Kiswahili kinaweza kutumika ngazi zote bila shida ila ni mapemz sana kwa nchi kama yetu kutaka itambulike kwa lugha yake kimataifa na hvyo elimu yetu itatusaidia ndano ya nchi pekee na matokeo yake ni kunyanyasika katka soko.la ajira!
tanzania bado ni masikini na tegemezi sana hivyo uwezo wake kushawishi nchi nyingine kitumia lugha yake ni mdogo pia! nchi ambazo zinauchumi mzur zinaweza hata kutoa scholarship kwa nchi zingine kupata elimu kwa lugha yao ili kuongeza wigo wa matumozi ya lugha na utamaduni wao duniani, ila kwa tz sisi ni tegemezi hatuna jeuri hiyo!
kuna kitu kingine kilicholetwa bungeni na wazir wa elimu kuhusu kuifanya elimu ya form 4 kua elimu ya msingi na ya lazima, hili nalo ni jambo jema sana ila nalo bado ni mapema sana! shule zenyewe za sec hazitoshi, walimu hakuna na wanaoishia std 7 bado ni wengi sana, vp hali itakuaje kama wote wangetakuwa kwenda sec school? Me naona serikali inatakiwa kujipanga sana ili iweze kutekeleza jambo kama hili!