Nipo senkenke machimboni, Kuna wachina wamefungua mgodi wa kuchimba dhahabu, sasa wanawandanganya watendaji wa serikali kuwa, hawajaanza uzalishaji.
Wachina wanasema bado wanakusanya mchanga, kumbe walishaanza siku nyingi kuzalisha!! juzi Kati Kuna wachina walikuwa wanarudi China, waliondoka na dhahabu ya kutosha! ambayo walienda kuiuza dar kwa mhindi mmoja hivi!! dhahabu hio iliuzwa kws Tsh 280 million.
Pili Kuna wachina wanafanya kazi bila kuwa na vibali vya kufanya kazi nchini!! Wachina hawa wamekuwa wskiingia Kama watalii na kupotelea hapa nchini!!
Nazishangaa mamlaka!! hazilioni hili?wachina wanasafiri kwa gari kutoka dar hadi shelui bila kukamatwa njiani!? hili linafikilisha!!
Mara nyingi huwa wakienda watu wa uhamiaji pale mgodini, wachina wasio na vibali vya kufanya kazi nchini, hutolewa hapo mgodini na kupelekwa maeno ya nkonkilangi na wakati mwingine hupolekwa ziwani doromon, inaonekana Kuna mkubwa huwa anajulisha!!
Leo nimeona Kuna watendaji ws serikali wamepita wakielekea mgodini, sijui Kama wanalijua hili!?