Inategemea na umri wa huyo msichana unaeanzisha nae mahusiano.
Wapo wale ambao unatongoza leo, anakubali kesho mchana, ikifika usiku anakwambia hana hela ya kula. Hapo unajiuliza nisingejitokeza angepitishaje usiku wa leo.
Wapo wale ambao baada ya wiki mbili kwenye mahusiano anakwambia kuna kiwanja alichukua goba akalipia nusu, bado nusu. Mwenyewe alimuahidi mwezi uliopita sasa hajamlipa, anasumbua huyo honey. Kidume Unajionea dubuli dubuli tu.
Wapo wale ambao kama mnafanya kazi ofisi moja au ofisi za karibu karibu, akishaamua kukubalia ombi lako basi atakuita baby mida ya breakfast na lunch ili umtoe. Mkiachana hapo hata usiku ukipiga simu haipokelewi, na akipokea atakwambia kachoka anaomba apumzike. Baada ya nusu saa ukijaribu kumpigia tena unakuta simu busy. Dah, ngachoka mie.
Kimsingi vyuma vimekaza. Ukiona kidume kinalalamika kwa kuhonga 20,000 ujue hali si hali.
Huu ni ule muda wa wenye visu vyao visivyoisha makali kuwa na mabebezi mingimingi tu tena wale classic wasiopenda za kuchuma wote.