Wabunge watatu wa Viti Maalum CHADEMA watangaza kuachana na chama hicho na kujiunga CCM

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Wabunge watatu wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, Dkt. Immaculate Sware Semesi, Anna Gidarya na Latifa Chande wametangaza leo Bungeni kuondoka katika chama hicho na kujiunga na CCM.

Dkt. Immaculate Sware Semesi na Latifa Chande ni miongoni mwa Wabunge waliotakiwa kujieleza baada ya kukiuka agizo la kukaa CHADEMA kutoenda Bungeni na kukaa Karantini.

Eaj6ig3WoAEcPY8.jpg
Eaj6jueWAAEkS6U.jpg


Eaj6jJ0WoAMtY7W.jpg
 
Wabunge watatu wa Viti Maalum wa CHADEMA wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga Chama cha Mapinduzi (CCM). Wabunge hao ni Dkt. Immaculate Semesi, Anna Gidalia na Latifa Chande. Uamuzi huo umekuja siku moja kabla ya Bunge la 11 kufikia mwisho.
 
Wanawahi usajili ila yajayo yanafurahisha sana sana!

Ngoja ni mark sura zao maana hawatasikika tena
 
Back
Top Bottom