Wadada tembeeni na kanga au kitenge cha dharura

Wadada tembeeni na kanga au kitenge cha dharura

Wanawake wana roho mbaya sana hasa katika kusaidiana wao kwa wao.
 
Ungechukua namba ili ajue namna ya kukurudishia sweta lako..

Ila wanaume wa dar mmezidi,yaani pamoja na joto lote la dar ila mnavaa masweta

Maofisini ni fuli kipupwe kama wako mufindi
 
Hii story yako imenikumbusha nikiwa shule ya msingi std 7 binti mmoja classmate yai lilipasuka, sketi ikalowa muda wa break akawa hataki kutoka pale masela wakaenda kumtoa kwa nguvu ghafla tunaona sketi haikosawa. Watu wakaanza kuconnect dot na somo la via vya uzazi mambo ya kubalehe.

Kwa kweli hakukuwa wa kumsaidia zaidi ya kumcheka. Nashukuru maisha yangu yote sijawahi kukutana na kisanga hicho tena mtaani.

Kina mama wa Dar huruma kwa wao zero saizi wako wachache sana wenye kujali wenzao. Hata mama mjamzito akiingia kumpisha siti wata kwambia kwa nini akuchukua Uber
 
Wanadai kutembea na khanga ni ushamba na uzwazwa....wakuja na Wa mikoani ndo wanabeba makhanga, wao Wa dar ni mwendo Wa kubeba handbag yenye pafyumu na lip shine tu.

Pole ni wadada Wa dar.
Wanaosema n ushamba Mungu awasaidie
 
Sasa hao waliomcheka wana mantiki gani "? Hiyo si ni hali ya kimaumbile tu " nani kawaida Mwanamke kufikwa na hiyo hali ..so chaajabu hapo nini !?

Mijitu mingine hovyo sana "...
 
Wangemsaidia vipi wakati wenyewe hawana kanga? Au ulitaka wavue walizovaa? Ushauri wa kutembea na kanga si mbaya
Hata kumpaishara tu amechafuka pia ni msaada tosha angejua mwenyew namna ya kujistiri
Wao wamemuangalia alafu wanacheka na kumpita kama sio roho mbaya ni nin
Walitaka adhalilike hakuna jingine
 
Wanawake ss ni waseng*** hatupendani hata sometimes i wish ningekuwa mwanaume aiseeee na ndio maana Mungu ametunyima baadhi ya vitu maana tungekuwa viumbe vikatili sana
mama yako liked ur post
 
Wanawake ss ni waseng*** hatupendani hata sometimes i wish ningekuwa mwanaume aiseeee na ndio maana Mungu ametunyima baadhi ya vitu maana tungekuwa viumbe vikatili sana
Hahahahaaa njo tubadirishane
 
Hongra, Mungu akuzidishie kwa kujali utu kuliko kitu.
 
Ungempa namba yako ili akifika hom alifue akurudishie, hakika asingekunyima
 
Kilicho tokea leo nimeshindwa kuwaelewa kabisa hawa wamama wameshidwa kabisa kumsaidia mwanamke mwenzao??

Leo nilikua nimepanda daladala nimekaa siti ya mwisho kabisa kulikua na wadada wa 2, mama mtu mzima mjoja na mm jumla wa 4' mbele yetu alikua amekaa mdada age kama 19-22,

Tulivyofika mwisho wa daladala kutokana sijui ni hizi bamnsi za barabaran huyo mdada alifikwa na menstruation period yeye mwenyewe bila kujua wakati tunajiandaa kushuka dha' wote tuliokaa siti ya nyuma yake tuliona ile hali, sasa baada ya kuona ile nikasubiri ili mm nishuke wa mwisho nikijua wale wamama watatu watamsaidia cha ajabu nilishangaa watu badala ya kumsaidia wanacheka chini chini wakati wanasuka kwenye daladala, aise nimeshangaa sana sikuamini hata...

Nikawaza chap chap ili kumfanya asije akaaibika nilikua nimebeba sweta langu mkononi nikalimpa ajifunge kumlindia heshima tu, Ameniangalia kwa aibu nilivyo mpa lile sweta ajifuge..

Aisee nimeshangaa leo kuona mwanawake wamemuacha mwanamke mwenzao bila msaada, lakini pia nyie wadada mnapotembea bebeni basi hata kanga au kitenge cha dharula sweta langu nilinunua elf 18 ameshachukua

Bila kapicha uzi haunogi
Mkuu weka Picha kabla na baada ya kupewa sweta
 
Back
Top Bottom