Wadau mnaishije na ndugu?

Wadau mnaishije na ndugu?

shuka chini

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2024
Posts
1,509
Reaction score
2,995
Habari wadau mimi ni kijana wa 30+ nina mke na mtoto mmoja ni muajiriwa wa serikali .

Nilimaliza chuo mwaka 2015 ila nikaajiriwa 2021 kipindi namaliza chuo nilipitia wakati mgumu sana wa ukosefu wa ajira nikaamua kwenda mpanda kwenda kukata mkaa nilipopata hela nikakodi shamba nikalima mahindi Mungu akasaidia nikapata gunia kumi nikauza yote kwa 480000 hiyo ni mwaka 2016

Baada ya kuuza na mkaa niliyokuwa nimechoma nilipata kama laki sita jumla da nikaamua kuhama kuja mwanza nikapanga maeneo ya kirumba mlimani nikaanza biashara ya kufata dagaa kisiwani nakuja kuuza mwaroni kirumba bahati mbaya madalali wakanipiga hela nikawa nimefuria huku nyuma mpenzi wangu akawa anahitaji aje tuanze maisha .

Nilimsihi anivumilie lakini akalazimisha kuja akapewa mchele ,unga, na vyombo akajanavyo hatimae nikawa nimeoa . Baada ya kuoa ndio nilikuwa nimejiongezea matatizo nilipitia wakati mgumu sana wa kiuchumi nilikonda hadi nikawa nawakimbia watu niliosoma nao nikiwaona mwanza.

Nikaanza kuwa natafuta vibarua vya ujenzi pia nikawa nafanya kazi za bustani kupanda ukoka na majani kwenye nyumba za watu hiyo kazi nilipewa na jamaa yangu anaitwa zabroni yupo hapo mwanza misheni karibu na kanisa la makongolo.

Muda nafanyanae kazi alikuwa hajui kama nimesoma nilijaribu kuficha mambo yangu.jamaa alikuwa anachukua tenda sisi tuna kuwa kama vibarua tumefanyq nae kazi maeneo mengi mfano isamilo,maina bendera tatu, bugarika pasiansi na sehemu zingine.

Lakini maisha yakawa yanazidi kuwa magumu sana.mke wangu akanishauri tuhamie dar maana yeye aliwahi kuishi dar sasa kimbembe kikawa nauli ikabidi tushauriane maamuzi yakawa aombe hela kwa mama yake.

Mama mkwe alikuwa ananipenda sana maana nilionesha mapenzibya dhati kwa mtoto wake na pia alikuwa anampenda mwanae ikabidi atutumie laki mbili nikatoa safari ya dar ikaanza

Tulisafiri kwa treni muda huo tuna godoro tu na vyombo tulivyofika dar akaniambia tukatafute chumba manzese siku hiyo hatukupata hiyo ilikuwa 2017 octoba

Tukalala gesti maeneo ya kigogo kesho yake akashauri twende kongowe njia ya kwenda vikindu tukaenda tukampata dalali tukapta chumba cha giza shilingi 15000 kwa mwezi tukaanza maisha hapo muda huo vyombo tunavyo kimbembe kikawa godoro kumbe behewa la mizigo lilibaki Tabora.

Ikabidi tulale chini bila godoro kwa muda wa wiki mbili ndio godoro likawa limefika tukalifata paceli .

Sasa ninanza maisha ya dar je nitafanya kazi gani .

Nikawa nazurura nakutana na waruguru wanauza ndizi mbichi ,njegere, na mbaazi nikawauliza wakanieleza wanapozitoa

Nikaenda kushaulianq na mke wangu akasema anapajua mabibo ataenda kuangalia ndizi

Kesho yake mke wangu nikamsindikiza stendi kongowe mwisho saa kumi usiku tukakubaliana tukutanie mbagala rangi tatu nakumbuka alienda na 15000 kama mtaji akaenda kununuq mikungu miwili ya ndizi bukoba tukaja tukagawana nusu kwa nusu.

Tukagawana mitaa ya kuuza maeneo yq kurasini mji mpya hapo mitaa siijui siku yakwanza nakumbuka tulipata faida ya shilingi 10000 ukiondoa mtaji

Tuliendelea kuwa tunauza nae ikabidi aniambie niwe naendq mimi sokoni kuchukuwa mzigo nikawa naenda mimi tunagawania mbagara tunauza kwa kichwa kila mtu mtaa wake .

Kumbe tulipotoka mwanza alikuwa mjamzito ikabidi tumbo lilivyofika miezi mitano akanza kuumwa ikabidi hospitali washauri apunguze kazi nzito ikabidi nimpumzishe nikaanza kukomaa mwenyewe hatimae nikawa na jina kwenye mabaa mengi nikawa nasambaza ndizi mzuzu na mshale.

Muda wa kujifungu ulipofika 2018 nikamsafirisha mkoani kwetu akaenda kujifungua mimi nikabaki nakomaa nilipata hela kweli mke wangu akajifungua kwa oparesheni mtoto wa kiume nilifurahi sana toto tunafanana nalo sana

Kule alikaa miezi miwili akarudi dar muda huo ninavihela tukashauriana tuhamie mbagara kibonde maji tukapanga nyumba ya umeme nikanunua tv ya chogo na sabufa sipiano alivyo baadae mke wangu akanishauri baskeli.

Ngoja niwakumbushe kitu kipindi tupo kongowe tuliweza kununua kitanda na godoro mpaka anaenda kujifungua tulikuwa tumesha nunuq hivyo vitu.

Tuendelee nikaenda kununua baskeli maeneo ya china plaza .

Nikaqnza kuuza ndizi kwa baskeli nikakipumzisha kichwa. Nikauza sana tu hapo kibonde maji kulitokea wizi ikabidi tuhamie kurasini mji mpya

20218 Serikali ikatangaza ajira nikaomba nikakosa niliumia sana ila mke wangu akanifariji sana nikazoea

Mungu saidia 2020 mwishoni nikapata ajira nikaanza kazi 2021
Pia nilikuwaga naomba kazi private lakini sikuwahi kupata

Kesho tutaendelea na kiini cha stori yangu. Ila niwakumbushe kuwa huyu mke wangu tulianza nae mahusiani 2008 mimi nilikuwa kidato cha tatu yeye cha kwanza ndio huyu tupo nae mpaka leo
 
Muendelezo.
Baada ya kupata kazi ilibidi tuhame dar kuja mkoani geita nilipo hadi sasa .ngoja niwarudishe nyuma makuzi yangu mimi ni mtu ambaye nilifiwa na wazazi wangu wote wawili kabla hata sijaanza shule kwahiyo tulilelewa na babu na bibi mwaka 2004 babu alifariki ikabidi mzigo wa malezi au bebe kaka mkubwa.

Yeye alikuwa mkulima tu hapo kijijini kwetu tumekuwa kwa tabu sana mungu saidia kati yetu wawili tumebahatika kuajiriwa wanne sio waajiriwa maana tupo sita na wote ni wakiume mimi wapili kutoka mwisho.

Changamoto za kifamilia

Kipindi nipo shule kaka yangu mkubwa alipata matatizo ya kimaisha ikampelekea kuyumba sana kiuchumi nikawa namtumia hela ndogondogo za boom na kaka ninae mfata ndio alianza kuajiriwa akawa amechukua mkopo kumsaidia broo mkubwa akawa amehama mkoa akaenda kununua mashamba na kuanza upya.

Sasa changamoto ya kaka yetu mkubwa ana matumizi mabaya sana anapenda wanawake na amezaa sana anawatoto timu ya mpira na lizevu watatu
.Huyu kaka niliyemfata amekuwa akichukua mikopo kumsapoti lakini kila mara analalamika tu .

Mimi mwenyewe nimekuwa nikimshauri kuacha tabia ya kuzaa sana ila amekuwa akikasirika sana kusema ukweli kaka yangu ni mpambanaji sana tatizo ni matumizi yake ndio mabovu huwa naumia sana basi tu .

Nilivyoingia kazini mwaka wapili tu yaani 2022 akawa ametuita nyumbani kumbe lengo lake ni kumchukulia mkopo pendekezo likawa kwangu kwamaana sijawahi kuchukua ikabidi nichukue milioni nne mbili na nusu nikamtumia kaka moja na nusu nikaongezea kupaua ka nyumba kangu nilikuwa nimeanza kujenga kadogo tu

Sasa shida ilianzia hapo ninamkopo wa chuo na huo wa nmb ila najikaza mungu anasaidia mdogomdogo.

Baada ya mwaka mmoja kaka yangu akataka nichukue tena mkopo hapo ndipo mgogoro ulipoanzia muda huo ninamkopo wa miaka mitatu tamaliza mwaka huu mwezi wa kumi na moja sasa anataka tena nimkopee tena da nikawa nimegoma na nikamueleza ukwelo ila haelewi .

Ukiondoa huo mkopo niliompa kuna hela nyingi nilikuwa na mtumia karibia laki tano.

Sasa wadau sio kwamba ninaroho mbaya ila kaka anatumia sana kuhonga wanawake maana hata shemeji alishalalamika sana kuhusu tabia yake.

Ninapitia wakati mgumu sana sijui wadau nifanyaje
 
Wanaume walozungumzwa kwenye vitabu vya dini ni wewe na mume wangu#kidding😅
Hongera sana ww ndo definition ya mpambanaji
Kuhusu huyo ndugu yako mu ignore inapowezaka sehemu ya kumpiga tafu fanya hivyo ila usichukue mkopo
kwa ajili yake
 
Habari wadau mimi ni kijana wa 30+ nina mke na mtoto mmoja ni muajiriwa wa serikali .

Nilimaliza chuo mwaka 2015 ila nikaajiriwa 2021 kipindi namaliza chuo nilipitia wakati mgumu sana wa ukosefu wa ajira nikaamua kwenda mpanda kwenda kukata mkaa nilipopata hela nikakodi shamba nikalima mahindi Mungu akasaidia nikapata gunia kumi nikauza yote kwa 480000 hiyo ni mwaka 2016

Baada ya kuuza na mkaa niliyokuwa nimechoma nilipata kama laki sita jumla da nikaamua kuhama kuja mwanza nikapanga maeneo ya kirumba mlimani nikaanza biashara ya kufata dagaa kisiwani nakuja kuuza mwaroni kirumba bahati mbaya madalali wakanipiga hela nikawa nimefuria huku nyuma mpenzi wangu akawa anahitaji aje tuanze maisha .

Nilimsihi anivumilie lakini akalazimisha kuja akapewa mchele ,unga, na vyombo akajanavyo hatimae nikawa nimeoa . Baada ya kuoa ndio nilikuwa nimejiongezea matatizo nilipitia wakati mgumu sana wa kiuchumi nilikonda hadi nikawa nawakimbia watu niliosoma nao nikiwaona mwanza.

Nikaanza kuwa natafuta vibarua vya ujenzi pia nikawa nafanya kazi za bustani kupanda ukoka na majani kwenye nyumba za watu hiyo kazi nilipewa na jamaa yangu anaitwa zabroni yupo hapo mwanza misheni karibu na kanisa la makongolo.

Muda nafanyanae kazi alikuwa hajui kama nimesoma nilijaribu kuficha mambo yangu.jamaa alikuwa anachukua tenda sisi tuna kuwa kama vibarua tumefanyq nae kazi maeneo mengi mfano isamilo,maina bendera tatu, bugarika pasiansi na sehemu zingine.

Lakini maisha yakawa yanazidi kuwa magumu sana.mke wangu akanishauri tuhamie dar maana yeye aliwahi kuishi dar sasa kimbembe kikawa nauli ikabidi tushauriane maamuzi yakawa aombe hela kwa mama yake.

Mama mkwe alikuwa ananipenda sana maana nilionesha mapenzibya dhati kwa mtoto wake na pia alikuwa anampenda mwanae ikabidi atutumie laki mbili nikatoa safari ya dar ikaanza

Tulisafiri kwa treni muda huo tuna godoro tu na vyombo tulivyofika dar akaniambia tukatafute chumba manzese siku hiyo hatukupata hiyo ilikuwa 2017 octoba

Tukalala gesti maeneo ya kigogo kesho yake akashauri twende kongowe njia ya kwenda vikindu tukaenda tukampata dalali tukapta chumba cha giza shilingi 15000 kwa mwezi tukaanza maisha hapo muda huo vyombo tunavyo kimbembe kikawa godoro kumbe behewa la mizigo lilibaki Tabora.

Ikabidi tulale chini bila godoro kwa muda wa wiki mbili ndio godoro likawa limefika tukalifata paceli .

Sasa ninanza maisha ya dar je nitafanya kazi gani .

Nikawa nazurura nakutana na waruguru wanauza ndizi mbichi ,njegere, na mbaazi nikawauliza wakanieleza wanapozitoa

Nikaenda kushaulianq na mke wangu akasema anapajua mabibo ataenda kuangalia ndizi

Kesho yake mke wangu nikamsindikiza stendi kongowe mwisho saa kumi usiku tukakubaliana tukutanie mbagala rangi tatu nakumbuka alienda na 15000 kama mtaji akaenda kununuq mikungu miwili ya ndizi bukoba tukaja tukagawana nusu kwa nusu.

Tukagawana mitaa ya kuuza maeneo yq kurasini mji mpya hapo mitaa siijui siku yakwanza nakumbuka tulipata faida ya shilingi 10000 ukiondoa mtaji

Tuliendelea kuwa tunauza nae ikabidi aniambie niwe naendq mimi sokoni kuchukuwa mzigo nikawa naenda mimi tunagawania mbagara tunauza kwa kichwa kila mtu mtaa wake .

Kumbe tulipotoka mwanza alikuwa mjamzito ikabidi tumbo lilivyofika miezi mitano akanza kuumwa ikabidi hospitali washauri apunguze kazi nzito ikabidi nimpumzishe nikaanza kukomaa mwenyewe hatimae nikawa na jina kwenye mabaa mengi nikawa nasambaza ndizi mzuzu na mshale.

Muda wa kujifungu ulipofika 2018 nikamsafirisha mkoani kwetu akaenda kujifungua mimi nikabaki nakomaa nilipata hela kweli mke wangu akajifungua kwa oparesheni mtoto wa kiume nilifurahi sana toto tunafanana nalo sana

Kule alikaa miezi miwili akarudi dar muda huo ninavihela tukashauriana tuhamie mbagara kibonde maji tukapanga nyumba ya umeme nikanunua tv ya chogo na sabufa sipiano alivyo baadae mke wangu akanishauri baskeli.

Ngoja niwakumbushe kitu kipindi tupo kongowe tuliweza kununua kitanda na godoro mpaka anaenda kujifungua tulikuwa tumesha nunuq hivyo vitu.

Tuendelee nikaenda kununua baskeli maeneo ya china plaza .

Nikaqnza kuuza ndizi kwa baskeli nikakipumzisha kichwa. Nikauza sana tu hapo kibonde maji kulitokea wizi ikabidi tuhamie kurasini mji mpya

20218 Serikali ikatangaza ajira nikaomba nikakosa niliumia sana ila mke wangu akanifariji sana nikazoea

Mungu saidia 2020 mwishoni nikapata ajira nikaanza kazi 2021
Pia nilikuwaga naomba kazi private lakini sikuwahi kupata

Kesho tutaendelea na kiini cha stori yangu. Ila niwakumbushe kuwa huyu mke wangu tulianza nae mahusiani 2008 mimi nilikuwa kidato cha tatu yeye cha kwanza ndio huyu tupo nae mpaka leo
Safisa
 
Back
Top Bottom