Wabunge wataka udini ukomeshwe

Mwambao

Member
Apr 11, 2011
22
6
WABUNGE wa Bunge la Tanzania wametaka tuhuma za kuwapo udini nchini ikiwa ni pamoja na ndani ya vyama vya siasa zishughulikiwe kwa kuchukuliwa hatua kuzikomesha.

Wakichangia Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Mwaka 2011/12 ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yaliyowasilishwa juzi na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, walisema udini huo ukiendelea kufumbiwa macho, nchi itafika pabaya.

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema), alisema "mimi ni kiongozi wa Kanisa Katoliki, viongozi wanazungumzia udini na tuhuma kwa baadhi ya vyama vya siasa nashangaa hawachukui hatua.

"Kama suala hili halishughulikiwi kikamilifu, huko mbele tutawatazama viongozi kwa mujibu wa dini zao, jambo hili ni baya kuliko maandamano ya Chadema ... kwa nini tuliowapa dhamana hawachukui hatua inaudhi ... Serikali ichukue hatua na suala hili lishughulikiwe haraka".

Mbunge wa Mbulu, Mustapha Akunaay(Chadema), alisema suala la udini liliibuka mwaka 1992 kulipoanza mfumo wa vyama vingi vya siasa kwa watu kuchanganya dini na siasa, lakini katika uchaguzi wa mwaka jana hali ilikuwa mbaya zaidi.

"Suala hilo limefikia pabaya hadi watu wanaogopa kusimamia dini zao na kulazimika kutoa salamu tatu za Asalaam aleykum, Bwana asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo. Serikali iliangalie hilo, ili watu warudi katika hali ya zamani hakukuwa na udini," alisema.

Mbunge wa Viti Maalumu, Zainab Kawawa (CCM), alisema "kwa sababu wenzangu wamezungumzia udini mimi nasema udini upo, tumeona Sumbawanga waumini 400 wa CCM wakitengwa na Kanisa Katoliki kwa sababu za kisiasa".

Akizungumzia utendaji wa watumishi wa umma, Selasini alisema Watanzania wengi wanaiibia Serikali kwa kutofanya kazi, lakini wanadai mshahara ambapo alifafanua:

"unawakuta wanatumia siku nzima kubishana mpira wa Simba na Yanga au wakati wa uchaguzi wanabishania vyama vya siasa, hadi wamegawanyika kwa vyama, mambo haya yanatia aibu … watumishi wafanye kazi.

"Hata hapa bungeni wapo wabunge wako nje hawafayi kazi, lakini baadaye wanataka mshahara".

Alisema, rushwa imekithiri hasa mahakamani na Polisi, lakini Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) inafumbia macho na kutolea mfano mahindi
yanasafirishwa kupitia Himo kutoka nchini kwenda Kenya, huku malori yakisindikizwa na polisi wa pikipiki wakiwa na silaha.

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), alisema tatizo la watuhumiwa wa rushwa kubwa kutochukuliwa hatua likiendelea bila kushitakiwa, wananchi watachoka na watachukua hatua ambazo hazijazoeleka.

Mbunge wa Viti Maalumu, Fakharia Shomari (CCM), alisema fomu za maadili ya viongozi zinazopelekwa Zanzibar hazifuatiliwi kama zinajazwa ambapo aliongeza: "Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais ni kubwa, wangeomba ofisi ili ofisa mmoja awepo pale kufuatilia kujazwa kwa fomu hizo".
Chanzo: Habari leo
 
Wabunge mbona mumesahau na kale ka MOU kamradi ka kanisa katoliki cha kufyonza pesa serikalini kwenda kanisani huo ndio udini wenyewe
 
Wabunge mbona mumesahau na kale ka MOU kamradi ka kanisa katoliki cha kufyonza pesa serikalini kwenda kanisani huo ndio udini wenyewe

Your own Ilussion- nothing of this kind- do not try to misleed others for your own interest!!!
 
cover.jpg
2-1.jpg
MEMO3.jpg
4.jpg
tano.jpg
sita.jpg
saba.jpg
 
Na BAKWATA ilianzishwa kwa masilahi ya nani?
MOU katika ya kanisa na serikali, matunda yake tunayaona
vyuo, mahospitali na mashule
Acha mawazo mgando wewe.
Wabunge mbona mumesahau na kale ka MOU kamradi ka kanisa katoliki cha kufyonza pesa serikalini kwenda kanisani huo ndio udini wenyewe
 
Yeah huo mjadala na upuuzi juu ya udini ukomeshwe, watu wa magamba wanadhan ndio SERA YA KUNADI. Hawana jipya!
 
Na BAKWATA ilianzishwa kwa masilahi ya nani?
MOU katika ya kanisa na serikali, matunda yake tunayaona
vyuo, mahospitali na mashule
Acha mawazo mgando wewe.

Hapo jibu lake ni kuwa.
BAKWATA ilianzishwa kwa maslahi ya J K Nyerere kwa nia na madhumuni ya kudhibiti maendeleo ya waislam na waislam wenyewe.
Na ukitaka kujua hili zaidi pitia kijitabu cha "" Kanisa Katoliki na siasa za Tanzania Bara 1953-1085""kilichoandikwa na Padre John c. Sivalon
 
Hapo jibu lake ni kuwa.
BAKWATA ilianzishwa kwa maslahi ya J K Nyerere kwa nia na madhumuni ya kudhibiti maendeleo ya waislam na waislam wenyewe.
Na ukitaka kujua hili zaidi pitia kijitabu cha "" Kanisa Katoliki na siasa za Tanzania Bara 1953-1085""kilichoandikwa na Padre John c. Sivalon
naona mashabiki wa hunga kapungu mmeibukia huku na data zake za chooni.
wajinga ndio waliwao huyo kapungu ni mchonganishi na katika waislamu anaowapata ni wale ambao elimu imewapita kando ili kuthibitisha hili pitisha sensa ya wanaohudhuria mkutano wake mtakuta ni walewale madrasa.
 
Zainab Kawawa anaongelea kitu ambacho hajui. Hao wana CCM walifungiwa baada ya kudharirisha msingi mkubwa wa Imani wakatoliki tunaita UTATU MTAKATIFU. Naamini kitendo walichofanya wangekua ndugu zetu Waislamu moto ungewaka Sumbawanga na pengine Tanzania nzima.
 
kama ni upuuzi basi umeanzia bungeni na Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema), alisema "mimi ni kiongozi wa Kanisa Katoliki, viongozi
Yeah huo mjadala na upuuzi juu ya udini ukomeshwe, watu wa magamba wanadhan ndio SERA YA KUNADI. Hawana jipya!
 
Waislamu wanazunguka nchi zima sasa hivi wanataka katiba mpya iwe na kadhi anayetambuliwa na kulipiwa na serikali sasa hapa utakomeshaje uduni
 
Waaambieni hao WABUNGE waache kutumia Biblia na Koran wanapo apishwa. Kama wanayo hiyo jeuri, basi tutawasikiliza.
 
Watu wanaoeneza udini kwa kasi ni ndugu zetu waislam kwa kutaka vya serikali vichanganywe na wao mf kadhi,halafu kuwe na salamu maalum ya watu wa serikali mf Salam ndugu wananchi basi kuliko asalam aleykum na blahblah nyingine
 
Wakulu, usiasa ndio hatari kwa Tanzania.

Tumeona jinsi usiasa ulivyo tumiwa na serikali huko Arusha na mikoa mingine kiasi cha kusababisha vifo vya bin adam. Bado sijaona madhara ya udini. MADHARA so far yako kwenye USIASA ambao kila kukicha unapoteza maisha ya watu na kuongeza murka kwa watanzania.
 
Back
Top Bottom