Wabunge, waziri watunishiana misuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge, waziri watunishiana misuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, May 27, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]Wabunge, waziri watunishiana misuli[/FONT]
  [FONT=&quot]* Ni Kabaka, Jenista Mhagama, Mbilinyi (Sugu)[/FONT]
  [FONT=&quot]* Wavutana katika kutembelea kiwanda[/FONT]
  [FONT=&quot]* Kiwandani wabunge washuhudia ‘madudu'[/FONT]
  [FONT=&quot]* Wafanyakazi wanalazimishwa kuvaa kaptura[/FONT]
  [FONT=&quot]* Wabunge watokwa machozi kwa waliyoyaona[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Na Arodia Peter[/FONT]
  [FONT=&quot]Dar es Salaam[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]WAZIRI wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Gaudensia Kabaka jana alivutana vikali na wabunge wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii waliokuwa wanataka kutembelea Kiwanda cha Vyombo vya Nyumbani cha Jambo Plastiki kilichoko Dar es Salaam.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Wakati wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa wamekwisha kujiandaa kwenda katika kiwanda hicho jana, ghafla Waziri Kabaka aliwaeleza kuwa ziara hiyo imeahirishwa hadi wakati mwingine.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kabaka alitoa sababu za kutaka kuahirisha ziara hiyo kuwa ni mgogoro wa wafanyakazi na mwajiri kiwandani hapo ambao upo mahakamani hivyo ziara hiyo itakuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Baada ya kutolewa taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jenista Mhagama alikuja juu na kumweleza Kabaka kuwa kamwe kamati yake haiwezi kuahirisha ziara hiyo bila kutolewa sababu za kuridhisha. Alisema kitendo alichokifanya Waziri kinadhalilisha kamati yake.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]"Mheshimiwa Waziri kitendo ulichokifanya unaingiza mgogoro mkubwa katika kamati ya Bunge… kwa mazingira ya sasa Watanzania hawana mahali popote pa kutolea shida zao zaidi ya bunge na hii inadhihirika wazi wataalamu wako hawakukushauri vizuri," alisema Mbunge huyo wa Peramiho kwa tiketi ya CCM na kuongeza:[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]"Basi kama ni hivyo, Mheshimiwa Waziri mimi nakupisha uwe mwenyekiti wa kamati ya Bunge maana naona hutaki kutuelewa."[/FONT]
  [FONT=&quot]Kuona hivyo, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alikwenda mbali zaidi kwa kusema kwa uzoefu uliopo nchini unaonyesha kuwa ziara hiyo tayari imekwicha kuchakachuliwa na wahusika kwa manufaa wanayoyajua wao.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Alisisitiza kwamba kama ziara itaahirishwa basi yeye hatakuwamo kwenye orodha hiyo.[/FONT]
  [FONT=&quot]Naye Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) alisema kama kamati haitaki kwenda kwenye kiwanda hicho yeye atapanga ziara yake kama mbunge wa Chadema na kwenda kusikiliza na kukagua mazingira kiwandani hapo.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Asumpta Nshunju (CCM) ambaye ni Mbunge wa Nkenge, alisema kuna dalili za wazi watu wamepokea chochote kutoka kwa mwekezaji ndiyo maana kamati imepigwa ‘stop' dakika za mwisho.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Akimsaidia waziri wake, Ofisa Kazi Mfawidhi wa Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Josephat Rugakingira aliwaambia wabunge kwamba haingekuwa vizuri kutembelea kiwanda hicho wakati mgogoro kati ya menejimenti na wafanyakazi bado uko Baraza la Usuluhishi wa Migogogro (CMA) ikiwa imefunguliwa kesi namba DMA/DSM/ILALA/ 2009.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo baada ya mvutano mkali hatimaye Waziri Kabaka alikubaliana na wabunge na kuamua kufanya ziara kiwandani hapo wakati huo ikiwa saa 7.00 mchana.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kiwandani[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Wabunge walipofika kiwandani walipangua ratiba iliyokuwa imeandaliwa iliyotaka wafanyakazi na menejimenti kukutana na kamati ya Bunge kwa pamoja.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kamati ya Bunge iliamua kukutana na wafanyakazi pekee, kikao kilichodumu kwa zaidi ya saa moja. Waandishi wa habari wa menejimenti hawakuruhusiwa katika kikao hicho.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Baada ya kumalizika kikao hicho, wabunge walitoka nje wakiwa wanafuta machozi na baadhi yao walisema waliingiwa na simanzi kubwa kutokana na mambo mazito waliyoelezwa katika kikao hicho.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo, ilibainika kuwa katika kikao hicho ambacho Waziri pia alishiriki, kesi iliyokuwa inasemwa kuwa ipo mahakamani haikuwa kweli kwa vile ilikwisha kutolewa uamuzi tangu mwaka 2009.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]"Hii kama siyo rushwa ni nini, ndiyo maana walitaka kutuchakachua tusije hapa kwa maslahi yao, hii ni aibu. Wataalamu wa Wizara ndiyo wanaotufanya sisi wabunge wa CCM tuonekane hatuna thamani mbele ya umma… kumbe ni watu wachache waliojiwekea mtandao wa rushwa kwa njia wanazozijua wao," alisema mmoja wa wabunge kwa sharti la kutotajwa jina.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Waziri Kabaka akiri, aiomba radhi kamati[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Baadaye Waziri Kabaka aliomba radhi kwa Kamati ya Bunge kutokana na hali iliyojitokeza awali. Alisema yeye hakujua kama alichoambiwa na wataalamu wa Wizara yake kilikuwa ni uongo na uzushi.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]"Mheshimiwa mwenyekiti naomba radhi kwa yaliyotokea, nakiri nilidanganywa sasa nimejifunza kutoka kwenu," alisema Kabaka kwa sauti ya upole.[/FONT]
  [FONT=&quot]Alipoulizwa na waandishi wa habari ni hatua gani atawachukulia wataalamu waliomdang'anya, alisema:[/FONT]
  [FONT=&quot]"Niachieni nitashughulika nao, tutaongea na wenzangu tuone ni kwa nini wamefanya hivyo".[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Wafanyakazi wanalazimishwa kuvaa kaptura[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kiwandani hapo wabunge walishuhudia wafanyakazi wakike na kiume wakiwa wamevaa kaptura na fulana ikiwa ndiyo sare za kiwanda hicho.[/FONT]
  [FONT=&quot]Wakizungumzia hali hiyo baadhi ya wafanyakazi walisema hawaruhusiwi kuvaa nguo tofauti na hizo kiasi kwamba wakati wa baridi wanapata shidakubwa lakini hawana la kufanya.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]"Hizi ndiyo nguo zetu rasmi hapa kazini. Tukivaa tofauti na hizi tunafukuzwa kazi, tunashukuru mmekuja wabunge wetu mtutetee tunaangamia," alisema mmoja wa wafanyakazi hao.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kwenye mgahawa wa wafanyakazi, hali pia ni mbaya na wabunge walishuhudia uchafu uliokithiri huku vyombo vya kulia chakula vikiwa vya plastiki jambo ambalo ni hatari kwa afya za wafanyakazi hao.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Baadhi ya wafanyakazi walisema licha ya kutumia vyombo vya plastiki pia wanalazimika kutumia vikombe kwa kupokezana kwa vile vilivyopo havitoshi.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]"Hata sisi tunaonekana kana mbwa, angalieni sehemu hii tunayolia chakula. Haifai hata kwa mnyama mbwa maana ni chafu kupindukia lakini hawatujali," walisema baadhi ya wafanyakazi.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Wafanyakazi wa kigeni[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Manoj Suchak aliulizwa kuhusu hatua ya kuajiri wafanyakazi wa kigeni katika nafasi zote za juu bila kuhusisha mfanyakazi mzawa hata mmoja.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Akijibu swali hilo lililoulizwa na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM), alisema kati ya mameneja saba wa kiwanda hicho ni watano tu ambao ni wazawa.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo Nkamia alipotaka amwone angalau mmoja ambaye ni mzawa, alitokea kijana mwenye asili ya Asia, jambo lililozua kicheko na miguno kutoka kwa wabunge.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Ziara hiyo ya wabunge ilikuwa pamoja na mambo mengine kukagua mazingira ya kiwanda, kusikiliza mgogoro baina ya wafanyakazi na manejimenti ya kiwanda hicho ambao umedumu kwa muda mrefu.[/FONT]
   
 2. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hao ndiyo wawekezaji wanaolindwa usiku na mchana na serikali ya CCM, huyo waziri kwa kuidanganya kamati ya bunge alitakiwa ajiuzulu pale pale. but not here in Tanzania.
   
 3. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kama ni wawekezaji wa namna hiyo basi wako wengi. Hiyo ni baadhi ya mambo ambayo mmeyasikia tembeleeni sehemu nyingine mkashudie mambo zaidi ya hayo kama kahama na kwingineko hasa mlipowapa kandalasi wachina na wahindi. Huyu Jk mi namshangaa kwa nini anan'gan'gania hawa wahindi na wachina wakati kwanza ni wajanja janja. Halafu anajua kabsa wanataka cheap labor kutoka Tanzania. Na nimemuona ameongozana na waziri mkuu wa India Hivi kuna matumaini hapo kweli. Baada ya miaka mingine mitano ya Jk sijajua vizuri tutakuwa wapi.

  PHP:
  NIMEWATOA HAPA NIKAWAFIKISHA PALE by JK Pof the United state of Tanzania
  .
   
 4. k

  kizazi kipya JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hii ndio serikali yetu...utakuta hata hao waliomdanganya waziri na kamati yake hawatachukuliwa hatua yoyote kwa uongo wao...hii ndio Tanzania.
   
 5. magessa78

  magessa78 JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimechoka jamani nimechokaaaaa....hivi kwa nini tume ya uchaguzi isiitshe uchaguzi sasa?!!!
   
 6. M

  Maga JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 325
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hivi watanzania tutajifunza lini kuwajibika? Kama waziri anakiri kuwa ameidanganya kamati kwa maelezo aliyopewa na maofisa wake je amewachukulia hatua gani maofisa hao?
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kusema huko nyuma kwamba Huyu Jennister Mhagama angefaa kabisa kuwa Spika wa bunge.
  Anaweza asiwe na elimu ya juu sana kwa maana ya VYETI lakini utendaji wake ni viwango vya juu kushinda hao wana-ccm wanaojiita wasomi. Kikao kilichopitaa aliongoza session na kwa kweli bunge lilionekana kuwa na hadhi. hata pale alipoona mbunge anakwenda kinyume na kanuni basi alimweleza mtoa hoja kwa style ya ustaarab na heshma.

  Sasa tunamwona anavyopambana na madudu wizara ya kazi. Watanzania wanaofanya kazi kwenye viwanda vya wenzetu wenye asili ya India hapa tanzania wanaangamia. Kuna udhalilishaji wa hali ya kutisha. hawana utu kabisa hawa waajiri. Na cha kushangaza zaidi ni kuwa kwenye management ni Wahindi toka India. Sijui Wizara ya Mambo ya ndani na Wizara ya Kazi wametoa vibali vya watu toka India kwa sababu zipi? Hata kwenye maduka, car show rooms ni India, Pakistan.

  Mawaziri vivuli LEMA na Regia Mtema angalieni hili kuna scandal za kutisha.
   
 8. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nafikiri SUGU nae afanye ziara kama mbunge wa chadema ili mambo mengi yawe hadharani. Hawa wanaoitwa wawekezaji wananyanyasa sana maskini wa Tanzania, si hapo tu na sehemu yoyote yenye wawekezaji walioajiri maskini wa Tanzania itembelewe.
   
 9. semango

  semango JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mhagama mhuni nae, asidanganye alikua hajui!
   
 10. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145

  Hapa tu mi binafsi nimejiskia kutokwa na machozi......!
  Ama kweli bora ukoloni wa bakora kuliko wa kiakili, maana ni rahisi kuhamasisha watawaliwa kwa ukombozi wao kuliko katika ukoloni wa kisaikologia......!
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaghrrrrrrrrrrrrrrr
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nadhani alipata fununu ndio maana akaamua kamati yake itembelee hicho kiwanda. Kumbuka viko viwanda vingi lakini kaenda huku na tayari unaweza kuona walakini maana waziri na wataalam wake wameonekana kumkinga mwenye kiwanda.
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Wataalam wake washapokea kitu kidogo na wanajua kuna kinachoendelea waziri badala ya kuwachukulia hatua anatoa bla bla zisizo na kichwa wala mguu
  Hii ni tanzania zaidi ya uijuavyo
   
 14. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  huyo josephat rugakingira na waziri kabaka ni kampuni moja ya rushwa co. ltd. hapo wizarani kwao. hakyanani ningekuwa rais wa nchi hii, sasa hivi wote wangeishaota sugu mattakoni kwa mboko za uhakika kabla sijawatimua kabisa serikalini kama sio kuwakolimba kabisa. nyamafu wakubwa hao!!
   
 15. b

  bartazary bon Member

  #15
  May 27, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimefuraishwa sana na habari hii hasa swala la ajira kwa wazawa hasa kakita sekta ya viwandani,Wabunge watusaidie hili kulipigia kelwle.
  Kwani wazawa hawapewi nafasi ili hali wana sifa na wanakidhi vigezo.kwa mfano pale SHELYS kiwandani mwenge wahindi wana fanya mpaka kazi za masoko(marketing).nenda huko kwenye masoko yani kwenye mahospitari,maduka ya madawa lazima utawaona kibao na mabegi yao kazi ambayo wazawa wanaiweza tu.Mamlaka husika wajua hili? na jua wanajua kwani ndio wanaotoa vibali
   
 16. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  CHADEMA nyie ndio tumaini la watanzania wanaoonewa na kudhurumiwa kiasi hiki TENA na wageni. Krunzi lenu linapaswa kukimulika kiwanda hicho! Tuangalie jinsi gani tunaweza kufanya mahojiano ya kina na wafanyakazi wa kiwanda hicho ili kuuanika uozo huu ambao hata Waziri alitaka kuukumbatia!
  Mapambano bado yanaendelea
  A luta continua
  The struggle continues
  PP DAIMA
   
 17. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #17
  May 27, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hapo waziri anapaswa kupeleka barua ya kujiuzulu kwa aliyemteua.
  huo ndo uwajibikaji
   
 18. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Sio tanzania hii mkuu labda izaliwe upya
   
 19. mkute

  mkute Member

  #19
  May 27, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Jamani hii serikali yetu ilishatuasi wananchi, haiko tena kwa maslahi ya wananchi, bali wako zaidi kwa ajili ya kuhakikisha masilahi ya wawekezaji yanalindwa, hamna haja kumshangaa waziri Kabaka kwani hiyo iko kwenye sera za uongozi wa ccm.Kama mtu haamini hilo si aone hata viongozi wa juu! president,p/minister ni nothing kwa kweli!
   
 20. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  yaani kwa kweli haya mambo yanasikitisha sana....lakini kwa nini watanzania tunakuwa watumwa ndani ya nchi yetu sababu ya viongozi wachache wasio kuwa na uzalendo....wananchi amkeni tuwang'oe hawa mafedhuli..kuna uonevu tunaofanyiwa watanzania sehemu mbalimbali but hakuna mtetezi zaidi ukiongea utaandamwa mpaka basi...wekeni tofauti za kisiasa pembeni kuikomboa hii nchi...umaskini sasa umekuwa jambo la kawaida while tuna rasilimali nyingi na wananufaika wageni na vibaraka wao wachache...
   
Loading...