Wachezaji Polisi Tanzania wapata ajali, mmoja avunjika miguu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kikosi cha timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kimepata ajali leo Ijumaa Julai 9, 2021 wakati kikitoka mazoezini katika Uwanja wa TPC.

Makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Robert Munisi amesema,”kwa sasa ni mapema kuwa na taarifa ya nini kilitokea lakini kwa kifupi gari liliacha njia na kugonga mti, hivyo kwa haraka walioumia ni zaidi ya wachezaji 10 na Mathias Mdau amevunjika miguu yote miwili.”

"Dereva wetu amevunjika mbavu moja, ndio taarifa za awali ninazoweza kukueleza lakini bado naendelea kufuatilia hapa KCMC walipokuwa majeruhi na kisha nitatoa majibu kamili ya kilichotokea.”

Polisi Tanzania inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 42 na ilikuwa inajiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliopangwa kuchezwa wiki ijayo katika Uwanja wa Ushirika Moshi.

Chanzo: Mwananchi
 
Poleni, mchezaji kupoteza miguu miwili na ukizingatia huduma ya tiba Tanzania!!! lazima achanganyikiwe. Kuacha njia is normally associated with speeding.
 
Wakiambiwa kulinda raia na mali zao wanasema polisi hawatoshi na muda haupo, mnaona sasa ajali zinawaumbua
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Mzee mpili atatajwa hapa na jamaa wa mudi..

Kwa huyo jamaa aliyevunjika miguu miwili na ukizingatia ajira yake ni soka na soka linategemea miguu.. Dah
 
Poleni sana, kuvunjika miguu yote miwili ni changamoto kubwa. Binafsi napitia changamoto hiyo ya kuvunjika mguu mmoja wa kushoto, nipo hapa mwezi wa nne sasa kazi zikiwa zimesimama.
Pole sana ndugu
 
Ukweli magari ya polisi huwa sina amani hata likinisogelea, hayanaga service kabisa, OC inaishia kwenye kulipa utilities na posho.
 
Poleni sana, kuvunjika miguu yote miwili ni changamoto kubwa. Binafsi napitia changamoto hiyo ya kuvunjika mguu mmoja wa kushoto, nipo hapa mwezi wa nne sasa kazi zikiwa zimesimama.
Pole sana mkuu.

Jamaa yetu alifanya fujo sehemu akajikuta amevunjika mguu mmoja. Amefahamishwa anatakiwa kupata bed rest ya miezi 6 then miezi 6 mingine ya mazoezi madogo madogo.

Pia Bwana Dakta ameshauri jamaa asigegede kabisa for the next 14 month kwasababu hilo litapelekea mfupa usiunge vizuri.

Terrible, ndo kwanza jamaa ana wiki ya pili
 
Pole sana mkuu.

Jamaa yetu alifanya fujo sehemu akajikuta amevunjika mguu mmoja. Amefahamishwa anatakiwa kupata bed rest ya miezi 6 then miezi 6 mingine ya mazoezi madogo madogo.

Pia Bwana Dakta ameshauri jamaa asigegede kabisa for the next 14 month kwasababu hilo litapelekea mfupo kutokuunga vizuri.

Terrible, ndo kwanza jamaa ana wiki ya pili
Miezi 14 bila kupiga miti Aisee? Si bora kujiua tu ufe kishujaa. Kuna haja gani sasa ya kuendelea kuishi bila nyoka kuteleza pangoni?
 
  • Kicheko
Reactions: Pep
Back
Top Bottom