Wadada wa Uchumi Supermarket - Quality Center

Wadada wa Uchumi Supermarket - Quality Center

Daa, ili tatizo ni ugonjwa ambao unahitaji natural remedies, maana kwenye maduka soko yote makubwa hasa ukikuta wadada wa kiswahili wana tabia hii, binafsi pale tegeta TSN supermarket huwa nawapa ukweli kwa uhuni wa hizi pesa wanazoziona ni ndogo.

Kila duka soko huwa wanaletewa sarafu kwa ajili ya chenji toka bank kuu kila siku, but wao washaona hii ni sehemu ya kujiongezea kipato.
Nasema MKOME..!!
 
Naandika haya kwa kuwa mimi ni mhanga wa hili suala.Hawa wadada huwa wanakukata 200 au 300 hawasemi ukihesabu salio lako unakuta limepungua ukiwauliza wanakuambia hawana change,nimefanyiwa zaidi ya mara mbili mara ya tatu nikatoa mia tatu ili nipewe 500 mdada akaniambia nisubiri,mpaka mteja mwingine aje ndipo afungue vidude vyao vile , nikae kula zangu nilivyomaliza nikaenda kukumbusha salio langu kumbe mdada kaondoka ,wale walioko zamu wakamjua mpokea pesa alietoka punde msela Mmoja akamfuata aliko akiwa na receipt yangu akarudi na 500 yangu(huku ni kule kwenye menu) wale wadada wajanjawajanja sana wengi wao.

TUWE MAKINI
ulitaka mema ya .nchi wajekula jf??hiyo.ndiomadhabahu yao..ndiomaana sadaka uruhusiwi kujua ikowapi inajua madhabahu imetumikaje
 
Hata Uchumi ya segerea ndo tabia zao
 
Wanapunguza matatizo ya kuambiwa na kila
mteja et "keep shenzi" sasa ya nini utukanwe kutwa nzima,
wanabana wenyewe bila kuambiawa:A S 39:
 
Kuna mtu aliniuliza mbona unanidai hadi mia
nikamjibu mbona unataka kunidhulumu hadi shilingi mia?

mkuu@MO11 watu wanadharau pesa ndogo namna hii hatuwezi kupiga hatua kama nchi na ndio maana hali halisi kwa viongozi wetu wanadharau mambo madogo magari ya bei mbaya wanayoyatumia kuliko walio yatengeneza.
 
Jamani bora hao private sector sisi tunavuka kigongo ferry mwanza nauli ya kivuko mia nne ukitoa mia tano hurudishiwi change tena ukidai unafokewa haswa.last week nimekuta wamebandika tangazo abiria waje na change kamili.Nilimuliza yule dada hilo tangazo linatokana na sheria ipi nchi hii akasema hayo ni maelekezo toka ofcn.Eti mh Magufuli ni kweli abiria tunavuka busisi tukitoa pesa ZAIDI YA MIA NNE HATUHUSIWI KURUSHIWA CHANGE?
 
Wasamehe bure! Mishahara isiyokidhi mahitaji imewafanya Watanzania wengi wawe wapiga dili kwenye vituo vyao vya kazi!
 
Jamani bora hao private sector sisi tunavuka kigongo ferry mwanza nauli ya kivuko mia nne ukitoa mia tano hurudishiwi change tena ukidai unafokewa haswa.last week nimekuta wamebandika tangazo abiria waje na change kamili.Nilimuliza yule dada hilo tangazo linatokana na sheria ipi nchi hii akasema hayo ni maelekezo toka ofcn.Eti mh Magufuli ni kweli abiria tunavuka busisi tukitoa pesa ZAIDI YA MIA NNE HATUHUSIWI KURUSHIWA CHANGE?

Abiria wa hapo mtakuwa wapole sana....
 
Jamani eeeeh, hivi mnajua mishahara yao au mnawalaumu tu. Wanaunga unga nauli mjini hapa, nani kakwambia watu wanaishi kwa mishahara tu. Lazima watengeneze njia mbadala
 
Abiria wa hapo mtakuwa wapole sana....

Mwenzangu we si unajua watu wa kanda ya ziwa cjui niseme waoga yani mtu anaambiwa na anaacha change anapitiliza imagine magari ya kampala kigoma bukoba geita wanapata shilingi ngapi?kuna siku nilihangaika kutafuta no ya waziri aniambie ni sheria ipi bahati sikupata.
 
Kama mishahara midogo kwa nini wasuombe kistarabu dada sina change niachie hii mdogo wako nipate nauli.kuna mdada wa parking aliwah kuniomba ivo nijampa elfu tano.lakini me ukinijibu sina change hata kama 50siiachi.huo ni wizi kabisaa
 
...frankly speaking, juzi tu nilienda kununua yogurt ya asas ile ya 2100, nikatoa elfu tano, lakini nilirudishiwa 3000 kamili, na pia sibishi kuwa hawakati ila nafikiri inaweza kuwa mtu na mtu, na ni hapo hapo uchumi ya quality
 
Jina lenyewe "uchumi" na wao wapo kuchuma! :hatari:
 
Back
Top Bottom