Wadau kwa mwenye msaada, Mchwa wananisumbua

Wadau kwa mwenye msaada, Mchwa wananisumbua

Nakushauri kua ni vizuri zaidi kwanza ukachunguza hao Mchwa wanakotokea ni sehemu gani?

Kama ulichimba msingi imara na ukamwaga zege,si rahisi Mchwa kutoka chini ya ardhi?
Huenda hayo maeneo kuna vichuguu vimekuzunguka,


Kabla ya kutatua tatizo jaribu kuchunguza nini chanzo cha tatizo lenyewe?
Mkuu maeneo nilipojenga hapakuwa dalili zozote zile za uwepo wa Mchwa na hamna kichuguu chochote kilichonizunguka ila nimeshangaa mara baada ya kumaliza kupiga plasta ,Mchwa wameaza kujitokeza kwenye baadhi ya vyumba,ila ninachoshukuru hawajaaza panda ukutani wapo chini tu na bado sijasakafia.
 
Mkuu mchwa ni wa ajabu home juzi nilienda kusimamia zoezi LA kumtoa Malkia pamoja na mfalme wao kwenye vyumba viwili baada ya hapo zoezi kubwa linakuwa limekwisha then ilibidi MTU apande juu ya Dari kusafisha maana walikuwa walishaanza kupanda juu ya Dari ,kuna dawa INA kuwa pamoja na carbonate hivi sijaikalili jina maana tulitumiwa tu tuliinyunyuzia KWENYE vyumba hivyo then floor ilipigwa upya ila ni wadudu wabaya Sana
 
Ikiwa inapajua kichuguu kilipo sema nikuelekeze.
Kichuguu sijaona kilipo labda mbali sana na eneo na Mimi nilipo ila sema kuna sehemu ndani ya nyumba ndo wanaazisha kichuguu.
 
Pole sana mkuu! Solution ya kudumu itakua ngumu saana... Wewe ndo umewafuata kwenye eneo lao.
Jitahidi utumie frame za chumba au mbao utakazotumia wapake dawa ya kuzuia mchwa. Sifahamu jina linaitwaje ila kuna dawa fundi aliwai nipakia milangoni na dirishani kuzuia mchwa.

Mwenye solution ya kudumu zaidi msaidie mkuu hapa!
Hiyo ndio ya kudumu nafikiri,ht mm nilinunua hiyo nikapata kwenye frame za milango na nilichanganyia udongo kwenye msingi wakati najenga.
 
Dawa zooote ni short time solution may be miaka 5 tu lkn nyumba unahitaji idumu kwa miongo mingi. Ushauri wangu: chimba mpk utoe makao yao. Bila hivyo utakuwa unacheza makidamakida na utapata hasara kubwa. All the Best
 
Kichuguu sijaona kilipo labda mbali sana na eneo na Mimi nilipo ila sema kuna sehemu ndani ya nyumba ndo wanaazisha kichuguu.
Kanunue ile dawa uweke, kuchimba itakusumbua sana kuwapata. maana huwa unapowachimba huwa kuna vialama vya kuangalia hadi uweze kumfikia malikia wao. Mimi nilishuhudia wachimbaji wakichimba hao mchwa ndo nikajifunza kutokea hapo. Ila kwangu mimi nimepiga hizo dawa na siwaoni.
 
Mkuu tumia dawa iitwayo karate Mimi mwenyewe walinisumbua sana, hivyo waweza mwaga wanapoishi, ila mimi nilichanganya cement na hiyo dawa mpaka leo two year hawapo
 
Nashukuru kwa michango yenu wadau ,nimempata malkia baada ya kuhangaika sana.

Sent from my TECNO M6 using JamiiForums mobile app
151714cd67ec4c4d17a3803e6231715a.jpg
250171fb6ac9117c8ddaada8f90c14b4.jpg
287dc5a925db66dd7c1282e6de0e6560.jpg
087f3168db94e2a4223dce45f9f7146b.jpg
fcd2b5b8b483c133584a6d313185a4a7.jpg
986f5625781a490fb5a0129358a5801d.jpg
 
Huyo ndio malkia mwenyewe tuliefanikisha kumtoa Leo ,baad ya kuhangaika sana.
 
Tafuta gamalin e40 changanya kama ilivyoainishwa, funika na karatasi la g1000. Kisha waga zege. Wakikusumbua tena ni pm nikurudishie pesa yako.
Hii ni kwa nyumba ambazo hazijawekwa zege ya jamvi.
 
kuna dawa ya mbao ina rangi ya kijani, siijui jina but wataalamu wauzaji watakua wanaifahamu
 
Nenda duka la dawa za kilimo ununue dawa inaitwa DUDUALL. Imetengenezwa kwa ajili ya matunda na mbogamboga lakini kwa wadudu wote inaua vibaya sana. Ukiinyunyiza kwenye mbao au ukachimbia ardhini kuzunguka ukuta na njia zote za mchwa hutawaona kwa miaka kadhaa. Mchwa anakufa kwa kugusa tu udongo wenye hiyo dawa. Mimi nimeitumia na habari ya mchwa nimesahau. Cha msingi uzingatie concentration yake katika kuchanganya na maji. Tumia mml 5 kwa lita moja. Dawa hii unaweza kuitumia pia kuua utitiri na viroboto kwenye mabanda ya kuku na mifungo ila kwa tahadhari mifugo wasile vitu vilivyoguswa na hiyo dawa


Nashukur kwa msaada, nitapitia maduka hayo kuulizia, hakika wanaudh hawa wadudu
 
Back
Top Bottom