Wadau naomba kuuliza swali kuhusu serikali ya Tanzania na ujenzi wa shule za sekondari

MZAWA JF

JF-Expert Member
Apr 4, 2014
4,120
3,346
Ni zaidi ya miaka 50 tangu tujitawale wenyewe. nimetafakari sana kuhusu hali ya miundombinu ya shule kongwe za sekondari za serikali ilivyokuwa mbaya kwa sasa. hizi shule tumezirithi toka kwa wakoloni lakini zilikuwa full(madarasa,maabara,maktaba,nyumba za staff kuanzia headmasters/mistress hadi wapishi, viwanja aina nyingi, halls,majiko nk)

Baada ya kuanza kuchakaa miaka ya 90 wakaja DANIDA kuzifanyia ukarabat. mwaka jana ukaja mpango wa kukarabati na ujenzi wa sehemu ya miundombinu ya shule mbili za sekondari ktk kila wilaya chini ya WORLD BANK.

Serikali imehamasisha wananchi kujenga shule nyingi za kata huku yenyewe ikiSAIDIA. Swali langu kuu ni je, serikali haiwezi kujenga shule zake kwa nguvu zake yenyewe? Naomba mtu anayejua shule iliyojengwa kwa mkono wa serikali ikakamilika (full) atutajie. hapo juu nimeshaeleza maana ya shule full. Karibuni tujadili kwa faida yetu.
 
Kuna mahali tulikosea.In real sense tulilala kidogo mfano kuna kipindi hata program ya sensa ilisimama.Imagine huwa tunaandaa bajeti kila mwaka mara moja bila kuwa na uhakika hata wa idadi ya tunaowaandalia.

Mengi huwa tunayakurupukia tu.Mfano Shule za kata tulijenga nyingi lakini zisizokamilika! Licha ya kutokuwa na uwezo wa kuzihudumia mf. walimu wasiotosha,Maabara hakuna,vitabu n.k.Halafu tunakimbilia kuwalaumu watendaji yaani walimu kuwa hawafanyi kazi.

Niseme kuwa Serikali yetu haina uwezo wa kujenga chochote bila msaada kutoka nje.Na in case tunafanya tunajali quantitatively and not qualitatively.
 
Back
Top Bottom