Wacha nipangue hoja dhaifu za Lowassa na UKAWA

Wacha nipangue hoja dhaifu za Lowassa na UKAWA

jibu na hoja ya mzee kingunge, ya kuwa mkapa alikuta ukuaji wa uchumi ni 4% na akauacha ni 7%jk ameukuta hapo na kuucha hapo hapo!! ina manisha nini? na ni mapendekezo gani ya CAG, aliyotoa na kufanyiwa kazi? hao unaosema wako jela kwa ufisadi ni wapi hao, kina mlamba hiyo miaka 2?!sakata la escrow tuliwajua upande mmoja tu, Unasema tukashangae kenya wakati yanayotokea Tz ni zaidi na ya kenya, ETI Hadi leo rais bado anateua wakuu wa wilaya????!!!!!

Suala la kukua au kutokua kwa uchumi linategemea hali ya uchumi duniani. Kunapotokea mdororo wa uchumi, ukuaji huathirika.

Kuhusu mapendekezo ya CAG, hebu yaorodheshe hapa tukusaidie. Usiongelee vitu vya kufikirika tu.

Sakata la escrow lilikuwa na pande ngapi? Hebu tuambie ili tukutajie wale uwatakao. Kumbuka hoja za CHADEMA katika hili ni batili kwa sababu wao hutunga uongo ili kuwapumbaza watanzania kisha husema, walikaa na mtuhumiwa anawafafanulia kwa kina, hivyo wao wamemwlewa.

Nyongeza, mwombe mzee Kingunge aelezee mradi wa stendi ubungo na biashara ya mwanaye kinje
 
Sasa unaweza sikia eti huyu naye lilefungu limemfikia.Mbona hakuna hoja yeyote uliyopangua bwanamdogo?
 
12109097_734542480022998_9142661312703990731_n.jpg



Acha nianze kupangua Vihoja vya UKAWA moja baada ya nyingine:
Tatizo la vijana wa UKAWA ni kusahau au labda walikuwa wadogo wakati wa kampeni zilizo pita!


Hivi hamkumbuki neno UKAPA lilikuwa na Maana gani!!?
Ni kwamba wakati wa Mkapa hela iliondoka mikononi mwa Wananchi,maana ndo alikuwa anajaribu Kuimilikisha Uchumi Serikali.


Mambo hayakuwa matamu kwetu kulinganisha na ilivyo leo.
Ndio maana nawambia Maendeleo ni hatua! Na sio siku mia za Lowassa. Ndio maana kuna msemo wa "ROMA haikujengwa kwa siku moja".


Yale ambayo Kikwete hakuyatimiza Yatatimizwa na Magufuli...hiyo haiondoi Ukweli kuwa Kikwete kafanya Makubwa!


UFISADI:
Kikwete kajitahidi sana kupambana na Ufisadi.
Ndio maana kukawepo na CAG!!! Hiyo ni Uwazi na Uwajibikaji...ndio maana kuna Watu wapo Jela na Wengine mahakamani nk...na ndio maana siku hizi Malipo yanafanywa kwa simu! YOTE HIYO NI JUHUDI ZA KUPAMBANA NA UFISADI!!!


Lakini kubwa zaidi KIKWETE KASIMAMIA KUKATALIWA KWA LOWASSA KUWA MGOMBEA WA CCM kwa sababu hizohizo za KIFISADI. Lowassa ni Fisadi kwenye damu, kwenye roho, kwenye nafsi na kwenye akili yake.


ELIMU hatuko zero...matatizo ni kawaida unapoongoza Watu.


Labda UKAWA mkashangae Kenya!
Maana wapo chini ya Mabadiliko ya UPINZANI uliomng'oa Daniel Arap Moi na Mpaka sasa WAALIMU HAWAPO MADARASANI.


Ama kuhusu kesho;sio Watanzania tu,VIUMBE WOTE HATUJUI KESHO ITAKUWAJE.
Ndio maana Mtikila katokea Njombe kaja kufia Msola!!!


Angejua bila shaka asingesafiri!!!


KAJIPANGE TU.


#HapaKaziTu

Mr Chin

Huna hoja wananchi wanakufa kwa kukosa dawa hospitalini wewe unaonyesha barabara.wananchi wanakufa hawana kazi wewe unaonyesha barabara jichunguze
 
Mr Chin

Unasema maisha yamekuwa matamu seriously?

Kwa upande wangu naona maisha yamekuwa mabovu kila sector sahiv vijana wengi sana wanamaliza chuo hakuna ajira serikali imebinafsisha viwanda na vingine vimekufa leo hii unasema maisha yamekuwa matamu hauko sahihi kabisa.

Haya sio yale maisha bora tulioambiwa kipindi kile hata robo hayajafika kwann niendelee kuwa na imani na hawa watu tena?

Kila siku magufuri anajivunia katika barabara tu coz ndio pekee walichofanikiwa Tanzania tunakosa nn tuna kila kitu lakin bado masikini kwann tusibadili mfumo?
 
Last edited by a moderator:
Nijibu swali hili dogo. Iweje kwa miaka 10 ya kikwete asifufue viwanda? kwanini iwe ahadi ya Magufuli? kilishindikana nini ambacho kitawezekana sasa?

Kafufua uwezo wa wananchi kuuza na kununua madawa ya kulevya
 
Kwa hiyo magufuli ni mkweli kusema atajenga viwanda? Serikali inaweza kujenga vingapi? kwa takwimu zako ni vingapi vimekufa? na je atajenga viwanda gani na gani?

Unapozungumzia kujenga viwanda maana yake unataka kuongeza fursa za ajira.

Maana yake ni ukweli kuwa kuna maendeleo kielimu yamezaa tatizo ajira. Sasa ni wazi kuwa Magufuli atajenga viwanda
 
Kingunge ni mtumwa wa pesa...naona anatengeneza mazingira ya kulimbikiziwa vyeo UKAWA. Ngoja Magufuli aingie amfilisi huyu mzee na mwana atiwe ndani maana sembe zinaharibu vijana

Aanze na hao waliopo ndani ya sisiem, mbona hao wauza sembe wenu mnawaogopa? Akitoka mtu kwenye chama chenu ndio mnasema FISADI, MUUZA SEMBE, nk watajeni basi na walipo humo ndani. Mnawaharibu vijana na sembe CCM bora ifweeeee!!!
 
Nijibu swali hili dogo. Iweje kwa miaka 10 ya kikwete asifufue viwanda? kwanini iwe ahadi ya Magufuli? kilishindikana nini ambacho kitawezekana sasa?

Kwa ufahamu mdogo tu, kila kiongozi ni visionary. Anakuwa na maono yake. Vinginevyo maisha yangekuwa domant. Tuache propaganda za kama yule hakufanya hiki, huyu atawezaje.
 
Ku-maintain ukuaji wa uchumi kwa 7% kwa miaka 10 mfululizo mbona ni credit? Iwapo gari limetoka speed 40km/h hadi 70km/h na kumaintain hiyo speed. Je utasema gari haliendi?

Buree kabisa,kwa speed ya 7% na population ilikua 32mil,na sasa speed ni hiyo hiyo kwa population ya 58mil...

Kuna maendeleo hapo au ni kurudi nyuma karibu nusu ya speed...wewe ni buree kabisa

Kingunge anakwambia kwa population hii ya 58mil walao speed ya 15% ,wewe unaleta upumbavu kwenye maendeleo ya nchi

Mkwere katurudisha nyuma ,ya ni ujinga ujinga tu
 
Naona hoja yenu ya Mageuzi ya Kenya unaikimbia.
Mkuu hiyo ya Kenya, walimu kutokuwa darasani ina afadhari, kuliko wa kwetu ambao wapo darasani ki mwili na kifikra wapo kwingine. Jana kwenye taarifa ya habari itv wameonesha shule moja yenye walimu wawili tu, mmoja mwalimu Mkuu bila shaka mwengine atakuwa wa zamu miaka yote. Kwenye hali hii kwanini watoto wasi hitimu bila kujua kusoma na kuandika
 
Kwa ufahamu mdogo tu, kila kiongozi ni visionary. Anakuwa na maono yake. Vinginevyo maisha yangekuwa domant. Tuache propaganda za kama yule hakufanya hiki, huyu atawezaje.

Angalia shwaini mwingine huyu...sio kila mtu ni visionary maana transformational leaders ni rare...

Yaani nimekuja kujua na nimeprove ccm ni bunch la wajinga to the core...use your brain,soma vitabu,jinga jinga tu
 
Kelele za CHura hizii...tulishafanya maamuzi tunasubilia tarehe tu..
 
Mr Chin

Unaleta vionjo vyako vya moyo nakuita ni HOJA! ama kweli Elimu ya shule za kata ni majanga! CCM wanaamini wewe ndie kiboko wa proaganda! "shame upon you and your stinking CCM"
 
Last edited by a moderator:
Kwa ufahamu mdogo tu, kila kiongozi ni visionary. Anakuwa na maono yake. Vinginevyo maisha yangekuwa domant. Tuache propaganda za kama yule hakufanya hiki, huyu atawezaje.

Hizi ni propaganda? unaelewa maana ya propaganda?? Hujajibu kilishoshindikana wakati ule kitakachowezekana sasa.
 
Hizi ni propaganda? unaelewa maana ya propaganda?? Hujajibu kilishoshindikana wakati ule kitakachowezekana sasa.

Kwamba kilichoshindikana kwa Mwinyi kiliwezekanaje kwa Mkapa!!? Huna hoja, Obama kaja na mtazamo tofauti na Clinton. Kwanza tujiulize kwa nini kilishindikana kisha tuone kwa nini kiwezekane. Sio propaganda zisizo msingi
 
Kwamba kilichoshindikana kwa Mwinyi kiliwezekanaje kwa Mkapa!!? Huna hoja, Obama kaja na mtazamo tofauti na Clinton. Kwanza tujiulize kwa nini kilishindikana kisha tuone kwa nini kiwezekane. Sio propaganda zisizo msingi

Ni mwaka gani ambapo CCM imekuja na ilani tofauti?? Unatumia bongo yako sawasawa kweli??
 
Back
Top Bottom