WABUNGE WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA WAMELIOMBA BUNGELA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAIHALALISHWE BADALA YA KUENDELA KUIPIGA VITA....MBUNGE WA MAKETE DK MAHENGE ALIHOJI KWANINI SERIKALI INAIPIGA VITA WAKATI ZIPO BAADHI YA POMBE AMBAZO NI KALI ZAIDI YA GONGO....AKINUKULIWA ALISEMA KAMA SIKOSEI WAKATI KIWANDA CHA KONYAGI KIKANZISHWA MOJA YA DHUMUNI LAKE NI KUKUSANYA GONGO ZOTE MA KUTENGENEZA KONYAGI...ALISEMA MWANASIA HUYO NA KUSHANGILIWA NA BUNGE ZIMA......MBUNGE HUYO ALISEMA HIVYO BAADA YA MB MARTHA KUULIZA SERIKALI WANAMPANGO GANI KUTOKOMEZA POMBE HIYO.....LOH GONGO MAMA UMECHEMSHA......
ZIPO POMBE KALI KAMA VODKA NA NINMGINE NI HALALI KAMA NA ZINAENDELEA KUUZWA HADHARANI IWEJE GONGO IHALALISHWE?????ALIHOJI DK MAHENGE....
kada mpinzani upo,....naona wanazidi kukulinda
GONGO HARAMU HARWAMU??????????
Two Wrongs don't make it right. Mheshimiwa Dr. Mahenge, ingekuwa vema ukasisitiza mambo yanayowasaidia wananchi. Pombe vijijini kwa ujumla zinatakiwa ziwe controlled zaidi maana zinaharibu wengi vijijini.
alikuwa anahoji uhalali wa vinywaji vingine vikali dhidi ya gongo,je wewe unaonaje kama kuna vinywaji vikali zaidi ya gongo vi halali kunywewa kisha gongo si halali?
Mambo yanayo saidia watu ni pamoja na pombe kama mimi imenisaidia ila kama utapitisha kiwango too much of anything is harmful msemo huu utahusika,kwa hiyo hilo ni swala la individual who use that stuff to control oneself.Kama ukinywa hata kidogo ni tatizo kwako basi chukulia kama ni allergic food to you don't take it.Kama vile unavyokwepa chakula kinachokuzuru AKA allergic food
Kila jambo linamuda wake wa kujadiliwa ndugu kama ulikuwa ni wakati wa kujadili pombe basi wacha wajadili hilo ,usiite mambo yasionamaana.
Nakumbuka kampeni za uchaguzi wa mwaka 1995 Mrema kama kawaida yake akiwa mgombea wa kiti cha urais kupitia NCCR Mageuzi,akiwa Bukoba aliwambia kwamba akichaguliwa kuwa rais wa TZ ataruhusu gongo kiwe kinywaji halali.Alishangiliwa kwa nguvu na wananchi hao.
Mimi nakubaliana na wabunge kwa sababu gongo imepigwa vita miaka na miaka lakini mpaka leo watu bado wanakunywa gongo.Kimsingi Gongo ni kali tena sana tu na wala sio pombe ya kufanyia masiala hata kidogo.Naunga mkono pombe hii iruhusiwe isipokua watumiaji wa pombe hiyo waelimishwe juu ya matumizi yake na kwa kiasi gani mtu anaweza kutumia bila kuwepo kwa athari yoyote.Vilevile watumiaji waelimishwe juu ya vyakula wanavyopaswa kuvitumia au kuvila kila watumiapo pombe hiyo kali.
Kuruhusiwa kwa pombe hiyo kutapunguza matukio ya rushwa hapa TZ kwani polisi wengi sana wanafuatilia hawa wapika gongo na wakiwakamata wanaishia kuchukua kitu kidogo.Kama tunaweza kufuta adhabu ya kunyongwa vipi kama tutaruhusu au kuhalalisha matumizi ya gongo.Naamini watu hawa wakiruhusiwa kutumia gongo watakua waangalifu sana kwa sababu watakua na uhakika wa kupatikana kwa pombe hiyo tofauti na sasa wanaitumia kwa kujificha.
alikuwa anahoji uhalali wa vinywaji vingine vikali dhidi ya gongo,je wewe unaonaje kama kuna vinywaji vikali zaidi ya gongo vi halali kunywewa kisha gongo si halali?