Wadada na nguo fupi!!!


Naomba kuuliza hapo unapodai vivazi "haviendani kabisa na utamaduni wetu wa kitanzania." Je, mavazi ya kitamaduni ya mtanzania ni yapi?
 
Mtuwache tupumue jamani.
Dar kuna joto kali.
Mwili wangu hauna ukurutu, mguu wangu mtamu.
Kwanini nisivae nguo fupi.

jamani eeeh msituchoshee. nyie wanaume wa miaka hii sijui mna nini mbona zamani wanawake walikuwa wanaficha papuchi tu kwa magome ya miti lakini wanaume walivumilia tu na hawakuwa na tatizo kabisa.

Sina ukurutu acha nipumue na min skirt yangu......ukiona unakereka bas taga yai kama la mbuni ndo ntaacha!!!


kama mnalipa , endeleeni kuvaa jamani ............... wengine tunapenda ajabu mkivaa hivyo.
 

Biashara ni matangazo
 
kama anamiguu mizuri ya kike , laini imewiva kwa mafuta , iliyobeba shepu nzuri ya kike.......... sina tatizo nao.

wananivutia sana...........

Kwahiyo umemaanisha ni haki kuyaonyesha?
 
Naomba kuuliza hapo unapodai vivazi "haviendani kabisa na utamaduni wetu wa kitanzania." Je, mavazi ya kitamaduni ya mtanzania ni yapi?

kama bado una bibi jaribu kuangalia nguo alizokuwa akizivaa miaka hiyo,.. Kama ni kabibi ka mjini basi hutapata jibu maana kashaingia tatizoni
 
Sio kama tunalipa......kuanzia hapo juu ni sista yetu Madame B, DEMBA ni pacha.Wote tunalipa ile mbaya!!!

Miili yetu ni mnato, inavutia.
Kwanini tusivae nguo fupi mdogo wangu!
Watuache tuvae miss strong...
Kama wanaona wivu, wamwambie Paw awapige Ban.
Watoto tumeumbika.
Mwili nyoronyoro.
 
Last edited by a moderator:
kama bado una bibi jaribu kuangalia nguo alizokuwa akizivaa miaka hiyo,.. Kama ni kabibi ka mjini basi hutapata jibu maana kashaingia tatizoni

Nauliza utamaduni wa mtanzania. Tusijekuwa sote twalaumiana kwa utamaduni wa kuiga. Tofauti ikawa nani kaiga nini na wapi. Tujue mavazi ya kitamaduni ya mtanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…