Wachungaji na Mashehe wanafiki! - Mmevuna mlichopanda!

 
Wanajamvi wenzangu,

Katika post yangu ya mwanzo niliafiki hatua ya serikali kuhusu kodi dhidi ya taasisi za dini. Nimemsikiliza Mama Kyendesya akichangia, mawazo yake yaliendana na yangu. Lakini nimetafakari usiku na kwenda mbali zaidi katika kuchambua suala hili hususani katika kipengere cha gharama za shule za taasisi za dini.

Nimebaini kwamba taasisi hizi hususani makanisa kama Roman Catholic, KKKT, Aglican na Moravian wanatoa huduma zaidi na justification ya hilo ni kama ifuatavyo;

Tuchukulie mfano wa St Frances ya Mbeya, ada ni shilingi milino 1.8 kwa mwaka ikiwa na wanafunzi 420 tu kwa kidato cha kwanza hadi nne. Hii ina maana kwamba makusanyo ya ada kwa mwaka ni shilingi milioni 756.

Shule ya Wazazi ya Mbalizi yenye ina wanafunzi 1,500 na ada kwa mwaka ni shilingi 800,000; Kwa maana hiyo makusanyo ya ada kwa shule hiyo ni shilingi bilioni 1.2 kwa mwaka.

Unapozilinganisha shule hizi mbili katika utoaji huduma kwa walimu na watumishi wake wengine, huduma kwa wanafunzi na mazingira ya shule zenyewe utabaini tofauti ya mbingu na ardhi, shule hiyo ya taasisi ya dini inaizidi kwa mbali sana hiyo shule nyingine.

Baada ya kuingia kwa undani kiasi hicho nakubaliana kabisa na wale wanaopinga hatua ya serikali kuzibana taasisi za dini, na kama wamebaini kuwepo kwa utapeli kwa baadhi basi wawashughulikie hao kama wahalifu.

Serikali yetu bado haijafikia hatua ya kutoa elimu bora kwa watoto wa wakulima kutokana na aina ya viongozi tulionao sasa, pengine huko bele tutakapopata watumishi wa wananchi.
 
 
Serikali imeondoa msamaha wa kodi kwenye supplies au importation ya goods au services ambazo hazitumiki kny ibada moja kwa moja kwa moja kama vile, magari ya kanisa au ya wachungaji, furniture etc

Is there a better way to exemplify shortsightedness?
 
naona ndoa ya serikali ya wanadamu na dini bandia inaimarika zaidi muda huu kwa kupeana mahela na kila mmoja kumsifia mwenzake kama mume na mke wanavyofanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…