Wachezaji Polisi Tanzania wapata ajali, mmoja avunjika miguu

Wako mstari wa mbele kupiga watu faini kwa sababu ya makosa madogo madogo! Chakushangaza wenyewe wanatumia gari bovu!!
 
Mungu awajarie wapone haraka, kagera sugar punguzeni basi kale kababu kayanga kanaharibu Sana soka la kisasa tuloaanza kulitengeneza kutoka kwenye hizo imani. Sasa hivi Kila team inaanza kuzifatilia imani za huyo mzee
 
Kikosi cha timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kimepata ajali leo Ijumaa Julai 9, 2021 wakati kikitoka mazoezini katika Uwanja wa TPC.

Makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Robert Munisi amesema,”kwa sasa ni mapema kuwa na taarifa ya nini kilitokea lakini kwa kifupi gari liliacha njia na kugonga mti, hivyo kwa haraka walioumia ni zaidi ya wachezaji 10 na Mathias Mdau amevunjika miguu yote miwili.”

"Dereva wetu amevunjika mbavu moja, ndio taarifa za awali ninazoweza kukueleza lakini bado naendelea kufuatilia hapa KCMC walipokuwa majeruhi na kisha nitatoa majibu kamili ya kilichotokea.”

Polisi Tanzania inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 42 na ilikuwa inajiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliopangwa kuchezwa wiki ijayo katika Uwanja wa Ushirika Moshi.

Chanzo: Mwananchi
Hivi Beti,wewe ni mtu au roboti? Sijawahi ona reply yako humu zaidi kutoa habari tuuu!! Natamani siku niuone mwandiko wako
 
Pole sana Mkuu.

Poleni sana, kuvunjika miguu yote miwili ni changamoto kubwa. Binafsi napitia changamoto hiyo ya kuvunjika mguu mmoja wa kushoto, nipo hapa mwezi wa nne sasa kazi zikiwa zimesimama.
 
Pole sana mkuu.

Jamaa yetu alifanya fujo sehemu akajikuta amevunjika mguu mmoja. Amefahamishwa anatakiwa kupata bed rest ya miezi 6 then miezi 6 mingine ya mazoezi madogo madogo.

Pia Bwana Dakta ameshauri jamaa asigegede kabisa for the next 14 month kwasababu hilo litapelekea mfupa usiunge vizuri.

Terrible, ndo kwanza jamaa ana wiki ya pili
@Pep sio mchezo usigegede dah
 
Poleni sana, kuvunjika miguu yote miwili ni changamoto kubwa. Binafsi napitia changamoto hiyo ya kuvunjika mguu mmoja wa kushoto, nipo hapa mwezi wa nne sasa kazi zikiwa zimesimama.
Pole mkuu
 
Poleni sana, kuvunjika miguu yote miwili ni changamoto kubwa. Binafsi napitia changamoto hiyo ya kuvunjika mguu mmoja wa kushoto, nipo hapa mwezi wa nne sasa kazi zikiwa zimesimama.
Pole sana mkuu.
 
PView attachment 1848322View attachment 1848324View attachment 1848323View attachment 1848325
IMG-20210709-WA0030.jpg
 
Pole sana mkuu.

Jamaa yetu alifanya fujo sehemu akajikuta amevunjika mguu mmoja. Amefahamishwa anatakiwa kupata bed rest ya miezi 6 then miezi 6 mingine ya mazoezi madogo madogo.

Pia Bwana Dakta ameshauri jamaa asigegede kabisa for the next 14 month kwasababu hilo litapelekea mfupa usiunge vizuri.

Terrible, ndo kwanza jamaa ana wiki ya pili
Asante sana mkuu,ila hapo kwenye kugegeda pagumu sana kukaa kwa mda wote huo
 
Back
Top Bottom