Wabunge wetu na mabinti wa vyuo!

Wabunge wetu na mabinti wa vyuo!

Naomba PICHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA......
 
teh teh teh uwiii kwakweli inafurahisha na inasikitisha sana.

Lakini inawezekana na madereva wenyewe wanajipatia hapo hapo si wabunge tu, na inawezekana pia wanatumwa kupeleka pesa kwa watoto zao wanaosoma hapo, na inawezekana pia wakawa wanatumwa na mabosi zao (wabunge) kwa maswala ya kingono. Kwakweli sijui nchi inaelekea wapi kila kukicha hili, mara lile basi vurugu tupu.

Ila wabunge kama wanajua kuwa hao ni watoto zao ki umri si dhani kama wangefanya mambo kama hayo ni aibu mtoto wa miaka kumi na nane au hata ishirini na mbili kumvulia nguo wewe mbunge mwenye miaka arobaini hivi jamani huoni aibu? au ndo useme mtoto wa mwenzio mkubwa mwenzio?? lakini kumbuka wananchi tumekutuma nini!!!! na mabinti nao waache tamaa? bora mnapata hata hizo posho?? kuna tuliosoma enzi hizo hata posho hakuna, na wabunge basi msitumie pesa kuwarubuni vijana wadogo chukulieni hao ni taifa la leo sasa mnataka mlipeleke wapi?

Makaburi yamejaa jamani hakuna pa kuwaweka.
 
Ni kweli...Lakini kwa mtindo unaoendelea Dodoma tujiandae kuzika vijana wa kiume wasio na hatia!!! kwani hao Mabinti watajaolewa na Wakaka ambao hawajui maisha walioyapitia huko nyuma... Kina dada hao wajirekebishe...

TB, hali hii sio hapo Dodoma to ni vyuo vyote uvijuavyo, ndio hali ya kawaida kabisa kwa mabinti kujiuza, yaani ni kama kuna mashindano, nenda Tabora, Mwanza, Mtwara, Dar kwenyewe kwenye hivyo vyo vikuu au vya Jamii sijui ni balaa.

Yaani hapa ushauri pekee kwa vijana wetu ni kuwa kabla ya kuanza mahusiano au kuoa ni LAZIMA kuhakikisha unapima ngoma, maana yake mambo ndo yeshakuwa hivyo.

Gurtu anasema

Kwa hiyo kinachofanyika ni kuwa wanafunzi wanajiongezea posho zao za siku kwa njia hiyo na wabunge wanajipunguzia posho zao za siku kwa njia hiyo. :becky::becky::becky:
 
nilikutana na wadada (18 - 24) wa mtaani Dodoma mjini wakiilaumu sana serikali ya Jamhuri kwa kujenga vyuo lukuki dodoma kwani wameharibu soko lao, waheshimiwa sasa wananchukua wananchuo kuliko hawa wa dada wa mtaani.
Soko limeharibika na hali ni mbaya sana ki uchumi.
 
lakini kumbuka anaetoa huo Uzinzi ni mdada.........wadada wa siku hizi bana sio kama kipindi kile huwezi hangaika nae saaana just one day hata kama hamjawahi kutana nae UNAKULA MZIGO..... Hii ni mbaya sana dada anaangalia tu usafili na mfukoni kuna nini lakini hajui mwilini kuna wadudu gani

angalia hapo kwenye red, kisha mtafute anayetafuta uzinzi huo ni nani....
 
fuso: ungewaambia kama hali ni mbaya kiuchumi wajaribu kifo. Hizo ngono wanazoendekeza zitawapeleka huko bora waende kabla ya kungonoka.
 
Inasikititisha sana, tatizo linalokabili vijana wengi hasa wadada na kujikuta wanatumbukia kwenye mtego wa hawa wakubwa ni tamaa ya vitu ambavyo hana uwezo navyo. vijana wengi wanashindwa kuridhika na maisha waliyo nayo.... hasa vyuo kuna hiyo tabia sana!! Struggle upate vya kwako na sio shoti kati...
 
Hao mabinti wanapewa fedha kidogo za mikopo ambayo ni kama Tsh.5,000 kwa siku kwa ajili ya chakula na malazi na wabunge wamekataa kuwapigania waongezewe mikopo. Wabunge wao wanapewa fedha nyingi zaidi Tsh.100,000 kwa siku na wabunge nao hawataki posho zao zipunguzwe.

Kwa hiyo kinachofanyika ni kuwa wanafunzi wanajiongezea posho zao za siku kwa njia hiyo na wabunge wanajipunguzia posho zao za siku kwa njia hiyo. Hapo panaeleweka?
nimekugongea thanks hapa
 
Jamani, labda wamepewa ushauri na madaktari wao kuwa njia nzuri ya ku-refresh mind
ili kuondokana na tatizo la shinikizo la damu (kwa kuwa wanakula sana vinono na kusinzia
bungeni) ni kuwa na madadapoa. Who knows!
 
na hivyo vibwana vyao vya chuo pia viachane nao kwani dau lao ni dogo sasa, wanatoka na baba zao watawaweza wapi? jamani UKIMWI utaisha kwa jinsi hii??? Nilikuwa chuo kimoja nikaambiwa siku hizi kuna mapenzi ya mwisho wa geti chuoni. Yani msichana anakuwa na boyfriend wa chuo, akishatoka nje ya geti sio wake tena anafuatwa na (papaa, mume wamtu, mbunge, fataki) au hata bf wa mtaani, kwa hiyo jamaa asimuharibie yani anapotongozwa na kukubaliwa masharti ndo hayo akishatoka getini biashara ya kumpigia simu "akome" . sasa fuatilia hiyo cheni inayozunguka hapo. ukimwi utatumaliza
 
Weka picha za hayo mashangingi zen tumfahamu na kumshughulikia weka picha mkuu
 
Natabiri hii thread maxence melo ataifutilia mbali.....
 
Waziri Mkuu wa zamani amuweka kimada shoga
-shoga mwenyewe ni mwanasiasa mwenzake
-atanua naye zaidi anapokuwa mjini Dodoma
Waziri mkuu wa zamani anatuhumiwa kumuweka kimada mwanasiasa mwenzake mwanaume amabye anaaminika kuwa ni shoga na sasa anaelezwa kuwa karibu naye kama nyumba ndogo ya mheshimiwa huyo.Habari za muda mrefu zinaeleza kwamba mapenzi kati ya Waziri Mkuu huyo wa zamani na mwanasiasa huyo shoga si siri tena kwa wengi hali ambayo imeeleza kutishia hata ndoa yake.Imeelezwa kwamba kabla hata ya kuingia siasa mwanasiasa huyo shoga amekuwa na uhusiano wa muda mrefu na waziri mkuu huyo mstaafu tokea akiwa mtumishi wa taasisi moja ya serikali.
Habari zaidi zinaeleza kwamba mahusiano kati ya wanasiasa hao wawili yamekuwa yakiwakera hata baadhi ya marafiki wenzao wa karibu ambao wameelezwa kusikia kinyaa kutokana na mahusiano kati yao wakiwa watu wa jinsia moja.
Mwanasiasa mmoja aliye karibu na wapenzi hao wawili ameliambia gazeti hili kwamba kitendo hicho ni uchafu uliokithiri hasa kwa watu ambao wanapaswa kuwa mfano kwa jamii inayowazunguka."Inatia kinyaa maana huu ni uchafu uliokithiri kwa wanaume kuwa wapenzi tena bila hata aibu. Na kwa kuwa wanaogopwa najua hata wee hutaandiika" alisema mwanasiasa mmoja aliyeko Dodoma-------------------

nadhani wanawasingizia....wanakulana wao kwa wao..mnaikumbuka hii way back 2k9
 
Mie nipo hapa Dodoma,

Tangu waheshimiwa Wabunge waanze kuja Dodoma kwa kikao cha Bunge la Bajeti, kumekuwepo na ongezeko kubwa la mashangingi hasa nyakati za jioni kuja hapa chuo kikuu cha Dodoma na kuwachukua watoto na kuondoka nao. Wabunge wanawatuma madereva tu, wao hawaonekani!

Je hii ndo kazi ambayo wametumwa na wapiga kura wao? Na je kwanini wanawaharibia maisha watoto wa watu wakati wao wameoa na kuwa na familia zao? Kama wanahusudu sana Ngono kwanini wasije na wake zao?

Nawakilisha wadau!!!

Wanawaharibia maisha kivipi?,kwa uelewa wangu mtu akiwa chuoni ni mtu mzima so anajua anachofanya,pia hao viongozi nafikiri hawawakamati kwa nguvu hao mabinti,wanakuwa nao kwa maridhiano yao wenyewe?,au umenyang'anywa na mbunge?,mulaumu huyo msichana wako kuwa weak na kukuacha wewe na kumfuata mwenye nacho!

 
Wanawaharibia maisha kivipi?,kwa uelewa wangu mtu akiwa chuoni ni mtu mzima so anajua anachofanya,pia hao viongozi nafikiri hawawakamati kwa nguvu hao mabinti,wanakuwa nao kwa maridhiano yao wenyewe?,au umenyang'anywa na mbunge?,mulaumu huyo msichana wako kuwa weak na kukuacha wewe na kumfuata mwenye nacho!


Sure! Hakuna anayemshika mkono mtu au kumlazimisha, vinginevyo wangekwenda kushtaki
 
lakini kumbuka anaetoa huo Uzinzi ni mdada.........wadada wa siku hizi bana sio kama kipindi kile huwezi hangaika nae saaana just one day hata kama hamjawahi kutana nae UNAKULA MZIGO..... Hii ni mbaya sana dada anaangalia tu usafili na mfukoni kuna nini lakini hajui mwilini kuna wadudu gani

Kula mzigo ndo nini, I mean kwani yeye hakuli mzigo?
 
Wanawaharibia maisha kivipi?,kwa uelewa wangu mtu akiwa chuoni ni mtu mzima so anajua anachofanya,pia hao viongozi nafikiri hawawakamati kwa nguvu hao mabinti,wanakuwa nao kwa maridhiano yao wenyewe?,au umenyang'anywa na mbunge?,mulaumu huyo msichana wako kuwa weak na kukuacha wewe na kumfuata mwenye nacho!


Zamani watoto wa kike Kinadada Walijifunza kusema Noooooooo ,kwa sasa wengi juu ya paji la uso wameandikwa Ndio mbona unachelewa kusema.
 
Inasikitisha sana,wanavyuo tatizo wanatamaa tamaa na pesa na hii pia inatokana na hali ngumu ya maisha vyuoni fedha inayotolewa kwa siku haitoshi,KWA NINI WASIJIDANGANYIKE?
 
Back
Top Bottom