Wachina kuvamia usafirishaji ni Halali?

Competition ndiyo mwarobaini wa bei za juu. Mlaji wa kawaida anachotaka ni unafuu wa maisha wakati wafanyabiara wanataka kuwakandamiza walaji. Serikali inachotaka ni kodi na ajira kwa wananchi wake. Wachina wakileta mabasi yao kwa wingi, huduma ya usafiri itapatikana kwa bei nafuu, serikali itapata kodi na kampuni hizo zitaajiri makonda, madereva, wafagizi, mafundi wa magari na baadaye youtong watafungua tawi la magari yao na vpuli vya youtong hapa. Uchumi utakua. Unasemea wafanyibiashara wa kitanzania wasiokuwa hata na vision wanataka nauli ya Mbeya DSM iwe shs 50,000 na wapandishe kila kukicha! Big up wachina
 
Okay.
Wakala wa #Yutong ni mtanzania ambaye na kwa taarifa yako mtoa chairmanships huyu jamaa anatoa mikopo kwa hayo mabasi hata kama ni 100, ili mradi mkubaliane kwenye
'term and conditions' na ndiyo maana #Yutong ni nyingi sana kuliko #Zhongton .

Wakala wa #Zhongton ni mchina ambaye hatoi mikopo kwa gari mpya ila anafanya ulichosema but ukiwa na pesa robo tatu ya gari used anakupa then umaliza kulipa taratibu.
Kuna watu wanafaidika nao hao kama utakuwa nao karibu si kuwaogopa.

Alafu hipo hv, huyo wakala wa #Zhongton ameingia mkataba na kampuni inayotengeneza hizo basi hivyo mnunuaji yeyote lazima apitie kwao, kama mfuko wako mkubwa basi unaweza kwenda kiwandani moja kwa moja, lkn kwa sababu wao ndiyo wameshika soko basi hunabudi kuwaona.

Mwisho mabenki unayasema vibaya mdau, #Bank zote zipo kibiashara labda kwa sababu hujui kuingia kibiashara kwenye hayo mabenki na ndiyo maana hauoni asubuhi kwako.
>>Ukiwa na mtaji unaozunguka na upo bank yoyote ya kibiashara na wewe ukataka kuwekeza kwenye biashara kama yako bank statement yako kama inapendeza kwenye in/out Manager wa bank yupo pale kwa ajili yako, hawezi kukunyima (labda kama mkono wako mfupi!!)

Mwisho ukifanya kazi kwa hao (wakoloni wa kichina bado kuna discipline ya kazi, hata kwa huduma, maana ukikosea wanakuadhibu wenyewe na ndiyo utaratibu wao.
 
wenzetu wanalipa mikopo,ila sisi ni wabishi,mfano Mbowe,Mengi,wana madeni sugu na ya mda mrefu hawataki kulipa
SASA KWA HAO WACHAGA WALAFI NDO IWE KIGEZO CHA WATZ WEUSI KUKOSA MIKOPO?
National Bank of Commerce ilikuwa inatujali mkaiuza
CRDB ilikuwa ya wakulima Mmeigeuza maumbile yake..
kama hujui ile ni Cooperative Rural Development Bank..
lakini iko kinyume na maumbile yake.
Sasa sisi Wazawa weuzi kimbilio letu ni lipi?
Au tuwe wezi?
 

wengi wetu hatulipi madeni
 
Nijuavyo mimi kila biashara ina masharti yake. Unapotaka kuniuzia kitu ni lazima pawepo na makubaliano, dalali sio, anajiingilia tu kituo cha mabasi na kuanza kupiga debe, kama sitaki ananifanyia fujo. Serikali iko kimya tu wakati mimi nailipa kodi na serikali ni jukumu lake kuweka mazingira mazuri kibiashara. Kama biashara ya udalali ni halali, basi ingefaa isajiliwe na wapewe masharti ya biashara. Sasa serikali iko kimya haimlindi mfanya biashara na kwa sababu hawaoni pingamizi wanazidi kuongezeka
 

Mkuu umeeongea kitu Cha msingi sana udalali ndio unaua uchumi wetu eti usipoweka dalali unaweza kususiwa . Wataje wakija wanawadanganya wateja kuwa magari hayo yamefilisika au ni mabovu. Na hawa ndio wamejaa ubongo juzi ndio walikuwa wanamtupia mawa makonda. Dawa hapa ni kuja na e bus ticket Kama ndege
 
Mleta mada atakoma anavyoshambuliwa ni kinyume na matarajio yake
 
Unapokata tiketi unaonyeshwa picha ya basi zuri, kesho yake sasa wakati wa safari ndo utaisoma namba unapandishwa basi kama banda la kuku na huna la kufanya....

Nimekuwa victim wa hii kitu mara mbili, nyakati tofauti...daaah
 
Huyu mleta mada sasa anasema nini jamani? Yaani sijaona sababu ya yeye kulia lia hapa jamvini. Sisi watanzania tunataka huduma bora tena kwa bei ambayo nafuu na inayoeleweka na siyo ujanja ujanja mnaofanya nyinyi ambao mnajiita wazalendo. Mzalendo gani unanyanyasa wengine tena kwa kuwabambikia bei. yaani unakuta ticket inaandikwa elfu 25, ila abiria unakamuliwa utoe elfu 30. wachina naamini hawawezi kufanya hayo magumashi. Tena ikiwezekana wachina waanzishe shirika la kutoa umeme hapa nchini, manake hawa Tanesco hawasomeki kabisa.
 
Reactions: mk4
acha hofu scandavia wako wapi walikuwa wanatoka na abiria watatu?
 
Hivi opportunity hii umiona baada ya wachina kuingia au la.
Tatizo letu sisi hatuko imaginative hatuko enterprising tunangojea mmoja aanze ili wengine wafuate.
Kutokana na hili wakulaumiwa siyo kinachopaswa kufanya ni kugundua fursa na kuitumia lakini sisi kazi yetu ni kuigana tu
nikifungua baa na ikaonekana kuwa na wateja basi jirani yangu naye atafanya hivyo pamoja na mwingine
na mwisho wa siku tunalalamika kuwa hakuna biashara wakati wanywaji wapo.
 
Asante saint ivugha.
Sijui watu wanafikiriaje !

Sasa nyie n mingarangara yenu na malori mnataka kuendelea kutuua kwa huduma mbovu? Mbasi yenu yamejaa kutu, ndani vyuma tupu, huduma mbovu!

Ndio maana Scandinavian Express aliwanyoosheni sana.
 
Tusimshambulie sana.. Ba Brio ila yeye lazima akubaliane na changamoto hii ya wawekezaji wa kichina Ktk sector ya usafiri
 
Last edited by a moderator:
Na huu ni mwanzo tu. Ujinga wa wabongo ni kufanya biashara kienyeji na kutegemea kujifichia kwenye uzalendo. Nani kawaambia kutumia huduma isiyokidhi ndio uzalendo?
Kwanza mlianza wenyewe kwenda kununua mabasi yao (YUTONG, ZHONG TONG BUS nk) badala ya kuendeleza kiwanda cha nchini au at least East Africa, sasa wameiona fursa wamekuja mnaanza kulia tena?
Uzalendo Tanzania ni msamiati wa kigeni tu.
Na mnaotulangua vyakula vya ovyo wakati wa safari katika hoteli zenu huko porini mjiandae maana wachina wanakuja kujenga za kwao na kutuuzia vyakula kwa bei nafuu kabisa
 
Usiletee mambo ya wazulu hapa kwetu Tanzania, dunia ya sasa iko kwenye biashara huria.pia Mimi nashukuru jins hawa wachina wanavyotusaidia wasafiri kwa kutuwezesha kusafir kwenye mabasi ya kisasa kwa bei nafuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…