Wachambuzi wa Clouds FM hawana weledi

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,980
4,451
Yani jana nimeishushia hadhi sana hii radio hasa kipindi cha michezo.

Binafsi sina ujuzi wowote wa kuchambua mpira lakini game ya jana kati ya Barca na PSG nilijua kabisa Barca anakufa, jambo la kushangaza kila mchambuzi akadai PSG hana pa kutokea kwa Barcelona.

Wachambuzi kama hawa wamaweza kwenda BBC kweli kwa ushabiki wao badala ya kuangalia vikosi? Kwanini waiuwe PSG moja kwa moja badala ya kusema game itakuwa ngumu?

Bado Edo Kumwembe na George Ambangile watatawala sana kwenye uchambuzi sio hawa wanazi na mashabiki.
 
Sasa Kosa ni nini apo kila mtu yupo na prediction zake na hakuna mchambuzi ambaye anayekuwa accurate yani acheze Simba Na kagera Na wachambuzi wakatabiri simba anashinda then Simba akafungwa na ww ukaanza kulaumu kwamba hawawezi kuchambua
Mfano hauendani
 
Yani jana nimeishushia hadhi sana hii radio hasa kipindi cha michezo.

Binafsi sina ujuzi wowote wa kuchambua mpira lakini game ya jana kati ya Barca na PSG nilijua kabisa Barca anakufa, jambo la kushangaza kila mchambuzi akadai PSG hana pa kutokea kwa Barcelona.

Wachambuzi kama hawa wamaweza kwenda BBC kweli kwa ushabiki wao badala ya kuangalia vikosi? Kwanini waiuwe PSG moja kwa moja badala ya kusema game itakuwa ngumu?

Bado Edo Kumwembe na George Ambangile watatawala sana kwenye uchambuzi sio hawa wanazi na mashabiki.
Brazee ulibet, ukampa Barca kwa uchambuz wao.
 
Kazi ya kutabiri siyo ya wachambuzi wa mpira....ingekua wanajua hizo predictions wasingeajiriwa kwenye hivyo viredio na vitv instead wangejiajiri kwenye ku bet maana kule mpunga ni mwingi....hizo lawama zako hazina msingi wowote as zime base kwenye prediction.
 
2019 clouds fm Ina wachambuzi feki ndio maana siwasikilizi binafsi Ni mpenzi Sana wa Sports Arena ya Wasafi fm
 
Kazi ya kutabiri siyo ya wachambuzi wa mpira....ingekua wanajua hizo predictions wasingeajiriwa kwenye hivyo viredio na vitv instead wangejiajiri kwenye ku bet maana kule mpunga ni mwingi....hizo lawama zako hazina msingi wowote as zime base kwenye prediction.
Mleta mada yupo sawa. Kwa kikosi alichonacho Barca au Madrid kwa sasa huwezi kusema wanashinda dhidi ya timu zenye vikosi imara kama PSG,BAYERN na Man City.
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom