Mentality hii ndiyo iliyowakomboa wachaga kibiashara

Mentality hii ndiyo iliyowakomboa wachaga kibiashara

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,618
Reaction score
20,556
Maneno haya yaliandikwa kabla ya uhuru, 1953


BIASHARA NA WAHINDI

Haiwezekani kufikiria biashara ya nchi ya Kilimajaro bila kuwakumbuka Wahindi. Wahindi wamejiingiza katika biashara ya Kilimanjaro kuliko kabila lingine lo lote. Wahindi wananunua na kuuza karibu kila kitu Wachagga Wanachonunua. Wamejenga majumba makubwa na wamezuia biashara yote ya nchi.

Zaidi ya hayo wanapata karibu fedha zote za biashara na wanazipeleka India.

Njia iliyopo ni Wachagga kujiunga na kufanya biashara kwa umoja. Kama maduka makubwa ya umoja yakifunguliwa kwa msaada wa serikali kwa maonyi na uongozi mwanzoni, faida nyingi itapatikana ambayo itatumiwa kwa njia nyingi zitakazohitaji fedha siku hizi.

Sisemi Wahindi ni watu wabaya na kwa hiyo wafukuzwe kwa nguvu. Wahindi tangu walipoingia Kilimanjaro wamekwisha fanya kazi ya manufaa kwa nchi; hapakuwako duka hata moja walipokuja. Ni vizuri Wachagga watoe ahsante kwao. Lakini wakati umekuja sasa ambao ni lazima Wachagga wafanye biashara ya nchi yao na kuanza kushindana na Wahindi katika biashara polepole.
 
Siku hizi raia wamekuwa wazito kuelewa maandishi😅 Sijui tatizo ni kitu gani! Ni simu kulia atasa! atasa! kila saa🤣🤣. Mi nimekopi tu kama yalivyoandikwa kitabuni, hayahitaji hata context.
 
Kwahiyo serikali ijitoe kuwa support wachagga kufungua maduka??

Zamani ningefikiri uko zako kwenye bodaboda chini mti unajipostia baada ya kumaliza certificate ya hotel management na kukosa kazi,

Lakini kwa niliyoyashuhudia kwa macho yangu sijahadithiwa na mtu, wewe uliyetoa hii suggestion unaweza kuta una Masters ya Business kabisa tena kutoka Marekani na umeajiriwa wizara ya fedha.

I'm telling you!
 
Njia iliyopo ni Wachagga kujiunga na kufanya biashara kwa umoja. Kama maduka makubwa ya umoja yakifunguliwa kwa msaada wa serikali kwa maonyi na uongozi mwanzoni, faida nyingi itapatikana ambayo itatumiwa kwa njia nyingi zitakazohitaji fedha siku hizi.
Ni kweli unakuta biashara iko kwenye mikono ya familia tokea vizazi vitatu nyuma
 
Back
Top Bottom