Wadaiwa mikopo tuishitaki HESLB

Wadaiwa mikopo tuishitaki HESLB

Yani HESLB wanatukata 15%. Huu ni uhuni wa hali ya juu. Ila kuhusu jpm kutusaidia, Sidhani kwa sababu nasikia yeye ndio aliwaambia wapandishe kutoka 7% mpaka hii ya SAA hizi 15%.
Atalipa tu...

He must PAY...

Mungu Yupo.
 
Hii inshu ni serious sana..nina mfano halisi wa jamaa yangu yeye ni mwalimu Kwa sasa anachukua mshahara laki na kidogo ana madeni lukuki..ana familia kubwa inamtegemea.

Bodi ya mikopo wanachoangalia ni kodi ya serikali tu kinachobaki wanalamba..hawaangalii unabaki na nini..
Duh...
Mkuu huyo Jamaa anaishije!!?
 
Na katika hili mswada ulipoletwa bungeni sikuwaona wabunge wa upinzani kutoka nje kuonesha kutokubaliana na uonevu wa namna hii: upinzani tz+ccm= njaa na ubinafsi
Bunge lote lilitusaliti kwa hili.... Siji kusahau..

Kitu kilipitishwa harakaharaka...
 
Moja ya ground za kuwashtaki ni kiwango kipya cha makato walichokileta.

Maana mkataba wa kukopa wengi wamesaini kiwango cha makato kikiwa chini ya hiki kinachokatwa hivi sasa.

Hivyo basi Heslb wamevunja mkataba kwa kutaka makato makubwa kinyume na mkataba halali kabisa walioingia na wakopaji.

Ingewezekana kabisa mtu asingekopa kama angejua makato haya waliyoleta
 
Kuna tabia mbaya Watanzania tunafikiri mkopo ni Ruzuku! Mkopo lazima ulipwe na wengi ambao wakimaliza vyuo wanagangamala kutolipa walikuwa wanaandamana ili wapate MKOPO na mkopo lazima urejeshwe. Tusisahau huwezi kutajirika bila kukopa lakini mkopo lazima urejeshwe
jifunze kuelewa hoja wewe ......wanachokisema watu kwa nini sheria inarudishwa nyuma kinyume na utaratibu, kwa nini baadhi ya mashariti waliyaficha na wanayaibua sasa hivi?
 
Kuna vijana fulani wanasheria walijipanga kwenda mahakamani kufungua kesi ya kudai kurejesha 8% ya makato..

Sijui ilikuaje. Walipotea kimya kimya
 
Kama mmepandishiwa % za makato kesi ikaenda mahakamani sijui imepotelea wapi
 
Mnawakumbuka hawa....nafkiri walifinywa juu kwa juu...
 
Bunge lote lilitusaliti kwa hili.... Siji kusahau..

Kitu kilipitishwa harakaharaka...
Mimi ndo maana siwaamini wabunge wanchi hii awe chadema,ccm au cuf wote wale wanapigania matumbo yao si ya wananchi!?!!!!
 
Kuna vijana fulani wanasheria walijipanga kwenda mahakamani kufungua kesi ya kudai kurejesha 8% ya makato..

Sijui ilikuaje. Walipotea kimya kimya
Katika lile kundi alikuwemo Shukuru Mlafu dogo yule alikuwa anatafuta kiki tu baada ya maisha ya dar kumuigilia kinyume na maumbile
 
Hiyo paragraph ya mwisho No3 Magufuli hakupi msaada wowote...never ever,yeye ndiye aliyewakurupusha hao jamaa waongeze riba kwa kiwango hiko ili kufidia mapengo ya makusanyo.unapomuona kwenye hotuba zake akijigamba hadhrani kwamba hatakopa popote hali biashara mijini zikizidi kuwa mbaya huku nyengine zikifungwa jua tunaokamuliwa ni sisi wananchi ili kujazia hiko kilichopungua.na kila mmoja ana aina yake ya ulipaji!
 
Umemaliza Mkuu...

Tutamenyeka kwelikweli.
 
Tunapigwa na hawa wezi tena hii 15% kutoka 8% ndo ushenzi mkubwa
 
Dawa ni kutokulipa tu hakuna namna. Binafsi ntakua wa mwisho kulipa, just in case.
Ila sitalipa iyo hela kamwe.... kwanza walikua wasumbufu kutuwekea ela zetu
 
Back
Top Bottom