Kama mishahara midogo kwa nini wasuombe kistarabu dada sina change niachie hii mdogo wako nipate nauli.kuna mdada wa parking aliwah kuniomba ivo nijampa elfu tano.lakini me ukinijibu sina change hata kama 50siiachi.huo ni wizi kabisaa
Jina lenyewe "uchumi" na wao wapo kuchuma! :hatari:
umetoa buku teni kitu kinauzwa 9999 unadai chenji
Naandika haya kwa kuwa mimi ni mhanga wa hili suala.Hawa wadada huwa wanakukata 200 au 300 hawasemi ukihesabu salio lako unakuta limepungua ukiwauliza wanakuambia hawana change,nimefanyiwa zaidi ya mara mbili mara ya tatu nikatoa mia tatu ili nipewe 500 mdada akaniambia nisubiri,mpaka mteja mwingine aje ndipo afungue vidude vyao vile , nikae kula zangu nilivyomaliza nikaenda kukumbusha salio langu kumbe mdada kaondoka ,wale walioko zamu wakamjua mpokea pesa alietoka punde msela Mmoja akamfuata aliko akiwa na receipt yangu akarudi na 500 yangu(huku ni kule kwenye menu) wale wadada wajanjawajanja sana wengi wao.
TUWE MAKINI
Wanatabia pia ya kukuzidishia idadi ya vitu..mfano umenunua chupa za beer 5 wao wanaingiza 6 ni hawafai wale
Sio kwenye chakula tu ni kote. Lakini hata m.city imetokea. Inachokera ni kwa nn wasikupe hata opt ya pipi ya 200. Wapuuzi sana. Kuna siku nlikomaa na mia yangu mpk wakanipa 200
mi siku hizi nakomaa. hata kama hana atatafuta mpaka apate...niliwahi kukataa kuchukua vitu wanirudishie hela yangu kama hawana 100!
Mpaka leo wananijua, nikienda, utasikia andaa change, mchaga kaja...!
Kuna bar moja kila nikienda hapo 200 hawana inabidi niwaachie
siku moja nimeapa pesa imepungua 50 ...wakakataa
toka siku hiyo hata ipungue 50 naisubiri hadi wanipe
Huu wizi ni maarufu sana Dar sasa....kila mtu anajifanya 200 hana bila aibu
Watanzania mjifunze kutoa tip, hao naona wanachukua tip kijanja.
Ingekuwa vizuri kama kwenye rising wangeandika percentage ya tip, kuliko kukata kijanja.
Mwenzangu we si unajua watu wa kanda ya ziwa cjui niseme waoga yani mtu anaambiwa na anaacha change anapitiliza imagine magari ya kampala kigoma bukoba geita wanapata shilingi ngapi?kuna siku nilihangaika kutafuta no ya waziri aniambie ni sheria ipi bahati sikupata.
Jaman wahusika wa uchumi ni kwa ajili gani hawachukui atua dhidi ya hii ishu, imekiwa ni kero kwa wateja
Teh Teh teh teh
Vp yamekukuta hata wewe?