kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,315
- 12,614
Nimeshuhudia dereva wa lori akichomolewa na kupigwa na dereva wa bodaboda baada ya dereva wa lori kumsukumia mtaroni dereva wa bodaboda.
Sio kwamba timu ikiwekeza sana lazima mara zote iifunge timu yenye uwekezaji mdogo. Wachambuzi wetu wanazilazimisha Al-Ahly na Mamelodi izifunge Simba na Yanga kwenye mashindano ya CAF champions eti kwakuwa zina uwekezaji mdogo kuliko al-ahly na mamelodi. Uchambuzi wa aina hii hauonyeshi weledi. Wachambuzi wanasahau factors za muunganiko wa timu, ari za wachezaji (self motivation) na uzuri wa mabenchi ya ufundi ya kila timu.
Ni kweli uwekezaji wa lori ni mkubwa kuliko uwekezaji wa bodaboda na ni kweli lori linapoigonga bodaboda mara zote lori litaiharibu zaidi pikipiki, lakini sio kweli kwamba mara zote dereva wa lori ana nguvu zaidi kuliko dereva wa bodaboda.
Timu zote zina wachezaji waliozifikisha timu zao robo finali, Pale uwanjani wanacheza wachezaji (madereva) sio pesa (malori na bodaboda).