Wadau mnaishije na ndugu?

Wanaume walozungumzwa kwenye vitabu vya dini ni wewe na mume wangu#kiddingπŸ˜…
Hongera sana ww ndo definition ya mpambanaji
Kuhusu huyo ndugu yako mu ignore inapowezaka sehemu ya kumpiga tafu fanya hivyo ila usichukue mkopo
kwa ajili yake
Asante dada yangu kwa ushauri
 
Hata mwanamke alie nae amechangia sana kumfanya jamaa atoboe, yaani ana wife material jamaa ali bahatisha aisee sio sie tunakutana na vikosi vya mizinga AkA golddiggers. Wanawake wa sasa wenye akili ya maisha ni wa kubahatisha sana..
Sie wengine tumekutana na misukule
 
We jamaa Mbona ulisema mwaka jana upo Mpanda una Lima!

 
Wanaume walozungumzwa kwenye vitabu vya dini ni wewe na mume wangu#kiddingπŸ˜…
Hongera sana ww ndo definition ya mpambanaji
Kuhusu huyo ndugu yako mu ignore inapowezaka sehemu ya kumpiga tafu fanya hivyo ila usichukue mkopo
kwa ajili yake
Una uhakika si chai
 
Muendelezo
Wadau kipindi nachukua mkopo nilichukua kwa furaha huku nikijua kuwa naenda kumsaidia mtu aliye nisaidia. Kumbe yeye amefanya kama kitega uchumi nakumbuka 2015 kipindi nimehitum chuo .yule kaka yangu aliyekuwa ameajiriwa alichukua mkopo ilikumsapoti broo mkubwa ila cha ajabu ile hela aliivuruga bila kuifanyia chochote ikaisha na maisha yakaendelea kuwa magumu.



Sasa wadau kwa upande wangu kiukweli baada ya mimi kuanza kazi nilijibana sana nikanunua kiwanja kwa shilingi milioni moja hapa nilipojenga sasa .nimoja ya makao makuu ya wilaya moja wapo wilaya za mkoa wa geita.

Baada ya kununua kiwanja nikamshirikisha kaka nikijua yeye kama mzazi wangu atafurahia nilichofanya kumbe nilikosea
Nilivyomwambia alikasirika sana na akasema ninaroho mbaya najiangalia mwenyewe.
Ndipo akatuita kikao nyumbani akahitaji mkopo nikaenda kumchukulia


Wadau kwa nilichojifunza kwenye maisha usiri ni jambo la muhimu sana baada ya kumsoma broo nikakaa na mke wangu tukashauriana nikamwambia kwamba kuanzia sasa hakuna kumwambia ndugu jambo lolote linalohusu maendeleo yetu hapa ni suala la ukimya
Nakweli hichokitu kimetusaidia japo kidogo .

Nilichagua kukaa kimya ndugu yangu yeyote simuambii chochote akija kunitembelea atakachokikuta akitaka atangaze au akae kimya shauri yake .

Turudi nyuma niwasimulie jinsi tulivyo anza mahusiano. Na huyu mke wangu. Ilikuwa hivi kipindi nimechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza nilibahatika kupelekwa shule ya makao makuu ya wilaya yetu nilianza vizuri kidato cha kwanza mwaka 2006
Shule ile ilikuwa day hivyo nilipanga mtaani kama wanafunzi wenzangu nilivyofika kidato cha pili nilitokea kumpenda mwanafunzi mwenzangu ila kutokana na yeye kuwa maisha bora hakunipenda kivile ikawa nikimtongoza ananitukana sikukataa tamaa sikumoja alikuja kwangu geto akakuta nalalia jamvi maana hata godoro sikuwa nalo da alinihurumia sana na akanishauri niachane na mapenzi nisome kwa juhudi siku hiyo alinitunuku tunda kiikweli nilimpenda sana ila baada ya kumaliza mtihani wa kidato cha pili ndio ilikuwa mwisho wa kuonana nae.
Maana alikuja kuhama shule ukizingatia hata cm tulikuwa hatuna.Nilivyorudi kuingia kidato cha tatu nikaja kuambiwa grace amehama shule niliumia sana ila sikuwa na lakufanya zaidi ya kuwa mpole.

Niliendelea kusoma kwa juhudi ilivyofika 2008 mwezi wa sita nikawa nimekutana na huyu mke wangu yeye alikuwa anasoma nilivyomtambua ilikuwa ni hivi huyu mke wangu alikuwa na urafiki na dada fulani tulikuwa tunasoma nao darasa moja hawa madada walikuwa watoto wa mchungaji siku moja nimeenda kuazima daftari la notsi niandike ndio namkuta huyu mke wangu nilivyomuona nikamtamani sindio nikaongea na hao watoto wa mchungaji wakaniambia ni rafiki yao.


Wakawa wananitania kuwa nimekapenda. Baada ya hapo nikaanza kukafatilia kimya kimya bila kumuambia chochote nikaja kugundua kumbe tunakaa jirani sema tumetenganishwa na kanisa hilo.

Unajua mimi ni mtu ambaye sikuwa na mambo mengi sanq mimi nilikuwa ni mtu wa shule tu ndiomaana hata huyu sikuwa na mjua mapema .

Sasa sikumoja baba yake nilikutana nae ameanguka na mzigo wa unga kumbe alikuwa ametoka kusaga kwakuwa nilikuwa namjua ila yeye hanijui nilimsaidia mzigo hadi kwake mungu saidia nilimkuta yule demu anaosha vyombo baada ya kutua mzigo mzee alinishukuru sana na akaniuliza nakaa wapi nilimuelekeza akapajua.

Sasa hapo ndio ikawa mwanzo wa yule demu kunijua tukqwa tukikutana nae tunasalimiana .sikumoja nimeendq kusali jumuia nikakutana na mama yake nikamsalimia nikamkumbusha akanifahamu

Mwanzo wa kumtongoza.
Nakumbuka ilikuwa mwezi wa nane 2008 ndio nilianza kumtongoza huyu mke wangu yeye alikuwa anapenda kupita jirani na nilipokuwa nimepanga kumbe alikuwa analala kwenye nyumba ya kaka yake.

Yeye alikuwa akishakula kwao anapita pale karibu na kwangu anaenda kulala kwa kaka yake.
Sikumoja nikamuita akaja tukaanza kuongea nae tukawa tumezoeanq na akaanza kunipenda sasa kimbembe kikawa kutoa tunda ikawa kazi tulienda hivyohivyo hadi nikafunga likizo ya mwezi wq kumi na mbili 2008 bila kula mzigo nikawa nimerudi kijijini kwetu .

Mwezi wa kwanza 2009 Tulivyofungua shule hapo nimeingia kidato cha nne nilirudi na nguvu mpya ya kujisomeq kwa juhudi zote ila yule demu akawa ameingia kidato cha pili lakini shule nyingine.

Tuliendelea kutongozana kufika mwezi wa nne ndio akanitunuku kiukweli nilikuta bikra nifurahi sana kiukweli japo kumla ilikuwa ngumu lakini kwa mara yakwanza nikutoa bikra ilikuwa hapo

Sasa penzi likanoga muda wote wa jioni tuponae kanisani jumapili akawa ananipitia tunaenda nae kusali kama mke na mme jumuiya alikuwa hasali akaanza kusali kwaajili yangu .

Mtaani wakaanza kujua huyo demu ni demu wangu kama mnavyojua mapenzi ni upofu tukawa tunajiachia vichochoro vyote vikatujua.

Vurugu za kaka zake.

Baada ya kuwa mapenzi yamenoga huku nyuma kaka zake wakawa wamesikia nipo nae wakaanza kuniwinda sikumoja walinikamata nae usiku wa saa mbili nilikula kipigo cha mbwa mwizi demu alikimbia aise kesho yake ilikuww jumapili demu hakuja kunipitia namimi mwenyewe nilikuwa nachechemea hapo ni mwezi wa nane 2009.

Baada ya kukaa kama siku mbili mida ya saa nne usiku nikonasoma nikasikia dirisha linagongwa kumbe alikuwa yule demu nilivyotoka aliniomba msamaha na kunihurumia sikuhiyo nilimgonga hapohapo nje tukawa tumepanga ratiba mpya ya kuonana maana ilikuwa muda wa kulala akitoka kwao kaka zake wanamfuata nyuma kwahiyo alikuwa anapitiliza ikifika saa sita usiku anakuja kugonga dirisha tunaonana nae .


Tuliendelea hivyo kumbe mmoja wa kaka zake akagundua sikumoja akanifata mchana akanipiga biti sana nikawa nimeogopa nikaanza kuwa sikai geto nikitoka tu shule naenda kwa jamaa yangu kusoma demu akapeleleza akapajua akawa ananifata hadi huko.

Sikumoja bwana tumeenda kanisani ile tunaingia getini tukakutana uso kwa uso na kaka yake mkubwa kwa kuwa ilikuwa kanisani alinikaushia sasa muda ule misa imeisha umefika muda wa matangazo nikatoka ilinisepe kumbe demu nae kaniona akanifata tukawa tumetoka nae huku mda wote nawaza leo itakuwaje kumbe kaka yake katuona akatufata na pikipiki yake kidogo anipamie niliruka kwa pembeni akamchukua dada yake hadi kwao.


Mimi nikapitia kwa jamaa yangu kumuelezea nilivyotoka hapo nikaenda geto nafika tu demu huyu hapa akawa ameniambia kuwa kama kaka zake wakinifata kwenda kwao nisigome napia niseme kuwa namfundisha tuisheni pia ameshampanga mama yake .


Kweli kufika saa kumi jioni nikaijiwa na kaka zake wawili nikabebwa kama mwizi kufika kwao nakuta kaka yake mkubwa,mama yake na baba yake wote wapo nikawekwa mtu kati nilipigwa biti sio la kitoto kaka yake akadai kesho atakuja kwa mkuu wa shule ili nifukuzwe shule.kiukweli nilitetemeka sana isitoshe huyo kaka yake alikuwa mwalimu wa primary.

Kesho yake akaja shule akaonana na mkuu wa shule nikaitwa uzuri ni kwamba shuleni sikuwa na skendo yoyote hatq mkuu wa shule alikuwa ananifahamu kwahiyo nilionywa tu nikarudi darasani.


Mapenzi nikitu kingine tuliendelea kuwa nae kwa siri hadi nikamaliza shule nikarudi kijijini kwetu niliumia sana kumuacha nilivyofika home nikakuta kaka amefungua kiduka nikawa nauza nikaiba hela nikanunua simu lengo niwe nawasiliana na demu wangu maana kipindi hicho kijijini kwetu kulikuwa na mnara wa celitel na nilivyotoka shule nilikuwa nimechukua namba ya mtoto wa kaka yake ambaye ni wakike nikawa naazima simu tunawasiliana na demu wangu kwahiyo nilivyonunua cm alifurahi sana akawa ananibipu nampigia .


Matokeo yalivyotoka nikawa nimepata division two ya 20 alifurahi sana nilivyomuambia kuwa nimefaulu nikapangiwq shule ya mwenge singida.

Siku ya kwenda kulipoti nikapita hapo wilayani kuchukua join nikaenda na kuonana na demu wangu nilifika hadi kwao nikamsalimia mama yake alikuwepo mama yake alifurahi sana hadi yule kaka yake mwalimu alinipongeza akanishauri nikasome kwa juhudi sana kiufupi nilikuwa natamba nilijiona shujaa .


Nikawa nimeenda advance kule sikuwa na mademu kwwnza shule ilikuwa boys tupu .niliendelea kuwasiliana na demu wangu akawa aninitumia hela kupitia akauntinya bank ya nmb ya jamaa yangu maana kwao kidogo walikuwa na unafuu wa maisha.

Nilivyokuwa nakuja likizo nilikuwa nafikia geto langu maana nilikuwa nasoma tuisheni hapo mjini nilivyomaliza advance nikafaulu nikawa nimepangiwa chuo hapa siwezi taja maana tafahamika.


Huko chuo niliendelea kuwasiliana na demu wangu yeye alivyomaliza kidoto cha nne alifeli akawa amekaa tu home ananisubilia tulikuwa tumepanga nikimaliza chuo tuoane

Baadae akaenda dar kwa dada yake akawa anafanya biashara akawa ananitumiq vihela nakumbuka kunakipindi nilimdanganya nimekwama ada akanitumia laki moja na nusu tuliendelea kuwasiliana nae nilipo maliza chuo nikarudi home hapo kaka alikuwa amehamia mpanda kama nilivyoeleza hapo mwanzoni .

Tukapanga nikiajiriwa ndio tuoane da kipindi cha magu ajira ikawa ngumu ndio kama nilivyoeleza huko juu ila tulikuja kuoana 2017 mengine yote nimeshaeleza huko juu .

Hadi leo tupo nae na mtoto wetu kipenzi .

Kwa upande wa kaka zake kwasasa wananiheshimu sana nikienda kwao nachinjiwa kuku tu .yule kaka yake mkubwa aliyetaka kunipamia na pikipiki alikuja kunitembelea kwangu mwaka jana nilimchinjia bonge la jogoo akafurahi sana kwasasa tumekuwa mandugu wananiheshimu sana na kunijari


Kuhusu mama mkwe wangu kipenzi bahati mbaya Mwaka 2020 mwezi wa nne alifariki kwa presha alianguka bafuni .huyu mama mungu amrehemu alikuwa msaada kwangu hatq kipindi tupo dar alikuwa anatutumia hela ya sikukuu nilikuwa nikiibiwa cm ananitumia hela nanunua cm nyingine .

Kiufupi alikuwa ananipenda na alikuwa anamshauri sana mwanae aendelee kuwa mvumilivu kwangu ipo siku tutafanikiwa.


Kiukweli hata familia ilivyosema mchango wa ujenzi wa kaburi nilitoa kwa moyo mmoja kabisa nimepanga kama tapata mtoto wa kike nitampa jinanla mama mkwe wangu .Maana huyu niliyenae sasa niwakiume nilimpa jina la mzee wangu.

Kww upande wa baba mkwe wangu yupo hai na huwa tunawasiliana.

Asanteni sana wadau kwasasa nakomaa na changamoto za ndugu zangu .

Ipo siku takuja kuhadithia wivu mke wangu maana anawivu sana ila sitokuja kumuacha maana amenivumilia wakati wa shida zangu acha nayeye nimvumilie .

Asanteni sana wakati mwingine .Tusameheane kwa muandiko labda siko vizuri kwenye kuandika ila najua ujumbe umefika.

Mwisho.
 
Huko mpanda naendaga kulima yupo kaka yangu na mdogo wangu ila mimi nimuajiriwa wa serikali huko naenda sana nalima mahindi maeneo ya mpanda ndogo/ majarila
 
Kichwa cha habari πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Dah,mzee unajua kupambana,hadi mkaa umechoma?
Ndio maisha yetu mzee nikupambana kazi ya mkaa ni nzito nilikonda hadi zile nguo nilizotokanazo chuo zilinipwaya nikaenda kuzimodoa
 
MIMI NI MWANAUME MWEZAKO ILA NDUGU YANGU UKITAJIRIKA NA UKAJA KUMUACHA HUYO MWANAMKE AU KUMNYANYASA KWA AINA YEYOTE ILE MUNGU ATAKULAANI .. HUU NI UKWELI NA KUAMBIA MAANA SISI WANAUME TUKIPATA KAZI NA HELA HUAGA TUNASAHAU WAKE ZETU TULIO TOKA NAO CHINI MAVUMBINI.
 
Mkuu pole sana kwa changamoto ulizopitia ila hongera sana kwa ukakamavu na upambanaji,ila sasa mkuu yaan wewe na kaka yako mnachukua mkopo bank kumpa bro wenu !bora angekuwa mama yako tena kwa dharula hasa ya ugonjwa,
Kama ni msaada ni bora uwe unampa pesa ndogo ndogo unapoipata kama elf 50,000 napo ukiwa nayo kama huna nafasi unamwambia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…