Wabunge, waziri watunishiana misuli

Wabunge, waziri watunishiana misuli

mama wa utatu amekamatika.....hahahaha..
 
Waziri Kabaka akiri, aiomba radhi kamati

Baadaye Waziri Kabaka aliomba radhi kwa Kamati ya Bunge kutokana na hali iliyojitokeza awali. Alisema yeye hakujua kama alichoambiwa na wataalamu wa Wizara yake kilikuwa ni uongo na uzushi.

"Mheshimiwa mwenyekiti naomba radhi kwa yaliyotokea, nakiri nilidanganywa sasa nimejifunza kutoka kwenu," alisema Kabaka kwa sauti ya upole.


Hivi huyu Mama si kipindi cha pili hiki anakuwa Waziri! "eti nimejifunza kutoka kwenu" hujui nini kuhusu kutafuniwa chakula nakuwekewa mdomoni??? anataka kufanya watu wajinga, naamini alitaka kuihairisha hiyo ziara kwa sababu alizozijua, period! Inatia hasira na uchungu, kitaeleweka tu soon, saa ya ukombozi haiko mbali.
 
Hii Nadhan Limekaa Kiumbea Zaidi, Kwenye kila kiwanda kuna taratibu za Kufuata ili kuwe na Usalama eneo la Kazi!! Huwezi kujifunga Kanga wakati unapita maeneo yenye Mashine zinazozunguka kwa kasi kwani ni hatari!! Vazi la kazi nadhan ni utaratibu ambao upo kwa ajili ya usalama!! Kama walikuwa wanatakiwa wakae Uchi hapo ningeona kuna tatizo kubwa Zaidi, Pia uchafu eneo la kulia naona hili linachangiwa na wafanyakazi wenyewe!! Kwani unapopenda usafi wa mazingira unayokaa pia utapenda yawe safi!! Kwani hicho chakula wanchokula si kinaandaliwa na watu?? Sasa kwa nini wafanyakazi wasiwabane hao waandaaji wa chakula Wakaweka mazingira ya usafi Zaidi?
Kwa Hali ilivyo kwenye Nchii hii sasa naona hata usafi kwenye Vyoo vya public au sehemu za kazi tutaanza kuomba msaada kutoka kwa wafadhili na wahisani waweze Kutusaidia!!
Hitimisho:
Hapa mimi naona suala la msingi Hapa ni Huenda malipo wanayolipwa hayaendani na hali ngumu ya Maisha pamoja na kupanda kwake na sio Malalamiko hayo hapo juu kwani yote yapo katika uwezo wao!! Nawasilisha
 
Eh hii ndiyo Tz ya sasa, Enzi za Mwl huwezi kusikia upuuzi kama huu.

Hebu angalia Waziri anaulizwa: Utachukua hatua gani kwa watendaji wako wizarani waliokudanganya? JIBU: "Nitaongea nao nijue kwa nini walinidanganya". Huyo ni waziri mwenye dhamana, Eti "Tutaongea na wenzang tuone kwa nini wamefanya hivyo". Use less. Bado unajiita waziri, Mama heri urudi sekondari, tena safari hii siyo kama Headmistress, bali mwl wa kawaida, hutufai. Tunajua aliyekupa hiyo post hatakuchukulia hatua yoyote, sasa ni vizuri ukajiongeza. Yaani "Changanya na za kwako" kabla hujakumbwa na kashfa nyingi.
 
Huyo waziri Kabaka alitakiwa kujiuzuru kwa kuidanganya Kamati ya Bunge. Anatakiwa kumwajibisha huyo aliyemdanganya kisha na yeye ajiwajibishe. Huo ndiyo utawala bora. Ni kamati ngapi za Bunge zimeshadanganywa na hao mawaziri? Najua Nishati na Madini wameshadanganya mara kibao.
Hata sijui hizo semina elekezi wanafundishwa nini kuhusu utawala bora!!
 
Hao tunaowaita wataalamu wa wizara mbalimbali ndiyo mbwa wa mafisadi na wezi wakuu wa nchi hii.
Wengi wa wanaoitwa wataalamu wa serikali akili zao zimehasiwa na hao mafisadi na mara nyingine wako tayari kuona wazawa wanakufa kwa ajili ya kujipendekeza kwa wageni wanaoiba jasho la wazawa pamoja na raslimali za nchi yetu.
Ni muhimu tujue kuwa maana halisi ya uhuru wa Tanzania ni ustawi na kuheshimika kwa wazawa (weusi) kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni.
Ukweli utabaki pale pale kwamba kupigania uhuru hakukuwa kwa ajili ya watanzania wenye asili nyingine kama arabuni, asia, ulaya n.k, kwa kuwa wao hawakunyonywa na walikuwa katika tabaka lililokuwa linawanyonya weusi.
Tudumishe uhuru kwa kupambana na vibaraka wote walioajiriwa serikalini na hapo ndipo ustawi wa wazawa utakapoongeeka kasi.
 
Watanzania wenzangu nyie jitahidini tu kukaza mikanda yenu, viongozi wetu ndio kwanza wamegundua raha ya kuwanyonya watanzania wenzao kupitia watu wanaowekeza vijisenti kwao.
Wote tununue mikanda ya ngozi isiyokatika upesi.
 
Watanzania wenzangu nyie jitahidini tu kukaza mikanda yenu, viongozi wetu ndio kwanza wamegundua raha ya kuwanyonya watanzania wenzao kupitia watu wanaowekeza vijisenti kwao.
Wote tununue mikanda ya ngozi isiyokatika upesi.

Bro inaelekea umechoka sana na huu utawala mbovu eeh? Ila kila mtanzania anawajibu wa kulijenga taifa lake, ikiwa nipomoja na kuipinga serikali iliyoko madarakani kuondokam

Nakutafuta serikali nyingine ya kuwaongoza Watanzania wenzangu mungu awabariki sana na poleni sana msife moyo nchi ni yenu maamuzi yapo mikononi mwenu.
 
Uyo mama nimla rushwa! Fukuza kazi Rais huyo mama tatizo sana.
 
thread kama hz huwa znanfanya natoa machoz,mtu unakuwa mtumwa ndan ya nch yako,JAMAN KAMA NCH IMEUZWA TUAMBIWE ILI KILA MTU APEWE CHAKE NA TUJUE WENGINE CHA KUFANYA.HIVI VIONGOZ WAKUBWA WHY HAMPEND NCH YENU JAMAN?NDIO AJRA HZ?
 
Niliwahi kusema huko nyuma kwamba Huyu Jennister Mhagama angefaa kabisa kuwa Spika wa bunge.
Anaweza asiwe na elimu ya juu sana kwa maana ya VYETI lakini utendaji wake ni viwango vya juu kushinda hao wana-ccm wanaojiita wasomi. Kikao kilichopitaa aliongoza session na kwa kweli bunge lilionekana kuwa na hadhi. hata pale alipoona mbunge anakwenda kinyume na kanuni basi alimweleza mtoa hoja kwa style ya ustaarab na heshma.

Sasa tunamwona anavyopambana na madudu wizara ya kazi. Watanzania wanaofanya kazi kwenye viwanda vya wenzetu wenye asili ya India hapa tanzania wanaangamia. Kuna udhalilishaji wa hali ya kutisha. hawana utu kabisa hawa waajiri. Na cha kushangaza zaidi ni kuwa kwenye management ni Wahindi toka India. Sijui Wizara ya Mambo ya ndani na Wizara ya Kazi wametoa vibali vya watu toka India kwa sababu zipi? Hata kwenye maduka, car show rooms ni India, Pakistan.

Mawaziri vivuli LEMA na Regia Mtema angalieni hili kuna scandal za kutisha.

ni kweli mkuu huyo mhagama anafa tatizi alikuwa si mwana mtandao zen alikuwa kambi ya sumaye 2005 hope umenisoma mkuu
 
Back
Top Bottom