Wachapana makonde kisa mke wangu

Wachapana makonde kisa mke wangu

Pedra buyer

Member
Joined
Apr 26, 2015
Posts
97
Reaction score
32
Habari zenu wana Jf,

Mke wangu kwa nini unafanya hivyo? Ni swali ninalojiuliza kila ninapomkumbuka,hakuna ambacho anakosa lakini anafanya mambo ya aibu roho inaniuma sana.Nilipigiwa simu nikiwa kazini ilihitaji nifike haraka nyumbani kuna tatizo, baada ya kufika nilishangaa kukuta watu kibao wakishuhudia vijana wawili wakipiga na kutoana damu nyumbani kwangu.

Nilimuuliza mmoja wa majirani zangu kuna nini nikaambiwa muulize mkeo! Mda huo mke wangu alivyoniona kakimbia sikujua kaelekea wapi, nikamuuliza dada wa nyumbani akaniambia "dada alitoka aliporejea alikuja na na mkaka mmoja alinionesha kwa kidole mara gafla ilikuja gari ndogo akashuka kijana yule mwingine na wenzake ndipo walipomuita dada nje alitoka wakiwa wameshikana na na mkaka alioingia naye.

Ndipo ugomvi ulipoanza mmoja akimshutumu mwenzake kwa mini unatembea na mpenzi wangu ndipo walipoanza kutukanana na kupigana''. Ni siku ya tatu leo tangu kutokea kwa tukio nimeshindwa kuchukua uamuzi wa aina yeyote sielewi nifanye nini na ndugu wa mke wangu wananiomba tukae tuyaongee, sasa nawauliza tuongee kuhusu nini? Eti tumuombee msamaha yaishe wakati sikumfukuza wala kumpiga kaondoka mwenyewe.

Naombeni ushauri, maana kila maamuzi nayotaka kuchukua naona sheria itanibana.
 
Duh sasa tukushauri nini?
au tukushauri na wewe uwapige hao vijana?
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Maamuzi gani tena..huyo kashajihukumu mwenyewe..cha msingi asirudi tu
 
Hivi mwanaume una act kama boy kwanini ?
 
''Muishi kwa shida na raha kwenye ndoa hadi kifo kitapowatenganisha''-Padri.
 
yaani mpaka majirani wanakereka na tabia yako ya kuacha nyumba yako kuwa danguro....
 
hiyo ni habari ya kutunga usifanye mchezo na mke, tena ushahidi ubaoni. Ndugu kama ujaoa nakuomba uoe halafu ujue uchungu wa mke. Hizo ni porojo
 
hata kama yeye ndie bread winner wa mji wako,mkuu asirudi kabisa..hii ni aibu ya karne.
by the way wewe ni mtunzi mzuri sana
 
Back
Top Bottom