Wadau kwa mwenye msaada, Mchwa wananisumbua

proxy

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
1,477
1,346
1bf746321f132f93a5186074779df2d3.jpg
74c9241cbe6b20316cd7584f7301ca6d.jpg

Nimejenga nyumba kabla sijamalizia finishing Mchwa wameingia na wananisumbua sana ,bado sijasakafia chini lakini mcha ashaaza tokeza kila kona na kilamahari pa nyumba yangu,hapo juu nimeweka picha ya kile kilichotokea,mwenye uelewa na hii kitu naomba mchango wenu maana kila kitu kimesimama na sielewi nifanyeje.
5b3724e9125eb73bee788ebc92e42e46.jpg
 
P

pole sana mkuu, weka madirisha na fremu za chuma za milango. Itakusaidia sana.
Nimeshaweka ila hofu yangu ni kwenye kenchi na namna walivyoaza kusambaa kwa haraka kwa kweli inanipa hofu kubwa mno.
 
Wasi wasi wangu umejenga juu ya kichuguu
Kweli kabisa atakuwa amejenga juu ya kichuguu. Mchwa watasababisha nyufa kwenye kuta za nyumba na sakafu hata kama hawatatokeza juu. Athari yake huwa inakuwa chini kwa chini baadhi ya sehemu za msingi wa nyumba zitakuwa zinadidimia.
 
Mkuu naweza kufanya hivyo ila nakaribu kutafuta solution ya kudumu zaidi.
Pole sana mkuu! Solution ya kudumu itakua ngumu saana... Wewe ndo umewafuata kwenye eneo lao.
Jitahidi utumie frame za chumba au mbao utakazotumia wapake dawa ya kuzuia mchwa. Sifahamu jina linaitwaje ila kuna dawa fundi aliwai nipakia milangoni na dirishani kuzuia mchwa.

Mwenye solution ya kudumu zaidi msaidie mkuu hapa!
 
1bf746321f132f93a5186074779df2d3.jpg
74c9241cbe6b20316cd7584f7301ca6d.jpg

Nimejenga nyumba kabla sijamalizia finishing Mchwa wameingia na wananisumbua sana ,bado sijasakafia chini lakini mcha ashaaza tokeza kila kona na kilamahari pa nyumba yangu,hapo juu nimeweka picha ya kile kilichotokea,mwenye uelewa na hii kitu naomba mchango wenu maana kila kitu kimesimama na sielewi nifanyeje.
5b3724e9125eb73bee788ebc92e42e46.jpg
Sijajua uko mkoa gani ningekuelekeza dula la dawa, ila kuna dawa ya mchwa ambayo huuzwa maduka ya Pembejeo za kilimo na mifugo. Mfano TFA.

Hii dawa inaweza kukaa kwa miaka 7 na inazuia mchwa. Unanyunyizia kuzinguka ukuta na pia kabla hujaweka sakafu unanyuza kote hapo chini. Inaondoa kabisa mchwa.
 
Nakushauri kua ni vizuri zaidi kwanza ukachunguza hao Mchwa wanakotokea ni sehemu gani?

Kama ulichimba msingi imara na ukamwaga zege,si rahisi Mchwa kutoka chini ya ardhi?
Huenda hayo maeneo kuna vichuguu vimekuzunguka,

Kabla ya kutatua tatizo jaribu kuchunguza nini chanzo cha tatizo lenyewe?
 
Nenda duka la dawa za kilimo ununue dawa inaitwa DUDUALL. Imetengenezwa kwa ajili ya matunda na mbogamboga lakini kwa wadudu wote inaua vibaya sana. Ukiinyunyiza kwenye mbao au ukachimbia ardhini kuzunguka ukuta na njia zote za mchwa hutawaona kwa miaka kadhaa. Mchwa anakufa kwa kugusa tu udongo wenye hiyo dawa. Mimi nimeitumia na habari ya mchwa nimesahau. Cha msingi uzingatie concentration yake katika kuchanganya na maji. Tumia mml 5 kwa lita moja. Dawa hii unaweza kuitumia pia kuua utitiri na viroboto kwenye mabanda ya kuku na mifungo ila kwa tahadhari mifugo wasile vitu vilivyoguswa na hiyo dawa
 
nina kampuni ya usafi & fumigation niite nije nikufanyie fumigation wakirud hao uje hapa hapa jf kuja kutoa ripot
 
Sijajua uko mkoa gani ningekuelekeza dula la dawa, ila kuna dawa ya mchwa ambayo huuzwa maduka ya Pembejeo za kilimo na mifugo. Mfano TFA.

Hii dawa inaweza kukaa kwa miaka 7 na inazuia mchwa. Unanyunyizia kuzinguka ukuta na pia kabla hujaweka sakafu unanyuza kote hapo chini. Inaondoa kabisa mchwa.
Mimi nipo Songea
 
Iliwahi tokea nyumba fulani hivi wakaitwa jamaa wakachimba kile kichuguu walipomtoa malkia tu kichuguu kikafa mpaka leo hakuna hata kubunguliwa kibao chochote.
Hata mimi nilifikilia hivyo ila kujua aliko malkia ndo ishu ilipo
 
Back
Top Bottom