Kuongezeka kwa kadi nyekundu katika raundi tano za mwanzo wa ligi ni jambo la kusikitisha. Hali hii imekuwepo kwa sababu inachochewa sana na vyombo vya habari.
Katika hali isiyo ya kawaida, mwaka jana, timu ya prisons walikuwa wakiruka mithili wanacheza kung-fu hasa walipokutana na Simba.Hali hii ilikuwa inahatarisha sana usalama wa wachezaji na Luis akifanyiwa ukatili mkubwa uwanjani bila hata kadi kutolewa.
Wachambuzi waliita jambo hilo eti "mgongano wa kawaida kwenye mpira"
Na walienda mbali zaidi na kuwahamasisha wachezaji wa timu nyingine kucheza michezo ya rafu sana ili kuwatisha Simba na hatimaye timu hizo zipate ushindi.
Pamoja na kuwepo watu wengine wakiwa viongozi wa serikali,kutoa pesa kwa lengo la kuhakikisha baadhi ya wachezaji muhimu wanaumizwa,ili club zote zisifanye vizuri kimataifa, bado naona watu hatari zaidi ni hawa wachambuzi ambao wamepewa platform ya kuongea kwa umma na wanasifia ujinga huu. Wao kumvunja mchezaji ili upate ushindi ni kitendo cha kawaida.
Sasa kwa vile kuna chuki, kukamiana, na waamuzi kutokuwa na uwezo wa kumudu kuchezesha soka kunakotokana na ushabiki wa vilabu hivi vikubwa, hali hii imewafanya wachezaji wanaodhania wanakamiwa na hatua aghalabu kuchukuliwa, kuanza kujilinda kwa kulipiza kisasi ama kucheza mpira wa nguvu na kukamiana.
Hali hii isipokemewa itasababisha wachezaji wengi waumie, wasicheze muda wa kutosha,na hata kuwastaafisha baadhi yao kabisa katika soka.
Ingekuwa ni katika siasa kuna wachambuzi wa soka walitakiwa kuwa mahakamani kujibu tuhuma za uchochezi wa vurugu mpirani.