na kipaimara usingeviscan umepoteza hela bure. Na hicho cha graduation ya dini sio cha muhimu.
We jamaa mhurumie huyu msomi mwenzio, elimu za mwendokasi hizi. Daaah nimecheka kwa sauti mno [emoji1] [emoji1] [emoji1] eti vyeti vya ubatizo na kipaimara mamamaaaee binadamu hamfai [emoji114] [emoji114]
 
Acha kupanic ndo unasaidiwa hivyo, kwa hizo mastazi za kurithi bora angezikwa nazo tu marehemu. Kifupi ni kwamba zipo kwenye vyeti tu na sio kwa bichwa, labda kama hiyo kazi umeahidiwa mradi vyeti tu.

Usile Mbegu.


!
!
Sijawahi ona jitu jinga kama hili. Yaani masters mzima ukakahanye kuscan doc saba? achana na hiyo pamoja na cheti cha computer juu halafu ashindwe kupata suluhu ya kitatizo kama hicho? nimeshindwa kumuelewa huyu msomi.
 
Hili nalo jipuu!!
Sijui nibadilishe mfumo wa kuajir watu???!!!!!!
Maan naona hata wenye vyeti halisi vilaza tu.
Wamekula mbegu!!!
 
!
!
Basi nikushauri umrudishie mwenyewe vyeti vyake havitakusaidia huko uendako. Kama ni vya urithi vitengenezee fremu uvipambe sebuleni. Kifupi bandiko lako halifanani na hivyo vyeti.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hata mimi nimeona bhana
 
Huyu amezidi
Assignments alikuwa hafanyi nn ?
Mm std 7 naweza sign kupitia tu kasimu kangu barua n documents zangu za std iv
Eti mwenye master anashindwa teh teh
Hakuna haya ya kwenda shule
Hawa ndio wanaoenda kuchukua n sio kusoma
 
Huyu amezidi
Assignments alikuwa hafanyi nn ?
Mm std 7 naweza sign kupitia tu kasimu kangu barua n documents zangu za std iv
Eti mwenye master anashindwa teh teh
Hakuna haya ya kwenda shule
Hawa ndio wanaoenda kuchukua n sio kusoma
Pia ana cheti cha Computer, sijui alikipataje.
 
Chet
Pia ana cheti cha Computer, sijui alikipataje.
Si makaratasi tu!




KUFANIKIWA KATIKA MAISHA SIO ELIMU TU, BALI NA UJASIRI WA KUJIAMINI NA KUTHUBUTU!

Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa.

Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi na magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!).

Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.

Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga.

Hii inachangiwa na mambo mawili.

1⃣ Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli.

Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio.

Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika.

2⃣ Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani.

Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti.

Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze.

UKWELI MCHUNGU!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom