Wachagga hii ni kweli?

Wachagga hii ni kweli?

Status
Not open for further replies.
Binafsi nawakubali wachaga kwa sababu ni wachapakazi tofauti na makabila mengine hasa ya mikoa ya Pwani. Kazi yao ni kukaa kwenye bao asubuhi mpk jioni na kuongeza wake tu.
 
Watu hawafanyi kazi,wanakalia majungu tu na fitna. Makazini humo wamejaa watu ni majungu tu ufanisi hamna.
 
Binafsi nawakubali wachaga kwa sababu ni wachapakazi tofauti na makabila mengine hasa ya mikoa ya Pwani. Kazi yao ni kukaa kwenye bao asubuhi mpk jioni na kuongeza wake tu.

hahahaaa...... Nakwenda sokoni
 
A MODEST PROPOSAL

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna vumbi la chuki, fitina, wivu, kisasi, na hisia za kibaguzi dhidi ya jamii ya Wachagga nchini. Kuna kila dalili kuwa jamii ya Wachagga nchini siyo tu inaanza kutengwa lakini uwepo wake katika nafasi mbalimbali za uongozi inazua hoja ya ukabila kwa haraka zaidi yawezekana kuliko kabila jingine lolote nchini. Katika Tanzania yetu, wachagga wameanza kunyoshewa kidole siyo kwa siri tena bali kwa wazi kabisa tena na watu ambao wakati mwingine hawapati hata kigugumizi.

Ubaguzi huo msingi wake mkubwa ni idadi ya wachagga katika nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kuhusiana na elimu yao. Kuanzia mara tu baada ya uhuru jamii ya wachagga mojawapo ya jamii ambayo watu wake wengi wamesoma sana na kufanikiwa kielimu na kiuchumi imekuwa ikinyoshewa kidole cha kupendelewa.

Mtu yeyote ambaye anaweza akafanya uchambuzi yakinifu hatoshangaa kukuta wataalamu wa kichagga katika nafasi mbalimbali za uongozi au taaluma nchini. Kwenye vyuo vikuu, kwenye idara za serikali na hata kwenye taasisi binafsi kumejaa watu wenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hususan watu wa jamii ya Kichagga.

Endapo itatangazwa nafasi yoyote ya kitaalamu usishangazwe ukiona kuwa waombaji wengi wana majina ya "Kichagga".

Ni kwa sababu hiyo basi kuna kila dalili kuwa kutokana na wingi wao katika nafasi muhimu na vyeo mbalimbali (hata ndani ya Jeshi la Polisi) Wachagga siyo tu ni wengi lakini wanaonekana kufanikiwa zaidi. Hili ni tishio kwa baadhi ya watu. Ni tishio kwa watu ambao hawako tayari kuangalia jitihada za watu katika kufanikiwa kwao na matokeo yake kushutumu ukabila kila idadi ya Wachagga kwenye kitengo fulani inazidi mmoja.

Ushauri wangu ni kuwa, kwa vile Wachagga wameshasoma sana na kuendelea katika biashara karibu mikoa mingi nchini. Na kwa vile wanaendelea kufanikiwa pia katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini, basi itakuwa vizuri kama watajitolea kuachilia nafasi hizo ili kuwapa nafasi watu wa makabila mengine.

Kwa vile ni wao wanaonekana kulalamikiwa kutokana na mambo ya kifisadi aidha kwa moja kwa moja au kwa kuashiria basi ni vizuri wawape watu wengine nafasi hizo hata kama watu hao hawajasoma sana. Hii yote itakuwa ni katika kudumisha mshikamano, umoja na udugu wa Taifa letu.

Endapo Wachagga wataachilia nafasi mbalimbali kama UCEO, Ukurugenzi, Ukuu wa Idara n.k watasababisha watu wawapende na kuwakubali kuwa ni wazalendo wa kweli. Sitoshangaa kuwa ndugu zetu wa Jamii ya Kichagga wakikaa pembeni, basi ufisadi utakoma serikalini, idara zitaongozwa na watu wazuri, na mara moja na daima Tanzania itaanza kukua katika uongozi.

Kwa kupendekeza nashauri wabunge wote ambao ni Wachagga au wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro kuachia ngazi mara moja ili watu wa makabila mengine wapewe nafasi hizo. Siyo wao tu bali pia wabunge ambao wameoa au kuolewa uchagani vile vile wafuate nyazo hizo.

Wakishamaliza hao, wakuu wote wa idara za serikali ambao wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hasa wa jamii ya kichagga (wamarangu, wamachame, wa Rombo, na wa Kibosho) na wao waamue kuachilia nafasi hizo kwa ndugu zao Wamakua, Wamwera, Wa Ndali, Wadigo n.k Katika hili Wapare hawahusishwi.

Tukishamaliza wakuu hao wa idara za serikali ningependekeza madaktari wote wenye kumiliki hospitali binafsi ambao ni wachagga au wameoa/kuolewa uchagani na wenyewe waamue kuingia ubia na watu wa makabila mengine kama wangengereko, wambuu, na wanjiro ili hayo makabila madogo na wenyewe wapate nafasi ya kujifunza fani hizi muhimu.

Zaidi ya yote, majaji na mahakimu wote ambao wana asili ya Uchaggani na wenyewe waamue kujitoa katika nafasi hizo kwani wingi wao pia unaonekana sana na hivyo kuwa kikwako kwa watu wa makabila mengine kufanikiwa zaidi katika nyanja ya sheria. Kwanza kabisa wale majaji wa Kichagga wa mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu wawe wa kwanza kuweka manyanga chini.

Katika kufanya hivyo jamii ya Watanzania ambao inaona ukabila wa wachagga katika sehemu nyingi itaridhika kwani kwa mara ya kwanza tutakuwa tumeshughulikia chanzo cha matatizo yetu mengi


I thought there is point here but it is rubbish,influenza. Send it to recycle !
 
Wachagga leo tukutane Rombo Green View hotel tujadili hii thread.
 
Ni kweli ni wachapakazi!!!! Huwezi kuta mchagga kijiweni anacheza bao na busha limening'inia eti ajiite muungwana!!
Hata Mimi nimeishi uchagani nimejifunza, nimebadilika na hata wakwetu pwanipwani nawasihi wabadilike!!!!

Mkuu tutake radhi!!! Busha! Astakhafilulah!!
 
At least wachaga tu cha kuzungumziwa, nyie wenzetu hamna makabila?
 
Hivi hao wachaga wamejaa wapi?! Mbona mimi naona kuna balance nzuri tu. Miaka ya nyuma kulikuwa na kauli kwamba nenda duka Fulani la mchaga, lakini kwa sasa kila mmoja ana duka mahala popote labda iwe Rombo au Kibosho. Wasukuma, Wahaya, Wanyakyusa, watu wa Tanga na wengie wengine wanachukua sana nafasi siku hizi. Nilichokiona ni wasi wasi wa Wachaga kuwa sasa dominance yao inapotea. kwa mfano, outcry kadhaa za siku za karibuni nchini zinatoka na huo wasi wasi wa Wachaga. Mifano ni kama mashirika ya Bima, NBC, nyumba kuna ukabila kiutawala, so was Wizara ya Madini, Mambo ya nje na siku za karibuni vyuo vikuu kama ilivyotokea kelele Sokoine Univesity of Agriculture na kadhalika. Huu ni wasi wasi wa declining dominance ya Wachanga na rise ya wengine katika anga ya utawala nchini na kazi kwa ujumla. Hii notion imepitwa na wakati tubadirike sasa. Tufanye kazi kwa bidii bila kuangalia upuuzi huu ambao kule Kenya unawatafuna kama malaria

Si kweli, wachaga bado wana-dominate in every field! Kuna vitu ambavyo haviitahi degree ya chuo kikuu kielewa. Just go to any field where the head is the boss, you will notice a string of fellow clans men below! Nadhani hiyo ipo (kwa kiasi) katika makabila mengine, but is very vivid in chaga case! Anyway, lakini wamesoma sana, kuwa pale kunaweza kukawa na justification ingawa kwa sasa makabila yote yamesoma!!! Tunategemea a balanced distribution of workforce in varioud fields!
 
Sisi tunajadili UKABILa wakati mkuu wa kaya na mwanae wanachumia tumboni mali za watanzania,Mkoloni alitualibu kweli akiri zetu,mpaka leo tumekuwa walemavu wa akiri.
 
Mbona mnapenda kuongelea makabila? hapa jana si ni nyinyi mliokuwa mnapinga habari zinazowahusu watu kutoka mkoa wa Kagera eti kufanya hivyo ni ukabila?sasa hapa mbona mnaongelea wachagga? ama hili sio kabila hapa Tanzania? ...Tatizo Mods mmeruhusu hata wenye akiri finyu na wao kuonekana wanajua kuandika Jf,tuleteeni watu wanaopembua mambo siyo hawa wanaojua kuandika tu kitu kidogo wao wanakimbilia eti ukabila.

Unapopoteza muda wako kujadili ya wachaga ndivyo unazidi kudidimia. Unachotakiwa kufanya ni kuangalia wapi umekosea katika kujipanga kimaisha halafu chukua hatua mara moja kuyaweka sawa mambo yako. Utakalia kuhoji ya Wachagaaaa Wahayaaa wanyakyusaa wadigoooo na wengine wengiiii,hisi masaa na siku zikisonga mbele na uzee ukikodolea macho na hatima yake unakufa masikini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom