Wadau badilisheni mbinu ya kudai Katiba Mpya

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Habari zenu,

Nimesikiliza na kufuatilia mijadala katika club house ya CHADEMA,mijadala ya humu JF na Twitter space hakika inaonesha wadau hasa wapinzani wamegotea katika mbinu za kudai katiba mpya na wanaona hakuna mbadala mwingine wa kufanya siasa na kuendesha maisha yao mpaka katiba mpya.

Mfano CHADEMA wanaamini au kuaminishwa kuwa bila Katiba mpya hakuna lolote linaweza kufanyika na kuwa ili ''wachukue dola'' mpaka katiba mpya iwepo maana itazaa Tume huru ya uchaguzi.

Wakati CHADEMA wakitumia falsafa hiyo wenzao CCM wanaamini kuwa ili waendelee kutawala milele ni lazima katiba mpya isiwepo au kwa maana nyingine kuruhusu katiba mpya ni sawa na kuazimisha silaha zake kwa mpinzani wako.

Sasa ukitazama falsafa mbili hapo juu nafikiri unaona hakika CCM watashinda hii battle wakati mwathirika wa mwisho ni mwananchi ambao ni wachache wanaolewa hili.

Sasa ili kumaliza hili kwanza ni kutambua kuwa 'mbinu' zinazotumiwa na wadau ni butu, haziwezi kuwafanya CCM waruhusu katiba mpya au waamue kuachia madaraka kupitia Tume huru ya uchaguzi.

Ili kutatua tatizo kwanza ni kujua chanzo cha tatizo.

Tuanze na hilo kwanza
 
Mawazo yako ni mazuri lqkini kuna kitu hujakifanyia utafiti wa kina. Kusema CHADEMA wameshikilia kwenye katiba mpya oekee unakuwa huwatendei haki, jaribu kuchungulia nje ya dirisha. Kinachofanywa na CHADEMA kwa sasa ni kikubwa sana. Kinachojengwa nchini kwa sasa kitazaa Matunda muda si mrefu na utashangaa.
 
Back
Top Bottom