Wadaiwa mikopo tuishitaki HESLB

Wadaiwa mikopo tuishitaki HESLB

Hujui mada, una ropoka tu.
Mkuu hajielewi huyo temana nae Ila subiri yake yamshike atakapo kuja spidi hapa,embu watz tuwe na utu basi.Uzi haupo kiharakati bali upo kimaslai ya kila mtu hata kama si wewe moja kwa moja basi una mdogo au ndugu aliekumbwa na hili janga
 
FACT tupu.

Wadaiwa wanapaswa kulipa kile walichokopa tu na si vinginevyo.

Uvivu/uzembe wa bodi kushindwa kuwapata wadaiwa wote isiwe mzigo kwa wengine.

Tabia ya kuwadai wasiodaiwa na kuwakata zaidi wanaolipa itakuja kuicost bodi watu watakapozinduka kutoka usingizini.

Kuna mambo hayajakaa sawa kabisa kwenye hiyo bodi...wajitafakari na kutafuta mbinu mbadala.

Zama zimebadilika...this is 2018 bado wana mbinu zile zile za kizamani.
 
Jameni wadaiwa wote wa mkopo wa Higher Education Students Loan Board (HESLB), tulio kwisha anza kulipa na ambao bado hawa jaanza kulipa tufanye utaratibu tuifungulie kesi HESLB.

Hoja zangu ni hizi:

1. Form za miaka ya 2000 hadi 2011 pesa zile hazi kuanishwa kuwa zilipaswa kurejeshwa. Hazikuandikwa kuwa ni mikopo. Pia sehemu ya fedha ilijulikana kama ruzuku... Mf. Accommodation.

2. Retention Fee na Interest Rate. Form za miaka tajwa hapo juu hazikuwa na kipengele cha fedha hizi kulipwa kwa riba wala kufidia thamani ya fedha. Binafsi na heshimu Form zile kama mkataba wangu na hii Loan Board. Kwa nn wa Introduce vipengele nje ya mkataba? Wao hawaoni huku ni kuvunja mkataba? Masharti ya riba hayakuwepo ktk Form zetu, huenda hizi mpya!! Ambazo sasa ni Online.

3. Riba na Retention Fee kwa mikopo ya HESLB imesababisha mikopo hii kuwa ya ghali zaidi ya mikopo ya Benki. Hivyo uwazi ulikosekana ili mkopaji ajue kama atamudu kulipa mkopo huo + riba na Retention fee. Ikumbukwe Benki zote huweka wazi kiasi unachokopa na kile utakacho rejesha (Principle + Interest). Hivyo mtu kuamua kukopa au kutokopa. Iweje huu mkopo wa Loan Board tozo za malipo ni siri na huja baadae?

Binafsi ningeoneshwa awali kiasi ambacho ningepaswa kurejesha nisinge uchukua mkopo huu!!

4. KIWANGO CHA MKOPO. Mkopo ni hiari ya mkopaji kwa kile kiasi akitakacho mkopaji. Iweje Loan Board wao ndio wanipangie kiwango cha kukopa na kunipa? Je wao wanajua uwezo wangu? Mara Priority Programme!! Agriculture, Medicine, Education, nk.

Kiwango/kiasi cha mtu kukopa ni hiari ya mkopaji Kutokana na uwezo wa kurejesha. Hakuna madaraja wala nn?

5. UKOKOTOAJI. Ukokoaji wa hesabu ni wa ajabu sn. Kila mtu ana hesabu zake!! Kila mtu na invoice yake! Hii inakuwa Mwanya (Loophole) ya watu kutapeliwa na kuibiwa.

Juzi kuna gazeti limeripoti Mwalimu mmoja kukatawa fedha zake kimakosa. Watu wanskatwa hata ambao hawajakopa!! Au kukatwa kiwango kikubwa sn. Waulizeni Walimu wa Secondary wanao katwa Loan Board, wana msisha ya ajabu sn. Ni si kwa muda mfupi. Its 5 to 15 yrs. Watu walipe kile tu walicho kopeshwa. Kupunguza ujanja ujanja.


6. Hizi hela siyo Mkopo. Ni jina la wahuni tu kuita fedha hizi mkopo. Mkopo ana kopeshwa mtu mwenye uwezo wa kuurejesha baadae, tena iwapo tu atakidhi vigezo na masharti kama dhamana ya nyumba, majengo, kukagua biashara yako, na hata kuchukua hati za mali husika. Mikopo ni Biashara kama biashara zingine mf. kama kuuza Mbao. Hivyo inapaswa ijiendeshe kibiashara. Ikopwe na irejeshwe.

Tofauti na mabenki, mkopo wa Loan Board, vigezo vya kuupata (kukopeswa) ni kuwa maskini, kusomea shule za kata au shule za serikali, kuwa yatima, kutoka ktk mazingira magumu, nk.

Ukitazama kwa makini vigezo hivi utagundua kabisa huu siyo mkopo bali ni social incentive ktl Elimu.
Hapa duniani, nchi yoyote ile maskini hakopesheki. Na hakopeshwi bali husaidiwa. Binafsi huwa na angalia mtu wa kumkopesha, asiye nacho huwa namsaidia tu kama ipo ndani ya ueezo wangu. Kwani atanisumbua bure na huenda asinilipe. Ni bora nimpe bure.

Huwezi ukamkopesha Yatima milioni 20 afu akulipe na riba ya milioni 7 Jumla milioni 27!!! Yy anategemewa, hajaoa/hajaolewa, hajajenga nyumba, haja nununua usafiri wake, hajasaidia wategemezi wake au ndg zake!! Ni ngumu kabisa mkopo huu kulipwa na mtu huyu!!!

Lasivyo tukubaliane kuwa lengo la mkopo huu siyo kusaidia maskini bali ni kuongeza pengo la kiuchumi (Income Inequality) kati ya walionacho na wasio nacho. Kwani wadaiwa watatumia miaka 5 hadi 10 kulipa mkopo wa HESLB huku watoto wa Matajiri wakizidi kusonga mbele ktk kujiendeleza kimaendeleo.


MAOMBI YANGU:

1. Mwenye kopi ya zile formu, wadau naomba mu zi attach hapa full. In word file au Pdf file. Tutazitumia kama ushahidi mahakamani Either Individually or as a group. Binafsi sina copy. Mwenye naza a scan au apige picha atutumie.

2. Loan Board itumie uzi huu kujisahihisha. Kuondoa Retention fee na Interest Rate. Hizi fee ndizo zinafanya mkopo huu kutolipika. Hakuna kijana asiye pende kurejesha fedha hizi. Ila hizo riba na retention fee for each day the money remains outstanding...ni mzigo kwa vijana. Huwezi fanya biashara ya faida kwa maskini. Maskini siyo mtaji wenu!!

3. JPM mtoto wa mkulima na mtetezi wa wanyonge. Washugulikie hawa LOAN BOARD. Wameiba hela. Kufidia hela walizo kwapua. Hutoza maskini riba za ajabu ajabu. Mhe: Rais futa aina zote za Riba. Vijana warejeshe walicho kopa tu. Ikumbukwe serikali ina wajibu wa kutoa incentive ktk Elimu (Riba na Retention).


Vijana mliosoma sheria. Sheria zenu mnazitumia wapi ndg zangu?

Naomba tuwashughulikie hawa HESLB ...
lipa wenzako wasome sasa kama waliokupa pesa HESLB kirefu chake unataka ujifanye hujui unakimbilia kwenye form na hizo form zilitolewa na idara ipi (naipenda nchi yangu lipa wenzako wasome )
 
Mlipe tu aseh Si mlipata mkopo na mliomba Mkopo au mliomba ruzuku ,No matter what Lipeni mkopo na Mdogo wapate ,isije ikàfika mwezi wa kumi madogo wa nahangaika kupata mkopo kumbe nyie hamjalipa
 
wamekwambia hawajakataa kulipa deni..tatizo ni kubadilishiwa makubaliano yao ya ulipaji...jamaa unakichwa kizito sana
Hilo jamaa ni jinga kupindukia,eti serikali haina wajibu wa kusomesha!. Unajua unaweza ukawa unamuelimisha chizi aiseee kwa uwezo huu wa kufikiri huyu si mfu kabisa
 
Mlipe tu aseh Si mlipata mkopo na mliomba Mkopo au mliomba ruzuku ,No matter what Lipeni mkopo na Mdogo wapate ,isije ikàfika mwezi wa kumi madogo wa nahangaika kupata mkopo kumbe nyie hamjalipa
Kwani wamekataa umesoma vzr hoja?walipe tu hata kama wananyanyaswa?tuwe na huruma banah na wenzetu tusishabikie maumivu yao
 

Attachments

  • upload_2018-1-5_12-34-12.png
    upload_2018-1-5_12-34-12.png
    21.5 KB · Views: 42
Bodi ya mikopo....jana wamerudi tena kwa kasi ya mwanga
 
Na kma aliyehitimu bado yupo kijijini anamsaidia baba yake kulima ataripa VP? Mtamkata % ya mazao aliyovuna? AJIRA hakuna,mshahara autoe WAP?
 
wanasheria petro mselewa na wengine tupeni hoja za kisheria juu ya hili saga la loarn board
 
Mm nilienda bodi nikakuta deni langu mil 30, ninaachana nao silipi.
Sijaajiliwa serikalini na situmii vyeti na majina nabadilisha, km cheti cha kuzaliwa etc
imefikaje hiyo 30 mkuu?
 
Lipa kama unadaiwa acha visingizio
Mkuu nmeshasema nadaiwa tena nlilipiwa 100% lkn silipi hata mia mpaka warud kwenye makubaliano ya mwanzo vinginevyo imekula kwao. Kama unaumia moyo kufa lkn nakuhakikishia siwalipi mpaka mkataba wa mwanzo uheshimiwe
 
Ni utahira wa kiwango cha mwenye hirizi kiunoni kama utalipa hizo hela wakati ulipigwa bomu za machozi ili ziingie kwenye akaunti yako.......silipi ng'oo!
 
WALISEMA UTALIPA UKIPATA KAZI TENA BILA RIBA, NDICHO NACHOFAHAMU MIMI,HALAFU HAWAKUSEMA UTALIPA KWA KUKATWA MSHAHARA NA WALA HAAWAKUANDIKA KIWANGO CHA KUKATA.

MWISHO,WAO WALISOMA BURE WASITUCHOSHE,TENA WAO HADI MISOSI WALIKUWA WANAPEWA.

HIVI SI WALIMGOMEA MWALIMU NYERERE PALE UDSM MIAKA HIYO HAWA ETI KWA SABABU WALIPEWA MKATE AMBAO HAUJAWEKWA SIAGI
 
imefikaje hiyo 30 mkuu?
baada ya kuhitimu huwa wanatoa grace period nadhani ya mwaka, baada ya hapo sasa usipolipa ndani ya mwaka wanakupiga fine asilimia fulani ya kile unachodaiwa. so deni linazidi tu.
 
baada ya kuhitimu huwa wanatoa grace period nadhani ya mwaka, baada ya hapo sasa usipolipa ndani ya mwaka wanakupiga fine asilimia fulani ya kile unachodaiwa. so deni linazidi tu.
mwisho wa siku watajilipa wenyewe huo ni upuuzi wa kuzalisha mkopo na hakuna makubaliano kama haya kwenye form zao mkuu
 
Back
Top Bottom