Dkt. Gwajima D
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 543
- 3,575
Ndugu Wanajukwaa, nawasalimu kwa Jina la JMT.
Kwa heshima tafadhali pokeeni ujumbe huu wa Wizara yenu ya Jamii, Ili twende Pamoja kwa Maendeleo na Ustawi wa Jamii.
Kesho 9 hadi 11 Okt 2023 tunaanza Mkutano wa Kimataifa wa kutokomeza Ukeketaji.
1. Mkutano huu utaenda sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo huwa ni tarehe 11 Okt kila mwaka.
2. Kuhusu ukeketaji kwa watoto wa kike; takwimu za Afya, Idadi ya Watu na Viashiria vya Malaria mwaka 2015/16; Ukeketaji umepungua kutoka 30% mwaka 2010 hadi 10% mwaka 2015. Mikoa yenye takwimu za juu ya wastani; Manyara (58%), Dodoma (47%), Arusha (41%), Mara (32%), Singida (31%) na Tanga (14%).
3. Kutokana na utekelezaji wa Sheria ya kuzuia vitendo hivi, baadhi ya jamii imekuwa ikikeketa watoto wadogo na wachanga ili isifahamike na kushtakiwa. Imetungwa Sheria ya Kanuni ya Adhabu kifungu 169A na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 na pia, Serikali na Wadau wanatoa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii kuhusu madhara ya ukeketaji ili waachane na mila hiyo.
4. Kwa Afrika, jitihada za pamoja zinahitajika. Hivyo, Tanzania ilishiriki Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Kutokomeza Ukeketaji nchini Burkina Faso mwaka 2018 ulioazimia kila Kanda Afrika ianzishe ushirikiano wa kupambana na mila na desturi ya ukeketaji ikiwemo kudhibiti mipaka ya nchi kuzuia mwingiliano wa mila.
5. Umoja wa Afrika umeichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Kutokomeza Ukeketaji ambao umepangwa kufanyika tarehe 9 hadi 11 Oktoba, 2023 DSM, Ukumbi wa JNICC. Mkutano huo utakutanisha Washiriki 900. Kaulimbiu ni “Mabadiliko katika kizazi kimoja kwenda kingine ni muhimu katika kutokomeza vitendo vya ukeketaji”.
6. Sambamba na mkutano huo, kutafanyika pia Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike tarehe 11 Oktoba. Kaulimbiu ni "Haki Zetu ni Hatima Yetu; Wakati ni Sasa”. Aidha, Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike Tanzania itaadhimishwa pia mikoa yote chini ya uongozi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
7. Kwenye kipindi hiki pia kutakuwa na mkutano mwingine wa Ajenda ya Wasichana wenye Kaulimbiu Mimi ni Nani?: Kubadili Tamaduni na Mazoea ili kujenga Kizazi cha Wasichana Wanaojiamini’’ ambao utafanyika tarehe 11 Okt, 2023 ukumbi wa Mlimani City Jijini DSM, 3.00 asubuhi.
Mikutano yote 3 inashabihiana kimkakati.
Ahsanteni sana, naomba kuwasilisha.