Wadau naomba msaada

mwankuga

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
334
120
Wadau,nina kaka ambaye ana miaka 31 na bado hajatahiriwa kutokana na sababu nyingi ikiwemo mila na desturi za kwetu.

Kwa kuwa tumezoeana sana tumekuwa tukijadili sana suala hili,ili aweze kutahiriwa hasa tukijua kuwa kutahiri kunapunguza kwa asilimia kadhaa kuambukizwa HIV/AIDS.

Yeye yuko tayari kutahiriwa,lakini tatizo anaona aibu kwenda hospitali akiamini atachekwa,na pili anasema anaweza kupata madhara ikiwemo kupungua nguvu za kiume.

Naomba ushauri wenu wadau,ili kaka yangu aweze kusafishwa.
 
Kuhusu hilo la kuambukizwa ukimwi not real sure..... But for sure ukitahiriwa inapunguza stim, kwa ushauri wangu kama hana shida ya kuimbiza na vimeo.... akae hivyo hivyo :coffee:
 
Nguvu za kiume hazitapungua na pia hakuna ambaye atamcheka kwa uamuzi huo.
 
Anaogopa nini sasa?aibu kwani inatangazwa?kama vipi akatahiriwe sehemu watu wasiyomfahamu.....ili asione aibu!!!Nguvu za kiume zipo tu kama anazo,so ni bora kuwa na nguvu za kiume kuliko kuwa katika risk kubwa ya kupata maambukizi???

Pole sana,tumia uwezo wako wa kike kumshawishi aende kutahiriwa:coffee::coffee:
 
Mimi dr, hakuna wa kumcheka kwani hayo ni majadiliano kati ya yeye na daktari. Lakin akibaki hivyo uchafu unaokusanyika waweza sababisha kansa kwake na pia mkewe ile ya shingo ya kizazi ni moja ya visababishi. Hivyo asiogope aende tu.
 
Ushauri wako mheshimiwa ni mzuri,nitaendelea kumshawishi kwa maana napata hoja zaidi za kushawishi,nashukuru
 
Hajawahi ku do huyo au?
Nashindwa kuelewa hajaogopa mbele ya mtoto wa kike, akaogope kwa daktari!
 
Anaogopa nini sasa?aibu kwani inatangazwa?kama vipi akatahiriwe sehemu watu wasiyomfahamu.....ili asione aibu!!!Nguvu za kiume zipo tu kama anazo,so ni bora kuwa na nguvu za kiume kuliko kuwa katika risk kubwa ya kupata maambukizi???

Pole sana,tumia uwezo wako wa kike kumshawishi aende kutahiriwa:coffee::coffee:
Nashukuru kwa ushauri wako Michelle,ila mie ni mwanaume,asante
 
Back
Top Bottom